1 Samweli 27 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Samweli 27 (Swahili) 1st Samuel 27 (English)

Ndipo Daudi aliposema moyoni mwake, Siku moja, basi, mimi nitaangamia kwa mkono wa Sauli; hakuna jema zaidi kwangu kuliko kukimbia mpaka nchi ya Wafilisti; naye Sauli atakata tamaa kwa habari yangu, asinitafute tena mipakani mwote mwa Israeli; hivyo nitaokoka katika mikono yake. 1 Samweli 27:1

David said in his heart, I shall now perish one day by the hand of Saul: there is nothing better for me than that I should escape into the land of the Philistines; and Saul will despair of me, to seek me any more in all the borders of Israel: so shall I escape out of his hand.

Basi Daudi akaondoka, yeye na hao watu mia sita aliokuwa nao, akamvukia Akishi, mwana wa Maoki, mfalme wa Gathi. 1 Samweli 27:2

David arose, and passed over, he and the six hundred men who were with him, to Achish the son of Maoch, king of Gath.

Daudi akakaa huko Gathi pamoja na Akishi, yeye na watu wake, kila mtu na watu wa nyumbani mwake; Daudi naye alikuwa na wakeze wawili, Ahinoamu wa Yezreeli, na Abigaili wa Karmeli, aliyekuwa mkewe Nabali. 1 Samweli 27:3

David lived with Achish at Gath, he and his men, every man with his household, even David with his two wives, Ahinoam the Jezreelitess, and Abigail the Carmelitess, Nabal's wife.

Naye Sauli akaambiwa ya kwamba Daudi amekimbia mpaka Gathi; wala hakumtafuta tena. 1 Samweli 27:4

It was told Saul that David was fled to Gath: and he sought no more again for him.

Daudi akamwambia Akishi, Sasa kama nimeona kibali machoni pako na nipewe mahali katika miji hii mmojawapo mashambani, nipate kukaa huko; mbona mtumwa wako akae katika mji wa kifalme pamoja na wewe? 1 Samweli 27:5

David said to Achish, If now I have found favor in your eyes, let them give me a place in one of the cities in the country, that I may dwell there: for why should your servant dwell in the royal city with you?

Ndipo Akishi akampa Siklagi siku ile; kwa sababu hiyo huo mji wa Siklagi ni mali ya wafalme wa Yuda hata hivi leo. 1 Samweli 27:6

Then Achish gave him Ziklag that day: why Ziklag pertains to the kings of Judah to this day.

Na hesabu ya siku alizokaa Daudi katika nchi ya Wafilisti ilikuwa mwaka mzima na miezi minne. 1 Samweli 27:7

The number of the days that David lived in the country of the Philistines was a full year and four months.

Naye Daudi na watu wake walikuwa wakikwea na kuwashambulia Wageshuri, na Wagirizi, na Waamaleki waliokuwa wenyeji wa nchi hiyo, tangu Telemu, hapo uendapo Shuri, hata mpaka nchi ya Misri. 1 Samweli 27:8

David and his men went up, and made a raid on the Geshurites, and the Girzites, and the Amalekites; for those [nations] were the inhabitants of the land, who were of old, as you go to Shur, even to the land of Egypt.

Tena Daudi akaipiga nchi hiyo, asimhifadhi hai mume wala mke, akateka nyara kondoo, na ng'ombe, na punda, na ngamia na mavazi; kisha akarejea na kufika kwa Akishi. 1 Samweli 27:9

David struck the land, and saved neither man nor woman alive, and took away the sheep, and the oxen, and the donkeys, and the camels, and the clothing; and he returned, and came to Achish.

Naye Akishi humwuliza, Je! Mmeshambulia upande gani leo? Na Daudi husema, Juu ya Negebu ya Yuda, au, juu ya Negebu ya Wayerameeli, au, juu ya Negebu ya Wakeni. 1 Samweli 27:10

Achish said, Against whom have you made a raid today? David said, Against the South of Judah, and against the South of the Jerahmeelites, and against the South of the Kenites.

Tena Daudi hakumhifadhi hai mume wala mke, ili kuwaleta Gathi maana alisema, Wasituchongee kusema, Ndivyo alivyofanya Daudi, tena ndivyo ilivyokuwa desturi yake wakati wote alipokaa katika nchi ya Wafilisti. 1 Samweli 27:11

David saved neither man nor woman alive, to bring them to Gath, saying, Lest they should tell of us, saying, So did David, and so has been his manner all the while he has lived in the country of the Philistines.

Hivyo Akishi akamsadiki Daudi, akasema, Amewachukiza kabisa hao watu wake Israeli; kwa hiyo atakuwa mtumishi wangu hata milele. 1 Samweli 27:12

Achish believed David, saying, He has made his people Israel utterly to abhor him; therefore he shall be my servant forever.