1 Wathesalonike 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wathesalonike 2 (Swahili) 1st Thessalonians 2 (English)

Maana ninyi wenyewe, ndugu, mwakujua kuingia kwetu kwenu, ya kwamba hakukuwa bure; 1 Wathesalonike 2:1

For you yourselves know, brothers, our visit to you wasn't in vain,

lakini tukiisha kuteswa kwanza na kutendwa jeuri, kama mjuavyo, katika Filipi, twalithubutu katika Mungu kuinena Injili ya Mungu kwenu, kwa kuishindania sana. 1 Wathesalonike 2:2

but having suffered before and been shamefully treated, as you know, at Philippi, we grew bold in our God to tell you the Gospel of God in much conflict.

Kwa maana maonyo yetu siyo ya ukosefu, wala ya uchafu, wala ya hila; 1 Wathesalonike 2:3

For our exhortation is not of error, nor of uncleanness, nor in deception.

bali kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuwekewe amana Injili, ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wanadamu, bali wampendezao Mungu anayetupima mioyo yetu. 1 Wathesalonike 2:4

But even as we have been approved by God to be entrusted with the Gospel, so we speak; not as pleasing men, but God, who tests our hearts.

Maana hatukuwa na maneno ya kujipendekeza wakati wo wote, kama mjuavyo, wala maneno ya juujuu ya kuficha choyo; Mungu ni shahidi. 1 Wathesalonike 2:5

For neither were we at any time found using words of flattery, as you know, nor a cloak of covetousness (God is witness),

Hatukutafuta utukufu kwa wanadamu, wala kwenu, wala kwa wengine tulipokuwa tukiweza kuwalemea kama mitume wa Kristo; 1 Wathesalonike 2:6

nor seeking glory from men (neither from you nor from others), when we might have claimed authority as apostles of Christ.

bali tulikuwa wapole katikati yenu, kama vile mlezi awatunzavyo watoto wake mwenyewe. 1 Wathesalonike 2:7

But we were gentle among of you, as when a nurse cherishes her own children.

Vivyo hivyo nasi tukiwatumaini kwa upendo mwingi, tuliona furaha kuwapa, si Injili ya Mungu tu, bali na roho zetu pia, kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu. 1 Wathesalonike 2:8

Even so, affectionately longing for you, we were well pleased to impart to you, not the Gospel of God only, but also our own souls, because you had become very dear to us.

Maana, ndugu, mnakumbuka taabu yetu na masumbufu yetu; kwa kuwa mchana na usiku tulifanya kazi tusije tukamlemea mtu wa kwenu awaye yote, tukawahubiri hivi Injili ya Mungu. 1 Wathesalonike 2:9

For you remember, brothers, our labor and travail; for working night and day, that we might not burden any of you, we preached to you the Gospel of God.

Ninyi ni mashahidi, na Mungu pia, jinsi tulivyokaa kwenu ninyi mnaoamini, kwa utakatifu, na kwa haki, bila kulaumiwa; 1 Wathesalonike 2:10

You are witnesses with God, how holy, righteously, and blamelessly we behaved ourselves toward you who believe.

vile vile, kama mjuavyo, jinsi tulivyomwonya kila mmoja wenu kama baba awaonyavyo watoto wake mwenyewe, tukiwatia moyo na kushuhudia; 1 Wathesalonike 2:11

As you know how we exhorted, comforted, and implored every one of you, as a father does his own children,

ili mwenende kama ilivyo wajibu wenu kwa Mungu, mwenye kuwaita ninyi ili mwingie katika ufalme wake na utukufu wake. 1 Wathesalonike 2:12

to the end that you should walk worthily of God, who calls you into his own Kingdom and glory.

Kwa sababu hiyo sisi nasi twamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kweli kweli; litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini. 1 Wathesalonike 2:13

For this cause we also thank God without ceasing, that, when you received from us the word of the message of God, you accepted it not as the word of men, but, as it is in truth, the word of God, which also works in you who believe.

Maana ninyi, ndugu, mlikuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyo katika Uyahudi, katika Kristo Yesu; kwa kuwa mlipata mateso yale yale kwa watu wa taifa lenu wenyewe, waliyoyapata na hao kwa Wayahudi; 1 Wathesalonike 2:14

For you, brothers, became imitators of the assemblies of God which are in Judea in Christ Jesus; for you also suffered the same things from your own countrymen, even as they did from the Jews;

ambao walimwua Bwana Yesu, na hao manabii, na kutuudhi sisi; wala hawampendezi Mungu, wala hawapatani na watu wo wote; 1 Wathesalonike 2:15

who killed both the Lord Jesus and their own prophets, and drove us out, and didn't please God, and are contrary to all men;

huku wakituzuia tusiseme na Mataifa wapate kuokolewa; ili watimize dhambi zao siku zote. Lakini hasira imewafikia hata mwisho. 1 Wathesalonike 2:16

forbidding us to speak to the Gentiles that they may be saved; to fill up their sins always. But wrath has come on them to the uttermost.

Lakini sisi, ndugu, tukiwa tumefarakana nanyi kwa kitambo, kwa uso si kwa moyo, tulizidi kutamani kwa shauku nyingi kuwaona nyuso zenu. 1 Wathesalonike 2:17

But we, brothers, being bereaved of you for a short season, in presence, not in heart, tried even harder to see your face with great desire,

Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, mara ya kwanza, na mara ya pili, na Shetani akatuzuia. 1 Wathesalonike 2:18

because we wanted to come to you--indeed, I, Paul, once and again-- but Satan hindered us.

Maana tumaini letu, au furaha yetu, au taji ya kujionea fahari, ni nini? Je! Si ninyi, mbele za Bwana wetu Yesu, wakati wa kuja kwake? 1 Wathesalonike 2:19

For what is our hope, or joy, or crown of rejoicing? Isn't it even you, before our Lord Jesus{TR adds "Christ"} at his coming?

Maana ninyi ndinyi utukufu wetu, na furaha yetu. 1 Wathesalonike 2:20

For you are our glory and our joy.