2 Wathesalonike 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wathesalonike 2 (Swahili) 2dThessalonians 2 (English)

Basi, ndugu, tunakusihini, kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake, 2 Wathesalonike 2:1

Now, brothers, concerning the coming of our Lord Jesus Christ, and our gathering together to him, we ask you

kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msisitushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo. 2 Wathesalonike 2:2

not to be quickly shaken in your mind, nor yet be troubled, either by spirit, or by word, or by letter as from us, saying that the day of Christ had come.

Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; 2 Wathesalonike 2:3

Let no one deceive you in any way. For it will not be, unless the departure comes first, and the man of sin is revealed, the son of destruction,

yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu. 2 Wathesalonike 2:4

he who opposes and exalts himself against all that is called God or that is worshiped; so that he sits as God in the temple of God, setting himself up as God.

Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo? 2 Wathesalonike 2:5

Don't you remember that, when I was still with you, I told you these things?

Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake. 2 Wathesalonike 2:6

Now you know what is restraining him, to the end that he may be revealed in his own season.

Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa. 2 Wathesalonike 2:7

For the mystery of lawlessness already works. Only there is one who restrains now, until he is taken out of the way.

Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake; 2 Wathesalonike 2:8

Then the lawless one will be revealed, whom the Lord will kill with the breath of his mouth, and bring to nothing by the brightness of his coming;

yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo; 2 Wathesalonike 2:9

even he whose coming is according to the working of Satan with all power and signs and lying wonders,

na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa. 2 Wathesalonike 2:10

and with all deception of wickedness for those who are being lost, because they didn't receive the love of the truth, that they might be saved.

Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo; 2 Wathesalonike 2:11

Because of this, God sends them a working of error, that they should believe a lie;

ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu. 2 Wathesalonike 2:12

that they all might be judged who didn't believe the truth, but had pleasure in unrighteousness.

Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, ndugu mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli; 2 Wathesalonike 2:13

But we are bound to always give thanks to God for you, brothers loved by the Lord, because God chose you from the beginning for salvation through sanctification of the Spirit and belief in the truth;

aliyowaitia ninyi kwa injili yetu, ili kuupata utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo. 2 Wathesalonike 2:14

to which he called you through our Gospel, for the obtaining of the glory of our Lord Jesus Christ.

Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu. 2 Wathesalonike 2:15

So then, brothers, stand firm, and hold the traditions which you were taught by us, whether by word, or by letter.

Na Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe, na Mungu Baba yetu, aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema, 2 Wathesalonike 2:16

Now our Lord Jesus Christ himself, and God our Father, who loved us and gave us eternal comfort and good hope through grace,

awafariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika kila neno na tendo jema. 2 Wathesalonike 2:17

comfort your hearts and establish you in every good work and word.