2 Wafalme 4 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wafalme 4 (Swahili) 2nd Kings 4 (English)

Basi, mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wana wa manabii alimlilia Elisha, akasema, Mtumishi wako mume wangu amekufa; nawe unajua ya kuwa mtumishi wako alikuwa mcha Bwana; na aliyemwia amekuja ili ajitwalie wana wangu wawili kuwa watumwa. 2 Wafalme 4:1

Now there cried a certain woman of the wives of the sons of the prophets to Elisha, saying, Your servant my husband is dead; and you know that your servant did fear Yahweh: and the creditor is come to take to him my two children to be bondservants.

Elisha akamwambia, Nikufanyie nini? Niambie; una kitu gani nyumbani? Akasema, Mimi mjakazi wako sina kitu nyumbani, ila chupa ya mafuta. 2 Wafalme 4:2

Elisha said to her, What shall I do for you? tell me; what have you in the house? She said, Your handmaid has nothing in the house, except a pot of oil.

Akasema, Nenda, ukatake vyombo huko nje kwa jirani zako wote, vyombo vitupu; wala usitake vichache. 2 Wafalme 4:3

Then he said, Go, borrow you vessels abroad of all your neighbors, even empty vessels; borrow not a few.

Kisha uingie ndani, ukajifungie mlango wewe na wanao, ukavimiminie mafuta vyombo vile vyote; navyo vilivyojaa ukavitenge. 2 Wafalme 4:4

You shall go in, and shut the door on you and on your sons, and pour out into all those vessels; and you shall set aside that which is full.

Basi akamwacha, akajifungia mlango yeye na wanawe; hao wakamletea vile vyombo, na yeye akamimina. 2 Wafalme 4:5

So she went from him, and shut the door on her and on her sons; they brought [the vessels] to her, and she poured out.

Ikawa, vilipokwisha kujaa vile vyombo, akamwambia mwanawe, Niletee tena chombo. Akamwambia, Hakuna tena chombo. Mafuta yakakoma. 2 Wafalme 4:6

It happened, when the vessels were full, that she said to her son, Bring me yet a vessel. He said to her, There isn't another vessel. The oil stayed.

Ndipo akaja akamwambia yule mtu wa Mungu. Naye akasema, Enenda ukayauze mafuta haya, uilipe deni yako; nayo yaliyosalia uyatumie wewe na watoto wako. 2 Wafalme 4:7

Then she came and told the man of God. He said, Go, sell the oil, and pay your debt, and live you and your sons of the rest.

Hata ikawa siku moja, Elisha alikwenda Shunemu; na huko kulikuwa na mwanamke mmoja mwenye cheo; naye akamshurutisha aje ale chakula. Ikawa kila alipopita njia ile, huingia kula chakula. 2 Wafalme 4:8

It fell on a day, that Elisha passed to Shunem, where was a great woman; and she constrained him to eat bread. So it was, that as often as he passed by, he turned in there to eat bread.

Yule mwanamke akamwambia mumewe, Tazama, mimi naona ya kuwa mtu huyu apitaye kwetu mara kwa mara ni mtu mtakatifu wa Mungu. 2 Wafalme 4:9

She said to her husband, See now, I perceive that this is a holy man of God, that passes by us continually.

Nakuomba, tumfanyie chumba kidogo ukutani; na ndani yake tumwekee kitanda, na meza, na kiti, na kinara cha taa; na itakuwa, atujiapo, ataingia humo. 2 Wafalme 4:10

Let us make, Please, a little chamber on the wall; and let us set for him there a bed, and a table, and a seat, and a lamp stand: and it shall be, when he comes to us, that he shall turn in there.

Ikawa siku moja akafika huko, akaingia katika chumba kile akalala. 2 Wafalme 4:11

It fell on a day, that he came there, and he turned into the chamber and lay there.

Akamwambia Gehazi mtumishi wake, Mwite yule Mshunami. Naye alipokwisha kuitwa, akasimama mbele yake. 2 Wafalme 4:12

He said to Gehazi his servant, Call this Shunammite. When he had called her, she stood before him.

Akamwambia, Sema naye sasa, Tazama, wewe umetutunza sana namna hii; utendewe nini basi? Je! Uombewe neno kwa mfalme, au kwa amiri wa jeshi? Yule mwanamke akamjibu, Mimi ninakaa katika watu wangu mwenyewe. 2 Wafalme 4:13

He said to him, Say now to her, Behold, you have been careful for us with all this care; what is to be done for you? would you be spoken for to the king, or to the captain of the host? She answered, I dwell among my own people.

Akasema, Basi, atendewe nini? Gehazi akajibu, Hakika hana mwana, na mumewe ni mzee. 2 Wafalme 4:14

He said, What then is to be done for her? Gehazi answered, Most assuredly she has no son, and her husband is old.

Akamwambia, Kamwite. Naye alipokwisha kuitwa, akasimama mlangoni. 2 Wafalme 4:15

He said, Call her. When he had called her, she stood in the door.

Akasema, Panapo wakati huu mwakani, utamkumbatia mwana. Akasema, La! Bwana wangu, wewe mtu wa Mungu, usiniambie mimi mjakazi wako uongo. 2 Wafalme 4:16

He said, At this season, when the time comes round, you shall embrace a son. She said, No, my lord, you man of God, do not lie to your handmaid.

Yule mwanamke akachukua mimba, akazaa mtoto mume wakati uo huo mwakani, kama Elisha alivyomwambia. 2 Wafalme 4:17

The woman conceived, and bore a son at that season, when the time came round, as Elisha had said to her.

Hata yule mtoto alipokua, ikawa siku moja alitoka kwenda kwa baba yake kwenye wavunao. 2 Wafalme 4:18

When the child was grown, it fell on a day, that he went out to his father to the reapers.

Akamwambia baba yake, Kichwa changu! Kichwa changu! Naye akamwambia mtumishi wake, Mchukue kwa mama yake. 2 Wafalme 4:19

He said to his father, My head, my head. He said to his servant, Carry him to his mother.

Akamchukua, akampeleka kwa mama yake, naye akakaa magotini mwake hata adhuhuri, kisha akafa. 2 Wafalme 4:20

When he had taken him, and brought him to his mother, he sat on her knees until noon, and then died.

Mamaye akapanda juu, akamlaza juu ya kitanda cha yule mtu wa Mungu, akamfungia mlango, akatoka. 2 Wafalme 4:21

She went up and laid him on the bed of the man of God, and shut [the door] on him, and went out.

Kisha akamwita mumewe, akasema, Tafadhali, uniletee mtu mmoja wa watumishi, na punda mmoja, ili nimwendee yule mtu wa Mungu kwa haraka, nikarudi tena. 2 Wafalme 4:22

She called to her husband, and said, Please send me one of the servants, and one of the donkeys, that I may run to the man of God, and come again.

Akasema, Kwa nini kumwendea leo? Sio mwandamo wa mwezi, wala sabato. Akasema, Si neno. 2 Wafalme 4:23

He said, Why will you go to him today? it is neither new moon nor Sabbath. She said, It shall be well.

Akatandika punda, akamwambia mtumishi wake, Mwendeshe, twendelee mbele. Usinipunguzie mwendo, nisipokuambia. 2 Wafalme 4:24

Then she saddled a donkey, and said to her servant, Drive, and go forward; don't slacken me the riding, except I bid you.

Basi akaenda, akafika kwa yule mtu wa Mungu, katika mlima wa Karmeli. Ikawa, yule mtu wa Mungu alipomwona kwa mbali, akamwambia Gehazi mtumishi wake, Tazama, Mshunami yule kule. 2 Wafalme 4:25

So she went, and came to the man of God to Mount Carmel. It happened, when the man of God saw her afar off, that he said to Gehazi his servant, Behold, yonder is the Shunammite:

Tafadhali piga mbio sasa kwenda kumlaki, ukamwambie, Hujambo? Mume wako hajambo? Mtoto hajambo? Akajibu, Hawajambo. 2 Wafalme 4:26

please run now to meet her, and ask her, Is it well with you? is it well with your husband? is it well with the child? She answered, It is well.

Naye alipofika kwa yule mtu wa Mungu kilimani, alimshika miguu. Gehazi akakaribia amwondoe; lakini mtu wa Mungu akamwambia, Mwache; maana roho yake ndani yake ina uchungu; na Bwana amenificha, wala hakuniambia. 2 Wafalme 4:27

When she came to the man of God to the hill, she caught hold of his feet. Gehazi came near to thrust her away; but the man of God said, Let her alone: for her soul is vexed within her; and Yahweh has hid it from me, and has not told me.

Yule mwanamke akasema, Je! Naliomba mwana kwa bwana wangu? Mimi sikusema, Usinidanganye? 2 Wafalme 4:28

Then she said, Did I desire a son of my lord? Didn't I say, Do not deceive me?

Ndipo Elisha akamwambia Gehazi, Jikaze viuno, ukachukue fimbo yangu mkononi mwako, ukaende zako; ukikutana na mtu, usimsalimu; na mtu akikusalimu, usimjibu; ukaweke fimbo yangu juu ya uso wa mtoto. 2 Wafalme 4:29

Then he said to Gehazi, Gird up your loins, and take my staff in your hand, and go your way: if you meet any man, Don't greet him; and if anyone greets you, don't answer him again: and lay my staff on the face of the child.

Na mama yake yule mtoto akasema, Kama Bwana aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha. Basi akaondoka, akamfuata. 2 Wafalme 4:30

The mother of the child said, As Yahweh lives, and as your soul lives, I will not leave you. He arose, and followed her.

Na Gehazi akawatangulia, akaiweka ile fimbo juu ya uso wa mtoto; lakini hapakuwa na sauti, wala majibu. Basi akarudi ili kumlaki, akamwambia, akisema, Mtoto hakuamka. 2 Wafalme 4:31

Gehazi passed on before them, and laid the staff on the face of the child; but there was neither voice, nor hearing. Therefore he returned to meet him, and told him, saying, The child has not awakened.

Basi Elisha alipofika nyumbani, tazama, mtoto amekwisha kufa, amelazwa kitandani pake. 2 Wafalme 4:32

When Elisha was come into the house, behold, the child was dead, and laid on his bed.

Basi akaingia ndani, akajifungia mlango, yeye na yule mtoto wote wawili, akamwomba Bwana. 2 Wafalme 4:33

He went in therefore, and shut the door on them both, and prayed to Yahweh.

Akapanda juu ya kitanda, akajilaza juu ya mtoto, akaweka kinywa chake juu ya kinywa chake, na macho yake juu ya macho yake, na mikono yake juu ya mikono yake; akajinyosha juu yake; mwili wake yule mtoto ukaanza kupata moto. 2 Wafalme 4:34

He went up, and lay on the child, and put his mouth on his mouth, and his eyes on his eyes, and his hands on his hands: and he stretched himself on him; and the flesh of the child grew warm.

Kisha akarudi, akatembea nyumbani, huko na huko mara moja; akapanda, akajinyosha juu yake; na yule mtoto akapiga chafya mara saba, na mtoto akafumbua macho yake. 2 Wafalme 4:35

Then he returned, and walked in the house once back and forth; and went up, and stretched himself on him: and the child sneezed seven times, and the child opened his eyes.

Akamwita Gehazi, akasema, Mwite yule Mshunami. Basi akamwita. Na alipofika kwake, Elisha akasema, Haya! Mchukue mwanao. 2 Wafalme 4:36

He called Gehazi, and said, Call this Shunammite. So he called her. When she was come in to him, he said, Take up your son.

Ndipo akaingia, akamwangukia miguu akainama mpaka nchi; kisha akamchukua mwanawe, akatoka. 2 Wafalme 4:37

Then she went in, and fell at his feet, and bowed herself to the ground; and she took up her son, and went out.

Elisha akafika Gilgali tena; na kulikuwa na njaa katika nchi; na hao wana wa manabii walikuwa wakikaa mbele yake. Akamwambia mtumishi wake, Teleka sufuria kubwa, uwapikie wana wa manabii. 2 Wafalme 4:38

Elisha came again to Gilgal. There was a dearth in the land; and the sons of the prophets were sitting before him; and he said to his servant, Set on the great pot, and boil stew for the sons of the prophets.

Na mmoja wao akaenda nje kondeni ili kuchuma mboga, akaona mtango-mwitu, akayachuma matango-mwitu, hata nguo yake ikawa imejaa, akaja akayapasua-pasua sufuriani; kwa maana hawakuyajua. 2 Wafalme 4:39

One went out into the field to gather herbs, and found a wild vine, and gathered of it wild gourds his lap full, and came and shred them into the pot of stew; for they didn't recognize them.

Basi wakawapakulia hao watu ili wale. Ikawa, walipokuwa katika kula chakula, wakapiga kelele, wakasema, Mauti imo sufuriani, Ee mtu wa Mungu. Wala hawakuweza kula. 2 Wafalme 4:40

So they poured out for the men to eat. It happened, as they were eating of the stew, that they cried out, and said, man of God, there is death in the pot. They could not eat of it.

Lakini yeye akasema, Leteni unga. Naye akautupa ndani ya sufuria; akasema, Wapakulie watu, ili wale. Wala hakikuwamo kitu kibaya sufuriani. 2 Wafalme 4:41

But he said, Then bring meal. He cast it into the pot; and he said, Pour out for the people, that they may eat. There was no harm in the pot.

Tena, akaja mtu kutoka Baal-shalisha, akamletea mtu wa Mungu chakula cha malimbuko, mikate ishirini ya shayiri, na masuke mabichi ya ngano guniani. Akasema, Uwape watu, ili wale. 2 Wafalme 4:42

There came a man from Baal Shalishah, and brought the man of God bread of the first fruits, twenty loaves of barley, and fresh ears of grain in his sack. He said, Give to the people, that they may eat.

Na mtumishi wake akasema, Je! Niwaandikie hiki watu mia? Lakini akasema, Uwape watu, ili wale; kwa kuwa Bwana asema hivi, Watakula na kusaza. 2 Wafalme 4:43

His servant said, What, should I set this before a hundred men? But he said, Give the people, that they may eat; for thus says Yahweh, They shall eat, and shall leave of it.

Basi akawaandikia, nao wakala, wakasaza, sawasawa na neno la Bwana. 2 Wafalme 4:44

So he set it before them, and they ate, and left of it, according to the word of Yahweh.