Danieli 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
Danieli 5 (Swahili) Daniel 5 (English)

Belshaza, mfalme, aliwafanyia wakuu wake elfu karamu kubwa akanywa divai mbele ya elfu hao. Danieli 5:1

Belshazzar the king made a great feast to a thousand of his lords, and drank wine before the thousand.

Belshaza, alipokuwa akionja ile divai, akaamuru wavilete vile vyombo vya dhahabu na fedha, ambavyo baba yake, Nebukadreza, alivitoa katika hekalu lililokuwako Yerusalemu; ili kwamba mfalme, na wakuu wake, na wake zake, na masuria wake, wapate kuvinywea. Danieli 5:2

Belshazzar, while he tasted the wine, commanded to bring the golden and silver vessels which Nebuchadnezzar his father had taken out of the temple which was in Jerusalem; that the king and his lords, his wives and his concubines, might drink from it.

Basi wakavileta vile vyombo vya dhahabu, vilivyotolewa katika hekalu la nyumba ya Mungu lililokuwako Yerusalemu; na mfalme na wakuu wake, na wake zake, na masuria wake, wakavinywea. Danieli 5:3

Then they brought the golden vessels that were taken out of the temple of the house of God which was at Jerusalem; and the king and his lords, his wives and his concubines, drank from them.

Wakanywa divai, wakaisifu miungu ya dhahabu, na ya fedha, na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe. Danieli 5:4

They drank wine, and praised the gods of gold, and of silver, of brass, of iron, of wood, and of stone.

Saa iyo hiyo vikatokea vidole vya mkono wa mwanadamu, vikaandika katika chokaa ya ukuta wa nyumba ya enzi ya mfalme, mahali palipokikabili kinara; naye mfalme akakiona kitanga cha ule mkono ulioandika. Danieli 5:5

In the same hour came forth the fingers of a man's hand, and wrote over against the lampstand on the plaster of the wall of the king's palace: and the king saw the part of the hand that wrote.

Ndipo uso wa mfalme ukambadilika; fikira zake zikamfadhaisha; viungo vya viuno vyake vikalegea; magoti yake yakagongana. Danieli 5:6

Then the king's face was changed in him, and his thoughts troubled him; and the joints of his loins were loosened, and his knees struck one against another.

Mfalme akalia kwa sauti kubwa, akaamuru waletwe wachawi, na Wakaldayo na wanajimu. Mfalme akanena, akawaambia wenye hekima wa Babeli, mtu awaye yote atakayesoma maandiko haya, na kunionyesha tafsiri yake, atavikwa mavazi ya rangi ya zambarau, na kuwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwake, naye atakuwa mtu wa tatu katika ufalme. Danieli 5:7

The king cried aloud to bring in the enchanters, the Chaldeans, and the soothsayers. The king spoke and said to the wise men of Babylon, Whoever shall read this writing, and show me the interpretation of it, shall be clothed with purple, and have a chain of gold about his neck, and shall be the third ruler in the kingdom.

Basi wakaingia wenye hekima wote wa mfalme; lakini hawakuweza kuyasoma yale maandiko, wala kumjulisha mfalme tafsiri yake. Danieli 5:8

Then came in all the king's wise men; but they could not read the writing, nor make known to the king the interpretation.

Ndipo mfalme Belshaza akahangaika sana, uso wake ukambadilika, na wakuu wake wakaona fadhaa. Danieli 5:9

Then was king Belshazzar greatly troubled, and his face was changed in him, and his lords were perplexed.

Basi malkia, kwa sababu ya maneno ya mfalme na ya wakuu wake, akaingia katika nyumba ya karamu; malkia akanena, akasema, Ee mfalme, uishi milele; fikira zako zisikufadhaishe; wala uso wako usibadilike. Danieli 5:10

[Now] the queen by reason of the words of the king and his lords came into the banquet house: the queen spoke and said, O king, live forever; don't let your thoughts trouble you, nor let your face be changed.

Yuko mtu katika ufalme wako, ambaye roho ya miungu watakatifu inakaa ndani yake; na katika siku za baba yako nuru na ufahamu na hekima zilionekana ndani yake; na mfalme Nebukadreza, baba yako, naam, mfalme, baba yako, akamfanya kuwa mkuu wa waganga, na wachawi, na Wakaldayo, na wanajimu; Danieli 5:11

There is a man in your kingdom, in whom is the spirit of the holy gods; and in the days of your father light and understanding and wisdom, like the wisdom of the gods, were found in him; and the king Nebuchadnezzar your father, the king, [I say], your father, made him master of the magicians, enchanters, Chaldeans, and soothsayers;

kwa kuwa roho njema kupita kiasi, na maarifa, na ufahamu, na uwezo wa kufasiri ndoto, na kufunua maneno ya fumbo, na kufungua mafundo, zilionekana katika Danielii huyo, ambaye mfalme alimwita Belteshaza. Basi na aitwe Danielii, naye ataionyesha tafsiri. Danieli 5:12

because an excellent spirit, and knowledge, and understanding, interpreting of dreams, and showing of dark sentences, and dissolving of doubts, were found in the same Daniel, whom the king named Belteshazzar. Now let Daniel be called, and he will show the interpretation.

Ndipo Danielii akaletwa mbele ya mfalme. Na Mfalme akanena, akamwambia Danielii, Je! Wewe ndiwe Danielii yule, aliye mmoja wa wana wa Yuda waliohamishwa, ambao mfalme, baba yangu, aliwaleta huku toka Yerusalemu? Danieli 5:13

Then was Daniel brought in before the king. The king spoke and said to Daniel, Are you that Daniel, who are of the children of the captivity of Judah, whom the king my father brought out of Judah?

Nimesikia habari zako, kwamba roho ya miungu imo ndani yako, na kwamba nuru na ufahamu na akili bora zimeonekana kwako. Danieli 5:14

I have heard of you, that the spirit of the gods is in you, and that light and understanding and excellent wisdom are found in you.

Basi sasa, watu wenye hekima na wachawi wameletwa mbele yangu, wapate kulisoma andiko hili, na kunijulisha tafsiri yake; lakini hawakuweza kunijulisha tafsiri ya jambo hili. Danieli 5:15

Now the wise men, the enchanters, have been brought in before me, that they should read this writing, and make known to me the interpretation of it; but they could not show the interpretation of the thing.

Lakini nimesikia habari zako, kwamba waweza kuleta tafsiri, na kufumbua mafumbo; haya! Kama ukiweza kulisoma andiko hili, na kunijulisha tafsiri yake, utavikwa mavazi ya rangi ya zambarau, na kuwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwako, nawe utakuwa mtu wa tatu katika ufalme. Danieli 5:16

But I have heard of you, that you can give interpretations, and dissolve doubts; now if you can read the writing, and make known to me the interpretation of it, you shall be clothed with purple, and have a chain of gold about your neck, and shall be the third ruler in the kingdom.

Ndipo Danielii akajibu, akasema mbele ya mfalme; Zawadi zako zishike wewe mwenyewe; na thawabu zako mpe mtu mwingine; walakini nitamsomea mfalme maandiko haya, na kumjulisha tafsiri yake. Danieli 5:17

Then Daniel answered before the king, Let your gifts be to yourself, and give your rewards to another; nevertheless I will read the writing to the king, and make known to him the interpretation.

Kwa habari zako, Ee mfalme, Mungu Aliye juu alimpa Nebukadreza, baba yako, ufalme, na ukuu, na fahari, na utukufu; Danieli 5:18

You king, the Most High God gave Nebuchadnezzar your father the kingdom, and greatness, and glory, and majesty:

na kwa sababu ya ule ukuu aliompa, watu wa kabila zote, na mataifa, na lugha, wakatetemeka na kuogopa mbele yake; aliyetaka kumwua alimwua; na aliyetaka kumwacha hai, alimwacha hai; aliyetaka kumtukuza, alimtukuza; na aliyetaka kumshusha, alimshusha. Danieli 5:19

and because of the greatness that he gave him, all the peoples, nations, and languages trembled and feared before him: whom he would he killed, and whom he would he kept alive; and whom he would he raised up, and whom he would he put down.

Lakini moyo wake ulipoinuliwa, na roho yake ilipokuwa ngumu akatenda kwa kiburi, aliuzuliwa katika kiti chake cha enzi, nao wakamwondolea utukufu wake. Danieli 5:20

But when his heart was lifted up, and his spirit was hardened so that he dealt proudly, he was deposed from his kingly throne, and they took his glory from him:

Akafukuzwa mbali na wanadamu, moyo wake ukafanywa kuwa kama moyo wa mnyama, na makao yake yalikuwa pamoja na punda-mwitu; akalishwa majani kama ng'ombe, mwili wake ukalowa maji kwa umande wa mbinguni; hata alipojua ya kuwa Mungu Aliye juu ndiye anayetawala katika ufalme wa wanadamu, na ya kuwa humweka juu yake yeye amtakaye, awaye yote. Danieli 5:21

and he was driven from the sons of men, and his heart was made like the animals', and his dwelling was with the wild donkeys; he was fed with grass like oxen, and his body was wet with the dew of the sky; until he knew that the Most High God rules in the kingdom of men, and that he sets up over it whoever he will.

Na wewe, mwanawe, Ee Belshaza, hukujinyenyekeza moyo wako, ijapokuwa ulijua hayo yote. Danieli 5:22

You his son, Belshazzar, have not humbled your heart, though you knew all this,

Bali umejiinua juu ya Bwana wa mbingu; nao wamevileta vyombo vya nyumba yake mbele yako; na wewe, na wakuu wako, na wake zako, na masuria wako, mmevinywea; nawe umeisifu miungu ya fedha na ya dhahabu na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe; wasioona, wala kusikia, wala kujua neno lo lote; na Mungu yule, ambaye pumzi yako i mkononi mwake, na njia zako zote ni zake, hukumtukuza. Danieli 5:23

but have lifted up yourself against the Lord of heaven; and they have brought the vessels of his house before you, and you and your lords, your wives and your concubines, have drunk wine from them; and you have praised the gods of silver and gold, of brass, iron, wood, and stone, which don't see, nor hear, nor know; and the God in whose hand your breath is, and whose are all your ways, you have not glorified.

Ndipo kile kitanga cha ule mkono kikaletwa kutoka mbele zake, na maandiko haya yameandikwa. Danieli 5:24

Then was the part of the hand sent from before him, and this writing was inscribed.

Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI. Danieli 5:25

This is the writing that was inscribed: MENE, MENE, TEKEL, UPHARSIN.

Na tafsiri ya maneno haya ni hii; MENE, Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha. Danieli 5:26

This is the interpretation of the thing: MENE; God has numbered your kingdom, and brought it to an end;

TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka. Danieli 5:27

TEKEL; you are weighed in the balances, and are found wanting.

PERESI, ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi. Danieli 5:28

PERES; your kingdom is divided, and given to the Medes and Persians.

Ndipo Belshaza akatoa amri, nao wakamvika Danielii mavazi ya rangi ya zambarau, wakatia mkufu wa dhahabu shingoni mwake, wakapiga mbiu kutangaza habari zake, ya kwamba yeye ni mtu wa tatu katika ufalme. Danieli 5:29

Then commanded Belshazzar, and they clothed Daniel with purple, and put a chain of gold about his neck, and made proclamation concerning him, that he should be the third ruler in the kingdom.

Usiku uo huo Belshaza, mfalme wa Wakaldayo, akauawa. Danieli 5:30

In that night Belshazzar the Chaldean King was slain.

Na Dario, Mmedi, akaupokea ufalme, naye umri wake alikuwa na miaka sitini na miwili.

Danieli 5:31

Darius the Mede received the kingdom, being about sixty-two years old.