Habakuki 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Habakuki 2 (Swahili) Habakkuk 2 (English)

Mimi nitasimama katika zamu yangu, nitajiweka juu ya mnara, nitaangalia ili nione atakaloniambia, na jinsi nitakavyojibu katika habari ya kulalamika kwangu. Habakuki 2:1

I will stand at my watch, and set myself on the ramparts, and will look out to see what he will say to me, and what I will answer concerning my complaint.

Bwana akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji. Habakuki 2:2

Yahweh answered me, "Write the vision, and make it plain on tablets, that he may run who reads it.

Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia. Habakuki 2:3

For the vision is yet for the appointed time, and it hurries toward the end, and won't prove false. Though it takes time, wait for it; because it will surely come. It won't delay.

Tazama, roho yake hujivuna, haina unyofu ndani yake; lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake. Habakuki 2:4

Behold, his soul is puffed up. It is not upright in him, but the righteous will live by his faith.

Naam, pamoja na hayo, divai ni mchumi mdanganyifu, mtu wa kiburi asiyekaa nyumbani mwake; huongeza tamaa yake kama kuzimu, naye huwa kama mauti, hawezi kushibishwa; bali hujikusanyia mataifa yote; hujiwekea kabila zote chungu chungu. Habakuki 2:5

Yes, moreover, wine is treacherous. A haughty man who doesn't stay at home, who enlarges his desire as Sheol, and he is like death, and can't be satisfied, but gathers to himself all nations, and heaps to himself all peoples.

Je! Hawa wote hawatapiga mfano juu yake, na mithali ya kusimanga juu yake, wakisema, Ole wake yeye aongezaye kisicho mali yake! Hata lini? Na ole wake yeye ajitwikaye mzigo wa rehani! Habakuki 2:6

Won't all these take up a parable against him, and a taunting proverb against him, and say, 'Woe to him who increases that which is not his, and who enriches himself by extortion! How long?'

Je! Hawatainuka ghafula wao watakaokuuma, hawataamka wao watakaokusumbua, nawe utakuwa mateka kwao? Habakuki 2:7

Won't your debtors rise up suddenly, and wake up those who make you tremble, and you will be their victim?

Kwa sababu umeteka nyara mataifa mengi, mabaki yote ya kabila watakuteka wewe; kwa sababu ya damu ya watu, na kwa sababu ya udhalimu iliotendwa nchi hii, na mji huu, na watu wote wanaokaa ndani yake. Habakuki 2:8

Because you have plundered many nations, all the remnant of the peoples will plunder you, because of men's blood, and for the violence done to the land, to the city and to all who dwell in it.

Ole wake yeye aipatiaye nyumba yake mapato mabaya, ili apate kukiweka kioto chake juu, apate kujiepusha na mkono wa uovu! Habakuki 2:9

Woe to him who gets an evil gain for his house, that he may set his nest on high, that he may be delivered from the hand of evil!

Wewe umeifanyia nyumba yako kusudi la aibu, kwa kukatilia mbali watu wengi, nawe umetenda dhambi juu ya roho yako. Habakuki 2:10

You have devised shame to your house, by cutting off many peoples, and have sinned against your soul.

Kwa maana jiwe litapiga kelele katika ukuta, nayo boriti katika miti italijibu. Habakuki 2:11

For the stone will cry out of the wall, and the beam out of the woodwork will answer it.

Ole wake yeye ajengaye mji kwa damu, awekaye imara mji mkubwa kwa uovu! Habakuki 2:12

Woe to him who builds a town with blood, and establishes a city by iniquity!

Angalieni; je! Jambo hili halikutoka kwa Bwana wa majeshi, kwamba watu wajishughulikie moto, na mataifa wajisumbue kwa ajili ya ubatili? Habakuki 2:13

Behold, isn't it of Yahweh of Hosts that the peoples labor for the fire, and the nations weary themselves for vanity?

Kwa maana dunia itajazwa maarifa ya utukufu wa Bwana, kama maji yaifunikavyo bahari. Habakuki 2:14

For the earth will be filled with the knowledge of the glory of Yahweh, as the waters cover the sea.

Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao! Habakuki 2:15

"Woe to him who gives his neighbor drink, pouring your inflaming wine until they are drunk, so that you may gaze at their naked bodies!

Umejaa aibu badala ya utukufu; unywe nawe, uwe kama mtu asiyetahiriwa; kikombe cha mkono wa kuume wa Bwana kitageuzwa ukipokee, na aibu kuu itakuwa juu ya utukufu wako. Habakuki 2:16

You are filled with shame, and not glory. You will also drink, and be exposed! The cup of Yahweh's right hand will come around to you, and disgrace will cover your glory.

Kwa maana udhalimu uliotendwa juu ya Lebanoni utakufunikiza, na kuangamizwa kwao wanyama kutakutia hofu; kwa sababu ya damu ya watu, na kwa sababu ya udhalimu iliotendwa nchi hii, na mji huu, na watu wote wanaokaa ndani yake. Habakuki 2:17

For the violence done to Lebanon will overwhelm you, and the destruction of the animals, which made them afraid; because of men's blood, and for the violence done to the land, to every city and to those who dwell in them.

Sanamu ya kuchora yafaa nini, hata yeye aliyeifanya ameichora? Sanamu ya kuyeyuka, nayo ni mwalimu wa uongo, yafaa nini, hata yeye aliyeifanya aiwekee tumaini lake, na kufanya sanamu zisizoweza kusema? Habakuki 2:18

"What value does the engraved image have, that its maker has engraved it; the molten image, even the teacher of lies, that he who fashions its form trusts in it, to make mute idols?

Ole wake yeye auambiaye mti, Amka; aliambiaye jiwe lisiloweza kusema, Ondoka! Je! Kitu hicho kitafundisha? Tazama, kimefunikwa kwa dhahabu na fedha, wala hamna pumzi ndani yake kabisa. Habakuki 2:19

Woe to him who says to the wood, 'Awake!' or to the mute stone, 'Arise!' Shall this teach? Behold, it is overlaid with gold and silver, and there is no breath at all in the midst of it.

Lakini Bwana yumo ndani ya hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze kimya mbele zake. Habakuki 2:20

But Yahweh is in his holy temple. Let all the earth be silent before him!"