Yoshua 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yoshua 3 (Swahili) Joshua 3 (English)

Yoshua akaondoka asubuhi na mapema, nao wakatoka Shitimu, wakafika mto wa Yordani, yeye na wana wa Israeli wote, wakakaa hapo kabla ya kuvuka. Yoshua 3:1

Joshua rose up early in the morning; and they removed from Shittim, and came to the Jordan, he and all the children of Israel; and they lodged there before they passed over.

Ikawa baada ya siku tatu, maakida wakapita katikati ya marago, Yoshua 3:2

It happened after three days, that the officers went through the midst of the camp;

wakawaamuru watu wote wakisema, Mtakapoliona sanduku la agano la Bwana, Mungu wenu, na makuhani Walawi wakilichukua, ndipo mtakapoondoka hapa mlipo na kulifuata. Yoshua 3:3

and they commanded the people, saying, When you see the ark of the covenant of Yahweh your God, and the priests the Levites bearing it, then you shall remove from your place, and go after it.

Lakini, na iwe nafasi kati ya ninyi na lile sanduku, kama dhiraa elfu mbili kiasi chake; msilikaribie mpate kuijua njia ambayo hamna budi kuiendea; kwa maana hamjapita njia hii bado. Yoshua 3:4

Yet there shall be a space between you and it, about two thousand cubits by measure: don't come near to it, that you may know the way by which you must go; for you have not passed this way heretofore.

Yoshua akawaambia watu, Jitakaseni; maana kesho Bwana atatenda mambo ya ajabu kati yenu. Yoshua 3:5

Joshua said to the people, Sanctify yourselves; for tomorrow Yahweh will do wonders among you.

Kisha Yoshua akawaambia makuhani, akasema, Liinueni sanduku la agano, mkavuke mbele ya hao watu. Wakaliinua sanduku la agano, wakatangulia mbele ya watu. Yoshua 3:6

Joshua spoke to the priests, saying, Take up the ark of the covenant, and pass over before the people. They took up the ark of the covenant, and went before the people.

Bwana akamwambia Yoshua, Hivi leo nitaanza kukutukuza mbele ya Israeli wote, wapate kujua ya kuwa mimi nitakuwa pamoja na wewe, kama nilivyokuwa pamoja na Musa. Yoshua 3:7

Yahweh said to Joshua, This day will I begin to magnify you in the sight of all Israel, that they may know that, as I was with Moses, so I will be with you.

Nawe uwaamuru hao makuhani walichukuao sanduku la agano, ukawaambie, Mtakapofika ukingo wa maji ya Yordani, simameni katika Yordani. Yoshua 3:8

You shall command the priests who bear the ark of the covenant, saying, When you are come to the brink of the waters of the Jordan, you shall stand still in the Jordan.

Basi Yoshua akawaambia wana wa Israeli, Njoni huku, mkayasikie maneno ya Bwana, Mungu wenu. Yoshua 3:9

Joshua said to the children of Israel, Come here, and hear the words of Yahweh your God.

Yoshua akasema, Kwa jambo hili mtajua ya kuwa Mungu aliye hai yu kati yenu, na ya kuwa hatakosa kuwatoa mbele yenu Mkanaani, na Mhiti, na Mhivi, na Mperizi, na Mgirgashi, na Mwamori, na Myebusi. Yoshua 3:10

Joshua said, Hereby you shall know that the living God is among you, and that he will without fail drive out from before you the Canaanite, and the Hittite, and the Hivite, and the Perizzite, and the Girgashite, and the Amorite, and the Jebusite.

Tazama, sanduku la agano la Bwana wa dunia yote linavuka mbele yenu na kuingia Yordani. Yoshua 3:11

Behold, the ark of the covenant of the Lord of all the earth passes over before you into the Jordan.

Basi sasa twaeni watu kumi na wawili katika kabila za Israeli, kila kabila mtu mmoja. Yoshua 3:12

Now therefore take twelve men out of the tribes of Israel, for every tribe a man.

Itakuwa, wakati nyayo za makuhani walichukuao sanduku la Bwana, Bwana wa dunia yote, zitakaposimama katika maji ya Yordani, hayo maji ya Yordani yatatindika, maji yale yashukayo kutoka juu; nayo yatasimama kama chuguu. Yoshua 3:13

It shall come to pass, when the soles of the feet of the priests who bear the ark of Yahweh, the Lord of all the earth, shall rest in the waters of the Jordan, that the waters of the Jordan shall be cut off, even the waters that come down from above; and they shall stand in one heap.

Hata ikawa, hao watu walipotoka katika hema zao, ili kuvuka Yordani, makuhani waliolichukua sanduku la agano wakatangulia mbele ya watu, Yoshua 3:14

It happened, when the people removed from their tents, to pass over the Jordan, the priests who bore the ark of the covenant being before the people;

basi hao waliolichukua hilo sanduku walipofika Yordani, na nyayo za makuhani waliolichukua sanduku zilipotiwa katika maji ya ukingoni, (maana Yordani hujaa hata kingo zake na kufurika wakati wote wa mavuno), Yoshua 3:15

and when those who bore the ark were come to the Jordan, and the feet of the priests who bore the ark were dipped in the brink of the water (for the Jordan overflows all its banks all the time of harvest),

ndipo hayo maji yaliyoshuka kutoka juu yakasimama, yakainuka, yakawa chuguu, mbali sana, huko Adamu, mji ule ulio karibu na Sarethani, na maji yale yaliyotelemkia bahari ya Araba, yaani Bahari ya Chumvi, yakatindika kabisa; watu wakavuka kukabili Yeriko. Yoshua 3:16

that the waters which came down from above stood, and rose up in one heap, a great way off, at Adam, the city that is beside Zarethan; and those that went down toward the sea of the Arabah, even the Salt Sea, were wholly cut off: and the people passed over right against Jericho.

Na hao makuhani waliolichukua sanduku la agano la Bwana wakasimama imara mahali pakavu katikati ya Yordani; Israeli wote wakavuka katika nchi kavu, hata taifa lile lote likaisha kuvuka Yordani. Yoshua 3:17

The priests who bore the ark of the covenant of Yahweh stood firm on dry ground in the midst of the Jordan; and all Israel passed over on dry ground, until all the nation were passed clean over the Jordan.