Luka 20 Swahili & English

Listen/Download Audio
Luka 20 (Swahili) Luke 20 (English)

Ikawa siku moja, alipokuwa akiwafundisha watu hekaluni, na kuihubiri habari njema, wakuu wa makuhani na waandishi pamoja na wazee walimtokea ghafula; Luka 20:1

It happened on one of those days, as he was teaching the people in the temple and preaching the Gospel, that the {TR adds "chief"}priests and scribes came to him with the elders.

wakamwambia, wakisema, Tuambie, unatenda mambo hayo kwa mamlaka gani? Tena, ni nani aliyekupa mamlaka hii? Luka 20:2

They asked him, "Tell us: by what authority do you do these things? Or who is giving you this authority?"

Akajibu akawaambia, Nami nitawauliza ninyi neno moja; niambieni, Luka 20:3

He answered them, "I also will ask you one question. Tell me:

Ubatizo wa Yohana, je! Ulitoka mbinguni au kwa wanadamu? Luka 20:4

the baptism of John, was it from heaven, or from men?"

Wakahojiana wao kwa wao, wakisema, Kama tukisema ulitoka mbinguni, atasema, Basi, mbona hamkumwamini? Luka 20:5

They reasoned with themselves, saying, "If we say, 'From heaven,' he will say, 'Why didn't you believe him?'

Na tukisema ulitoka kwa wanadamu, watu wote watatupiga kwa mawe, kwa kuwa wamemkubali Yohana kuwa ni nabii. Luka 20:6

But if we say, 'From men,' all the people will stone us, for they are persuaded that John was a prophet."

Wakajibu, kwamba, Hatujui ulikotoka. Luka 20:7

They answered that they didn't know where it was from.

Yesu akawaambia, Wala mimi siwaambii ninyi ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya. Luka 20:8

Jesus said to them, "Neither will I tell you by what authority I do these things."

Akaanza kuwaambia watu mfano huu; Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu; akapangisha wakulima, akaenda akakaa katika nchi nyingine muda mrefu. Luka 20:9

He began to tell the people this parable. "A {NU (in brackets) and TR add "certain"}man planted a vineyard, and rented it out to some farmers, and went into another country for a long time.

Na wakati wa mavuno alituma mtumwa kwa wale wakulima ili wampe baadhi ya matunda ya mizabibu; wakulima wakampiga wakamfukuza mikono mitupu. Luka 20:10

At the proper season, he sent a servant to the farmers to collect his share of the fruit of the vineyard. But the farmers beat him, and sent him away empty.

Akatuma na mtumwa mwingine. Wakampiga huyu naye, wakamwaibisha wakamfukuza mikono mitupu. Luka 20:11

He sent yet another servant, and they also beat him, and treated him shamefully, and sent him away empty.

Akamtuma na wa tatu; huyu naye wakamtia jeraha, wakamtupa nje. Luka 20:12

He sent yet a third, and they also wounded him, and threw him out.

Basi, bwana wa shamba la mizabibu alisema, Nifanyeje? Nitamtuma mwanangu, mpendwa wangu; yamkini watamheshimu yeye. Luka 20:13

The lord of the vineyard said, 'What shall I do? I will send my beloved son. It may be that seeing him, they will respect him.'

Lakini, wale wakulima walipomwona, walishauriana wao kwa wao, wakisema, Huyu ndiye mrithi; haya, na tumwue, ili urithi uwe wetu. Luka 20:14

"But when the farmers saw him, they reasoned among themselves, saying, 'This is the heir. Come, let's kill him, that the inheritance may be ours.'

Wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamwua. Basi, bwana wa shamba la mizabibu atawatendeje? Luka 20:15

They threw him out of the vineyard, and killed him. What therefore will the lord of the vineyard do to them?

Atakuja na kuwaangamiza wakulima wale, na lile shamba la mizabibu atawapa wengine. Waliposikia hayo walisema, Hasha! Yasitukie haya! Luka 20:16

He will come and destroy these farmers, and will give the vineyard to others." When they heard it, they said, "May it never be!"

Akawakazia macho akasema, Maana yake nini basi neno hili lililoandikwa, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni? Luka 20:17

But he looked at them, and said, "Then what is this that is written, 'The stone which the builders rejected, The same was made the chief cornerstone?'

Kila mtu aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-vunjika; na ye yote ambaye litamwangukia litamsaga kabisa. Luka 20:18

"Everyone who falls on that stone will be broken to pieces, But it will crush whomever it falls on to dust."

Nao waandishi na wakuu wa makuhani walitafuta kumkamata saa iyo hiyo, wakawaogopa watu, maana walitambua ya kwamba mfano huu amewanenea wao. Luka 20:19

The chief priests and the scribes sought to lay hands on Him that very hour, but they feared the people--for they knew He had spoken this parable against them.

Wakamvizia-vizia, wakatuma wapelelezi waliojifanya kuwa watu wa haki, ili wamnase katika maneno yake, wapate kumtia katika enzi na mamlaka ya liwali. Luka 20:20

They watched him, and sent out spies, who pretended to be righteous, that they might trap him in something he said, so as to deliver him up to the power and authority of the governor.

Wakamwuliza, wakisema, Mwalimu, twajua ya kwamba wasema na kufundisha yaliyo ya haki, wala hujali cheo cha mtu, bali unafundisha njia ya Mungu kwa kweli. Luka 20:21

They asked him, "Teacher, we know that you say and teach what is right, and aren't partial to anyone, but truly teach the way of God.

Je! Ni halali tumpe Kaisari kodi, au sivyo? Luka 20:22

Is it lawful for us to pay taxes to Caesar, or not?"

Lakini yeye alitambua hila yao, akawaambia, Luka 20:23

But he perceived their craftiness, and said to them, "Why do you test me?

Nionyesheni dinari. Ina sura na anwani ya nani? Wakamjibu, Ya Kaisari. Luka 20:24

Show me a denarius. Whose image and inscription are on it?" They answered, "Caesar's."

Akawaambia, Basi, vya Kaisari mpeni Kaisari, na vya Mungu mpeni Mungu. Luka 20:25

He said to them, "Then give to Caesar the things that are Caesar's, and to God the things that are God's."

Wala hawakuweza kumshitaki kwa maneno yake mbele ya watu; wakastaajabia majibu yake, wakanyamaa. Luka 20:26

They weren't able to trap him in his words before the people. They marveled at his answer, and were silent.

Kisha baadhi ya Masadukayo wakamwendea, wale wasemao ya kwamba hakuna ufufuo, wakamwuliza, Luka 20:27

Some of the Sadducees came to him, those who deny that there is a resurrection.

wakisema, Mwalimu, Musa alituandikia ya kuwa, mtu akifiwa na ndugu yake mwenye mke, lakini hana mtoto na amtwae huyu mke, ampatie ndugu yake mzao. Luka 20:28

They asked him, "Teacher, Moses wrote to us that if a man's brother dies having a wife, and he is childless, his brother should take the wife, and raise up children for his brother.

Basi, kulikuwa na ndugu saba. Wa kwanza alioa mke, akafa hana mtoto; Luka 20:29

There were therefore seven brothers. The first took a wife, and died childless.

na wa pili [akamtwaa yule mke, akafa hana mtoto;] Luka 20:30

The second took her as wife, and he died childless.

hata wa tatu akamwoa, na kadhalika wote saba, wakafa, wasiache watoto. Luka 20:31

The third took her, and likewise the seven all left no children, and died.

Mwisho akafa yule mke naye. Luka 20:32

Afterward the woman also died.

Basi, katika ufufuo atakuwa mke wa yupi? Maana aliolewa na wote saba. Luka 20:33

Therefore in the resurrection whose wife of them will she be? For the seven had her as a wife."

Yesu akawaambia, Wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa; Luka 20:34

Jesus said to them, "The children of this age marry, and are given in marriage.

lakini, wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na kule kufufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi; Luka 20:35

But those who are considered worthy to attain to that age and the resurrection from the dead, neither marry, nor are given in marriage.

wala hawawezi kufa tena; kwa sababu huwa sawasawa na malaika, nao ni wana wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa ufufuo. Luka 20:36

For they can't die any more, for they are like the angels, and are children of God, being children of the resurrection.

Lakini, ya kuwa wafu hufufuliwa, hata na Musa alionyesha katika sura ya Kijiti, hapo alipomtaja Bwana kuwa ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Luka 20:37

But that the dead are raised, even Moses showed at the bush, when he called the Lord 'The God of Abraham, the God of Isaac, and the God of Jacob.'

Naye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai; kwa kuwa wote huishi kwake. Luka 20:38

Now he is not the God of the dead, but of the living, for all are alive to him."

Waandishi wengine wakajibu wakamwambia, Mwalimu, umesema vema; Luka 20:39

Some of the scribes answered, "Teacher, you speak well."

wala hawakuthubutu kumwuliza neno baada ya hayo. Luka 20:40

They didn't dare to ask him any more questions.

Akawaambia, Wasemaje watu kwamba Kristo ni Mwana wa Daudi? Luka 20:41

He said to them, "Why do they say that the Christ is David's son?

Maana, Daudi mwenyewe asema katika chuo cha Zaburi, Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Luka 20:42

David himself says in the book of Psalms, 'The Lord said to my Lord, "Sit at my right hand,

Hata niwaweke adui zako Kuwa kiti cha kuwekea miguu yako. Luka 20:43

Until I make your enemies the footstool of your feet."'

Basi Daudi amwita Bwana; amekuwaje mwana wake? Luka 20:44

"David therefore calls him Lord, so how is he his son?"

Na watu wote walipokuwa wakimsikiliza, aliwaambia wanafunzi wake, Luka 20:45

In the hearing of all the people, he said to his disciples,

Jilindeni na waandishi, wapendao kutembea wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa masokoni, na kuketi mbele katika masinagogi, na viti vya mbele karamuni. Luka 20:46

"Beware of the scribes, who like to walk in long robes, and love greetings in the marketplaces, the best seats in the synagogues, and the best places at feasts;

Wanakula nyumba za wajane, na kwa unafiki husali sala ndefu. Hao watapata hukumu iliyo kuu. Luka 20:47

who devour widows' houses, and for a pretense make long prayers: these will receive greater condemnation."