Mika 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mika 1 (Swahili) Micah 1 (English)

Hili ndilo neno la Bwana lililomjia Mika, Mmorashti, katika siku za Yothamu, na Ahazi, na Hezekia, wafalme wa Yuda; maono aliyoyaona katika habari za Samaria, na Yerusalemu. Mika 1:1

The word of Yahweh that came to Micah the Morashtite in the days of Jotham, Ahaz, and Hezekiah, kings of Judah, which he saw concerning Samaria and Jerusalem.

Sikilizeni, enyi watu wa kabila zote; sikiliza, Ee dunia, na vyote vilivyomo; Bwana MUNGU na ashuhudie juu yenu, yeye Bwana kutoka hekalu lake takatifu. Mika 1:2

Hear, you peoples, all of you. Listen, O earth, and all that is therein: And let the Lord Yahweh be witness against you, The Lord from his holy temple.

Kwa maana, angalieni, Bwana anakuja akitoka mahali pake, naye atashuka, na kupakanyaga mahali pa dunia palipoinuka. Mika 1:3

For, behold, Yahweh comes forth out of his place, And will come down and tread on the high places of the earth.

Na hiyo milima itayeyuka chini yake, nayo mabonde yatapasuliwa, kama vile nta iliyo mbele ya moto, kama maji yaliyomwagika tena kutelemka gengeni. Mika 1:4

The mountains melt under him, And the valleys split apart, Like wax before the fire, Like waters that are poured down a steep place.

Kwa sababu ya kosa la Yakobo yametokea haya yote, na kwa sababu ya makosa ya nyumba ya Israeli. Nini kosa la Yakobo? Je, silo Samaria? Na nini mahali pa Yuda palipoinuka? Sipo Yerusalemu? Mika 1:5

"All this is for the disobedience of Jacob, And for the sins of the house of Israel. What is the disobedience of Jacob? Isn't it Samaria? And what are the high places of Judah? Aren't they Jerusalem?

Kwa ajili ya hayo nitafanya Samaria kuwa kama chungu katika shamba, na kama miche ya shamba la mizabibu; nami nitayatupa mawe yake bondeni, nami nitaifunua misingi yake. Mika 1:6

Therefore I will make Samaria like a rubble heap of the field, Like places for planting vineyards; And I will pour down its stones into the valley, And I will uncover its foundations.

Na sanamu zake zote za kuchonga zitapondwa-pondwa, na ijara zake zote zitateketezwa kwa moto, na sanamu zake zote nitazifanya ukiwa; kwa kuwa amezikusanya kwa ujira wa kahaba, nazo zitaurudia ujira wa kahaba. Mika 1:7

All her idols will be beaten to pieces, And all her temple gifts will be burned with fire, And all her images I will destroy; For of the hire of a prostitute has she gathered them, And to the hire of a prostitute shall they return."

Kwa ajili ya hayo nitaomboleza na kulia, Nitakwenda nimevua nguo, ni uchi; Nitafanya mlio kama wa mbweha, Na maombolezo kama ya mbuni. Mika 1:8

For this I will lament and wail; I will go stripped and naked; I will howl like the jackals, And moan like the daughters of owls.

Kwa maana jeraha zake haziponyekani; Maana msiba umeijilia hata Yuda, Unalifikia lango la watu wangu, Naam, hata Yerusalemu. Mika 1:9

For her wounds are incurable; For it has come even to Judah. It reaches to the gate of my people, Even to Jerusalem.

Msiyahubiri haya katika Gathi, msilie kamwe; Katika Beth-le-Afra ugae-gae mavumbini. Mika 1:10

Don't tell it in Gath, Don't weep at all. At Beth Ophrah{Beth Ophrah means literally "House of Dust."} I have rolled myself in the dust.

Piteni; uende ukaaye Shafiri, hali ya uchi na aibu; Hivyo akaaye Saanani hajatokea nje; Maombolezo ya Beth-eseli yatawaondolea tegemeo lake; Mika 1:11

Pass on, inhabitant of Shaphir, in nakedness and shame. The inhabitant of Zaanan won't come out. The wailing of Beth Ezel will take from you his protection.

Maana akaaye Marothi ana utungu wa mema; Kwa kuwa msiba umeshuka toka kwa Bwana, Umefika mpaka lango la Yerusalemu. Mika 1:12

For the inhabitant of Maroth waits anxiously for good, Because evil has come down from Yahweh to the gate of Jerusalem.

Mfungie gari la vita farasi Aliye mwepesi, ukaaye Lakishi; Alikuwa mwanzo wa dhambi kwa binti Sayuni; Maana makosa ya Israeli yameonekana kwako. Mika 1:13

Harness the chariot to the swift steed, inhabitant of Lachish. She was the beginning of sin to the daughter of Zion; For the transgressions of Israel were found in you.

Kwa hiyo utaipa Moresheth-Gathi zawadi ya kuagia; Nyumba za Akzibu zitakuwa kijito kidanganyacho wafalme wa Israeli. Mika 1:14

Therefore you will give a parting gift to Moresheth-gath. The houses of Achzib will be a deceitful thing to the kings of Israel.

Bado, ukaaye Maresha, nitakuletea yeye atakayekumiliki; Utukufu wa Israeli utafika mpaka Adulamu. Mika 1:15

I will yet bring to you, inhabitant of Mareshah, He who is the glory of Israel will come to Adullam.

Jifanyie upaa, jikate nywele zako, Kwa ajili ya watoto waliokufurahisha; Panua upaa wako kama tai; Kwa maana wamekwenda mbali nawe utumwani. Mika 1:16

Shave your heads, And cut off your hair for the children of your delight. Enlarge your baldness like the vulture; For they have gone into captivity from you!