Nehemia 6 Swahili & English

Listen/Download Audio
Nehemia 6 (Swahili) Nehemiah 6 (English)

Basi ikawa, walipoarifiwa Sanbalati, na Tobia, na Geshemu, Mwarabu na adui zetu hao wengine, kwamba nimeujenga ukuta, wala hayakusalia mavunjiko ndani yake; (ijapokuwa hata wakati ule sijaisimamisha milango katika malango); Nehemia 6:1

Now it happened, when it was reported to Sanballat and Tobiah, and to Geshem the Arabian, and to the rest of our enemies, that I had built the wall, and that there was no breach left therein; (though even to that time I had not set up the doors in the gates;)

Sanbalati na Geshemu wakatuma wajumbe kwangu, wakasema, Njoo, tukutane huko vijijini katika nchi tambarare ya Ono. Walakini wakakusudi kunifanyia mabaya. Nehemia 6:2

that Sanballat and Geshem sent to me, saying, Come, let us meet together in [one of] the villages in the plain of Ono. But they thought to do me mischief.

Na mimi nikatuma wajumbe kwao, nikasema, Hii ni kazi kubwa ninayoifanya mimi, hata nisiweze kushuka; mbona kazi ikome, hapo ninapoiacha, niwashukie? Nehemia 6:3

I sent messengers to them, saying, I am doing a great work, so that I can't come down: why should the work cease, while I leave it, and come down to you?

Nao wakaniletea maneno kama hayo mara nne; nikawajibu maneno kama yale. Nehemia 6:4

They sent to me four times after this sort; and I answered them after the same manner.

Ndipo Sanbalati akamtuma kwangu mtumwa wake vile vile mara ya tano, na barua wazi mkononi mwake; Nehemia 6:5

Then sent Sanballat his servant to me in like manner the fifth time with an open letter in his hand,

nayo yakaandikwa humo, Habari imeenea katika mataifa, naye Geshemu asema neno lilo hilo, ya kwamba wewe na Wayahudi mwakusudi kuasi; ndiyo sababu waujenga huo ukuta; nawe wataka kuwamiliki, ndivyo wasemavyo. Nehemia 6:6

in which was written, It is reported among the nations, and Gashmu says it, that you and the Jews think to rebel; for which cause you are building the wall: and you would be their king, according to these words.

Nawe umewaweka manabii ili wakuhubirie huko Yerusalemu, kusema, Yuko mfalme katika Yuda; basi sasa ataarifiwa mfalme sawasawa na maneno haya. Njoo sasa basi, na tufanye shauri pamoja. Nehemia 6:7

You have also appointed prophets to preach of you at Jerusalem, saying, There is a king in Judah: and now shall it be reported to the king according to these words. Come now therefore, and let us take counsel together.

Ndipo mimi nikatuma kwake wajumbe, kusema, Hakukufanyika mambo kama hayo uyasemayo, lakini kwa moyo wako wewe mwenyewe umeyabuni. Nehemia 6:8

Then I sent to him, saying, There are no such things done as you say, but you feign them out of your own heart.

Kwani hao wote walitaka kutuogofisha, wakisema, Italegea mikono yao katika kazi, isifanyike. Lakini sasa nitaitia mikono yangu nguvu. Nehemia 6:9

For they all would have made us afraid, saying, Their hands shall be weakened from the work, that it not be done. But now, [God], strengthen you my hands.

Nikaingia nyumbani kwa Shemaya, mwana wa Delaya, mwana wa Mehetabeli, aliyekuwa amefungwa; naye akasema, Tukutane nyumbani mwa Mungu, ndani ya hekalu, tukaifunge milango ya hekalu; kwa maana watakuja kukuua; naam, wakati wa usiku watakuja kukuua. Nehemia 6:10

I went to the house of Shemaiah the son of Delaiah the son of Mehetabel, who was shut up; and he said, Let us meet together in the house of God, within the temple, and let us shut the doors of the temple: for they will come to kill you; yes, in the night will they come to kill you.

Nami nikasema, Je! Mtu kama mimi nikimbie? Naye ni nani, akiwa kama nilivyo mimi, atakayeingia hekaluni ili kuponya maisha yake? Sitaingia. Nehemia 6:11

I said, Should such a man as I flee? and who is there that, being such as I, would go into the temple to save his life? I will not go in.

Nikatambua, na tazama, siye Mungu aliyemtuma; lakini amefanya unabii huu kinyume changu; nao Tobia na Sanbalati ndio waliomwajiri. Nehemia 6:12

I discerned, and, behold, God had not sent him; but he pronounced this prophecy against me: and Tobiah and Sanballat had hired him.

Kwa sababu hii aliajiriwa, ili mimi niogope, nikafanye hivyo na kutenda dhambi, kisha wao wawe nazo habari mbaya, ili wanishutumie. Nehemia 6:13

For this cause was he hired, that I should be afraid, and do so, and sin, and that they might have matter for an evil report, that they might reproach me.

Uwakumbuke, Ee Mungu wangu, Tobia na Sanbalati sawasawa na hayo matendo yao, na yule nabii mke Noadia, na hao manabii waliosalia, waliotaka kuniogofya. Nehemia 6:14

Remember, my God, Tobiah and Sanballat according to these their works, and also the prophetess Noadiah, and the rest of the prophets, that would have put me in fear.

Basi huo ukuta ukamalizika siku ya ishirini na tano ya mwezi wa Eluli, katika muda wa siku hamsini na mbili. Nehemia 6:15

So the wall was finished in the twenty-fifth [day] of [the month] Elul, in fifty-two days.

Ikawa adui zetu wote waliposikia, ndipo makafiri wote waliotuzunguka wakaogopa, nao wakakata tamaa sana machoni pao wenyewe; maana waliitambua kazi hiyo ilivyotendwa na Mungu wetu. Nehemia 6:16

It happened, when all our enemies heard [of it], that all the nations that were about us feared, and were much cast down in their own eyes; for they perceived that this work was worked of our God.

Tena siku zile wakuu wa Yuda walimletea Tobia nyaraka nyingi, nazo nyaraka za Tobia zikawafikilia. Nehemia 6:17

Moreover in those days the nobles of Judah sent many letters to Tobiah, and [the letters] of Tobiah came to them.

Kwa maana walikuwa watu wengi katika Yuda waliomwapia, kwa sababu alikuwa mkwewe Shekania, mwana wa Ara; naye Yehohanani mwanawe amemwoa binti Meshulamu, mwana wa Berekia. Nehemia 6:18

For there were many in Judah sworn to him, because he was the son-in-law of Shecaniah the son of Arah; and his son Jehohanan had taken the daughter of Meshullam the son of Berechiah as wife.

Tena waliyanena mema yake mbele yangu, nayo maneno yangu humwambia yeye. Tobia naye akaniletea mimi nyaraka za kuniogofisha. Nehemia 6:19

Also they spoke of his good deeds before me, and reported my words to him. Tobiah sent letters to put me in fear.