Warumi 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
Warumi 1 (Swahili) Romans 1 (English)

Paulo, mtumwa wa Kristo Yesu, aliyeitwa kuwa mtume, na kutengwa aihubiri Injili ya Mungu; Warumi 1:1

Paul, a servant of Jesus Christ, called to be an apostle, set apart for the Gospel of God,

ambayo Mungu amekwisha kuiahidi kwa kinywa cha manabii wake katika maandiko matakatifu; Warumi 1:2

which he promised before through his prophets in the holy Scriptures,

yaani, habari za Mwanawe, aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili, Warumi 1:3

concerning his Son, who was born of the seed of David according to the flesh,

na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo wa wafu, Yesu Kristo Bwana wetu; Warumi 1:4

who was declared to be the Son of God with power, according to the Spirit of holiness, by the resurrection from the dead, Jesus Christ our Lord,

ambaye katika yeye tulipokea neema na utume ili mataifa yote wapate kujitiisha kwa imani, kwa ajili ya jina lake; Warumi 1:5

through whom we received grace and apostleship, for obedience of faith among all the nations, for his name's sake;

ambao katika hao ninyi mmekuwa wateule wa Yesu Kristo; Warumi 1:6

among whom you are also called to belong to Jesus Christ;

kwa wote walioko Rumi, wapendwao na Mungu, walioitwa kuwa watakatifu. Neema na iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo. Warumi 1:7

to all who are in Rome, beloved of God, called to be saints: Grace to you and peace from God our Father and the Lord Jesus Christ.

Kwanza namshukuru Mungu wangu katika Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa kuwa imani yenu inahubiriwa katika dunia nzima. Warumi 1:8

First, I thank my God through Jesus Christ for all of you, that your faith is proclaimed throughout the whole world.

Kwa maana Mungu, nimwabuduye kwa roho yangu katika Injili ya Mwana wake, ni shahidi wangu jinsi niwatajavyo pasipo kukoma, Warumi 1:9

For God is my witness, whom I serve in my spirit in the Gospel of his Son, how unceasingly I make mention of you always in my prayers,

siku zote katika sala zangu, nikiomba nije kwenu hivi karibu, Mungu akipenda kuifanikisha safari yangu. Warumi 1:10

requesting, if by any means now at last I may be prospered by the will of God to come to you.

Kwa maana ninatamani sana kuwaona, nipate kuwapa karama ya rohoni, ili mfanywe imara; Warumi 1:11

For I long to see you, that I may impart to you some spiritual gift, to the end that you may be established;

yaani, tufarijiane mimi na ninyi, kila mtu kwa imani ya mwenzake, yenu na yangu. Warumi 1:12

that is, that I with you may be encouraged in you, each of us by the other's faith, both yours and mine.

Lakini, ndugu zangu, sipendi msiwe na habari, ya kuwa mara nyingi nalikusudia kuja kwenu, nikazuiliwa hata sasa, ili nipate kuwa na matunda kwenu ninyi pia kama nilivyo nayo katika Mataifa wengine. Warumi 1:13

Now I don't desire to have you unaware, brothers, that I often planned to come to you, and was hindered so far, that I might have some fruit among you also, even as among the rest of the Gentiles.

Nawiwa na Wayunani na wasio Wayunani, nawiwa na wenye hekima na wasio na hekima. Warumi 1:14

I am debtor both to Greeks and to foreigners, both to the wise and to the foolish.

Kwa hiyo, kwa upande wangu, mimi ni tayari kuihubiri Injili hata na kwenu ninyi mnaokaa Rumi. Warumi 1:15

So, as much as is in me, I am eager to preach the Gospel to you also who are in Rome.

Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia. Warumi 1:16

For I am not ashamed of the Gospel of Christ, for it is the power of God for salvation for everyone who believes; for the Jew first, and also for the Greek.

Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani. Warumi 1:17

For in it is revealed God's righteousness from faith to faith. As it is written, "But the righteous shall live by faith."

Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu. Warumi 1:18

For the wrath of God is revealed from heaven against all ungodliness and unrighteousness of men, who suppress the truth in unrighteousness,

Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia. Warumi 1:19

because that which is known of God is revealed in them, for God revealed it to them.

Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru; Warumi 1:20

For the invisible things of him since the creation of the world are clearly seen, being perceived through the things that are made, even his everlasting power and divinity; that they may be without excuse.

kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. Warumi 1:21

Because, knowing God, they didn't glorify him as God, neither gave thanks, but became vain in their reasoning, and their senseless heart was darkened.

Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika; Warumi 1:22

Professing themselves to be wise, they became fools,

wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo. Warumi 1:23

and traded the glory of the incorruptible God for the likeness of an image of corruptible man, and of birds, and four-footed animals, and creeping things.

Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. Warumi 1:24

Therefore God also gave them up in the lusts of their hearts to uncleanness, that their bodies should be dishonored among themselves,

Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina. Warumi 1:25

who exchanged the truth of God for a lie, and worshiped and served the creature rather than the Creator, who is blessed forever. Amen.

Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; Warumi 1:26

For this reason, God gave them up to vile passions. For their women changed the natural function into that which is against nature.

wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao. Warumi 1:27

Likewise also the men, leaving the natural function of the woman, burned in their lust toward one another, men doing what is inappropriate with men, and receiving in themselves the due penalty of their error.

Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa. Warumi 1:28

Even as they refused to have God in their knowledge, God gave them up to a reprobate mind, to do those things which are not fitting;

Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya, Warumi 1:29

being filled with all unrighteousness, sexual immorality, wickedness, covetousness, maliciousness; full of envy, murder, strife, deceit, evil habits, secret slanderers,

wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, Warumi 1:30

backbiters, hateful to God, insolent, haughty, boastful, inventors of evil things, disobedient to parents,

wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema; Warumi 1:31

without understanding, covenant-breakers, without natural affection, unforgiving, unmerciful;

ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao. Warumi 1:32

who, knowing the ordinance of God, that those who practice such things are worthy of death, not only do the same, but also approve of those who practice them.