Tito 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Tito 2 (Swahili) Titus 2 (English)

Lakini wewe nena mambo yapasayo mafundisho yenye uzima; Tito 2:1

But say the things which fit sound doctrine,

ya kwamba wazee wawe wenye kiasi, wastahivu, wenye busara, wazima katika imani na katika upendo na katika saburi. Tito 2:2

that older men should be temperate, sensible, sober-minded, sound in faith, in love, and in patience:

Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema; Tito 2:3

and that older women likewise be reverent in behavior, not slanderers nor enslaved to much wine, teachers of that which is good;

ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao; Tito 2:4

that they may train the young women to love their husbands, to love their children,

na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe. Tito 2:5

to be sober-minded, chaste, workers at home, kind, being in subjection to their own husbands, that God's word may not be blasphemed.

Vivyo hivyo na vijana waume uwaonye kuwa na kiasi; Tito 2:6

Likewise, exhort the younger men to be sober-minded;

katika mambo yote ukijionyesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema, na katika mafundisho yako ukionyesha usahihi na ustahivu, Tito 2:7

in all things showing yourself an example of good works; in your teaching showing integrity, seriousness, incorruptibility,

na maneno yenye uzima yasiyoweza kuhukumiwa makosa, ili yule mwenye kupinga atahayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu. Tito 2:8

and soundness of speech that can't be condemned; that he who opposes you may be ashamed, having no evil thing to say about us.

Watumwa na wawatii bwana zao, wakiwapendeza katika mambo yote; wasiwe wenye kujibu, Tito 2:9

Exhort servants to be in subjection to their own masters, and to be well-pleasing in all things; not contradicting;

wasiwe waibaji; bali wauonyeshe uaminifu mwema wote, ili wayapambe mafundisho ya Mwokozi wetu Mungu katika mambo yote. Tito 2:10

not stealing, but showing all good fidelity; that they may adorn the doctrine of God, our Savior, in all things.

Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; Tito 2:11

For the grace of God has appeared, bringing salvation to all men,

nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; Tito 2:12

instructing us to the intent that, denying ungodliness and worldly lusts, we would live soberly, righteously, and godly in this present world;

tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; Tito 2:13

looking for the blessed hope and appearing of the glory of our great God and Savior, Jesus Christ;

ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema. Tito 2:14

who gave himself for us, that he might redeem us from all iniquity, and purify for himself a people for his own possession, zealous for good works.

Nena maneno hayo, onya na kukaripia kwa mamlaka yote; asikudharau mtu awaye yote. Tito 2:15

Say these things and exhort and reprove with all authority. Let no man despise you.