1 Wakorintho 4 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wakorintho 4 (Swahili) 1st Corinthians 4 (English)

Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu. 1 Wakorintho 4:1

So let a man think of us as Christ's servants, and stewards of God's mysteries.

Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu. 1 Wakorintho 4:2

Here, moreover, it is required of stewards, that they be found faithful.

Lakini, kwangu mimi, si kitu kabisa nihukumiwe na ninyi, wala kwa hukumu ya kibinadamu, wala sijihukumu hata nafsi yangu. 1 Wakorintho 4:3

But with me it is a very small thing that I should be judged by you, or by man's judgment. Yes, I don't judge my own self.

Maana sijui sababu ya kujishitaki nafsi yangu, lakini sihesabiwi haki kwa ajili hiyo; ila anihukumuye mimi ni Bwana. 1 Wakorintho 4:4

For I know nothing against myself. Yet I am not justified by this, but he who judges me is the Lord.

Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulikisha yaliyositirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu. 1 Wakorintho 4:5

Therefore judge nothing before the time, until the Lord comes, who will both bring to light the hidden things of darkness, and reveal the counsels of the hearts. Then each man will get his praise from God.

Basi ndugu, mambo hayo nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na Apolo kwa ajili yenu, ili kwamba kwa mfano wetu mpate kujifunza kutokupita yale yaliyoandikwa; ili mmoja wenu asijivune kwa ajili ya huyu, kinyume cha mwenziwe. 1 Wakorintho 4:6

Now these things, brothers, I have in a figure transferred to myself and Apollos for your sakes, that in us you might learn not to think beyond the things which are written, that none of you be puffed up against one another.

Maana ni nani anayekupambanua na mwingine? Nawe una nini usichokipokea? Lakini iwapo ulipokea, wajisifia nini kana kwamba hukupokea? 1 Wakorintho 4:7

For who makes you different? And what do you have that you didn't receive? But if you did receive it, why do you boast as if you had not received it?

Mmekwisha kushiba, mmekwisha kupata utajiri, mmemiliki pasipo sisi. Naam, laiti mngemiliki, ili sisi nasi tumiliki pamoja nanyi! 1 Wakorintho 4:8

You are already filled. You have already become rich. You have come to reign without us. Yes, and I wish that you did reign, that we also might reign with you.

Maana nadhani ya kuwa Mungu ametutoa sisi mitume mwisho, kama watu waliohukumiwa wauawe; kwa sababu tumekuwa tamasha kwa dunia; kwa malaika na wanadamu. 1 Wakorintho 4:9

For, I think that God has displayed us, the apostles, last of all, like men sentenced to death. For we are made a spectacle to the world, both to angels and men.

Sisi tu wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi ni wenye akili katika Kristo; sisi tu dhaifu, lakini ninyi mna nguvu; ninyi mna utukufu, lakini sisi hatupati heshima. 1 Wakorintho 4:10

We are fools for Christ's sake, but you are wise in Christ. We are weak, but you are strong. You have honor, but we have dishonor.

Hata saa hii ya sasa, tuna njaa na kiu, tu uchi, twapigwa ngumi, tena hatuna makao; 1 Wakorintho 4:11

Even to this present hour we hunger, thirst, are naked, are beaten, and have no certain dwelling place.

kisha twataabika tukifanya kazi kwa mikono yetu wenyewe. Tukitukanwa twabariki, tukiudhiwa twastahimili; 1 Wakorintho 4:12

We toil, working with our own hands. When people curse us, we bless. Being persecuted, we endure.

tukisingiziwa twasihi; tumefanywa kama takataka za dunia, na tama ya vitu vyote hata sasa. 1 Wakorintho 4:13

Being defamed, we entreat. We are made as the filth of the world, the dirt wiped off by all, even until now.

Siyaandiki hayo ili kuwatahayarisha; bali kuwaonya kama watoto niwapendao. 1 Wakorintho 4:14

I don't write these things to shame you, but to admonish you as my beloved children.

Kwa kuwa ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo, walakini hamna baba wengi. Maana mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili. 1 Wakorintho 4:15

For though you have ten thousand tutors in Christ, yet not many fathers. For in Christ Jesus, I became your father through the Gospel.

Basi, nawasihi mnifuate mimi. 1 Wakorintho 4:16

I beg you therefore, be imitators of me.

Kwa sababu hii nimemtuma Timotheo kwenu, aliye mwanangu mpendwa, mwaminifu katika Bwana, atakayewakumbusha njia zangu zilizo katika Kristo, kama vile nifundishavyo kila mahali katika kila kanisa. 1 Wakorintho 4:17

Because of this I have sent Timothy to you, who is my beloved and faithful child in the Lord, who will remind you of my ways which are in Christ, even as I teach everywhere in every assembly.

Basi wengine wamejivuna kana kwamba siji kwenu. 1 Wakorintho 4:18

Now some are puffed up, as though I were not coming to you.

Lakini nitakuja kwenu upesi, nikijaliwa, nami nitafahamu, si neno lao tu waliojivuna, bali nguvu zao. 1 Wakorintho 4:19

But I will come to you shortly, if the Lord is willing. And I will know, not the word of those who are puffed up, but the power.

Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu. 1 Wakorintho 4:20

For the Kingdom of God is not in word, but in power.

Mnataka vipi? Nije kwenu na fimbo, au nije katika upendo na roho ya upole? 1 Wakorintho 4:21

What do you want? Shall I come to you with a rod, or in love and a spirit of gentleness?