1 Wakorintho 7 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wakorintho 7 (Swahili) 1st Corinthians 7 (English)

Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke. 1 Wakorintho 7:1

Now concerning the things about which you wrote to me: it is good for a man not to touch a woman.

Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe. 1 Wakorintho 7:2

But, because of sexual immoralities, let each man have his own wife, and let each woman have her own husband.

Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake. 1 Wakorintho 7:3

Let the husband render to his wife the affection owed her, and likewise also the wife to her husband.

Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe. 1 Wakorintho 7:4

The wife doesn't have authority over her own body, but the husband. Likewise also the husband doesn't have authority over his own body, but the wife.

Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu. 1 Wakorintho 7:5

Don't deprive one another, unless it is by consent for a season, that you may give yourselves to fasting and prayer, and may be together again, that Satan doesn't tempt you because of your lack of self-control.

Lakini nasema hayo, kwa kutoa idhini yangu, si kwa amri. 1 Wakorintho 7:6

But this I say by way of concession, not of commandment.

Ila nipendalo ni kwamba watu wote wawe kama mimi nilivyo; walakini kila mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi. 1 Wakorintho 7:7

Yet I wish that all men were like me. However each man has his own gift from God, one of this kind, and another of that kind.

Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo. 1 Wakorintho 7:8

But I say to the unmarried and to widows, it is good for them if they remain even as I am.

Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa. 1 Wakorintho 7:9

But if they don't have self-control, let them marry. For it's better to marry than to burn.

Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe; 1 Wakorintho 7:10

But to the married I command--not I, but the Lord--that the wife not leave her husband

lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe. 1 Wakorintho 7:11

(but if she departs, let her remain unmarried, or else be reconciled to her husband), and that the husband not leave his wife.

Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache. 1 Wakorintho 7:12

But to the rest I--not the Lord--say, if any brother has an unbelieving wife, and she is content to live with him, let him not leave her.

Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe. 1 Wakorintho 7:13

The woman who has an unbelieving husband, and he is content to live with her, let her not leave her husband.

Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu. 1 Wakorintho 7:14

For the unbelieving husband is sanctified in the wife, and the unbelieving wife is sanctified in the husband. Otherwise your children would be unclean, but now are they holy.

Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani. 1 Wakorintho 7:15

Yet if the unbeliever departs, let there be separation. The brother or the sister is not under bondage in such cases, but God has called us in peace.

Kwa maana wajuaje, wewe mwanamke, kama utamwokoa mumeo? Au wajuaje, wewe mwanamume, kama utamwokoa mkeo? 1 Wakorintho 7:16

For how do you know, wife, whether you will save your husband? Or how do you know, husband, whether you will save your wife?

Lakini kama Bwana alivyomgawia kila mtu, kama Mungu alivyomwita kila mtu, na aenende vivyo hivyo. Ndivyo ninavyoagiza katika makanisa yote. 1 Wakorintho 7:17

Only, as the Lord has distributed to each man, as God has called each, so let him walk. So I command in all the assemblies.

Je! Mtu fulani ameitwa hali amekwisha kutahiriwa? Asijifanye kana kwamba hakutahiriwa. Mtu fulani ameitwa hali hajatahiriwa bado? Basi asitahiriwe. 1 Wakorintho 7:18

Was anyone called having been circumcised? Let him not become uncircumcised. Has anyone been called in uncircumcision? Let him not be circumcised.

Kutahiriwa si kitu, na kutokutahiriwa si kitu bali kuzihifadhi amri za Mungu. 1 Wakorintho 7:19

Circumcision is nothing, and uncircumcision is nothing, but the keeping of the commandments of God.

Kila mtu na akae katika hali ile ile ambayo alikuwa nayo alipoitwa. 1 Wakorintho 7:20

Let each man stay in that calling in which he was called.

Je! Uliitwa u mtumwa? Usione ni vibaya lakini kama ukiweza kuwa na uhuru, afadhali kuutumia. 1 Wakorintho 7:21

Were you called being a bondservant? Don't let that bother you, but if you get an opportunity to become free, use it.

Kwa maana yeye aliyeitwa katika Bwana hali ya utumwa, ni huru wa Bwana. Vivyo hivyo yeye naye aliyeitwa hali ya uhuru, ni mtumwa wa Kristo. 1 Wakorintho 7:22

For he who was called in the Lord being a bondservant is the Lord's free man. Likewise he who was called being free is Christ's bondservant.

Mlinunuliwa kwa thamani; msiwe watumwa wa wanadamu. 1 Wakorintho 7:23

You were bought with a price. Don't become bondservants of men.

Ndugu zangu, kila mtu na akae mbele za Mungu katika hali iyo hiyo aliyoitwa nayo. 1 Wakorintho 7:24

Brothers, let each man, in whatever condition he was called, stay in that condition with God.

Kwa habari za wanawali sina amri ya Bwana, lakini natoa shauri langu, mimi niliyejaliwa kwa rehema za Bwana kuwa mwaminifu. 1 Wakorintho 7:25

Now concerning virgins, I have no commandment from the Lord, but I give my judgment as one who has obtained mercy from the Lord to be trustworthy.

Basi, naona hili kuwa jema, kwa ajili ya shida iliyopo, kwamba ni vema mtu akae kama alivyo. 1 Wakorintho 7:26

I think that it is good therefore, because of the distress that is on us, that it is good for a man to be as he is.

Je! Umefungwa kwa mke? Usitake kufunguliwa. Umefunguliwa? Usitafute mke. 1 Wakorintho 7:27

Are you bound to a wife? Don't seek to be freed. Are you free from a wife? Don't seek a wife.

Lakini, kama ukioa, huna hatia; wala mwanamwali akiolewa, hana hatia; lakini watu kama hao watakuwa na dhiki katika mwili nami nataka kuwazuilia hayo. 1 Wakorintho 7:28

But if you marry, you have not sinned. If a virgin marries, she has not sinned. Yet such will have oppression in the flesh, and I want to spare you.

Lakini, ndugu, nasema hivi, muda ubakio si mwingi; basi tokea sasa wale walio na wake na wawe kama hawana; 1 Wakorintho 7:29

But I say this, brothers: the time is short, that from now on, both those who have wives may be as though they had none;

na wale waliao kama hawalii; na wale wafurahio kama hawafurahi; na wale wanunuao, kama hawana kitu. 1 Wakorintho 7:30

and those who weep, as though they didn't weep; and those who rejoice, as though they didn't rejoice; and those who buy, as though they didn't possess;

Na wale wautumiao ulimwengu huu, kama hawautumii sana; kwa maana mambo ya ulimwengu huu yanapita. 1 Wakorintho 7:31

and those who use the world, as not using it to the fullest. For the mode of this world passes away.

Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana; 1 Wakorintho 7:32

But I desire to have you to be free from cares. He who is unmarried is concerned for the things of the Lord, how he may please the Lord;

bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe. 1 Wakorintho 7:33

but he who is married is concerned about the things of the world, how he may please his wife.

Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe. 1 Wakorintho 7:34

There is also a difference between a wife and a virgin. The unmarried woman cares about the things of the Lord, that she may be holy both in body and in spirit. But she who is married cares about the things of the world--how she may please her husband.

Nasema hayo niwafaidie, si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine. 1 Wakorintho 7:35

This I say for your own profit; not that I may ensnare you, but for that which is appropriate, and that you may attend to the Lord without distraction.

Lakini mtu awaye yote akiona ya kuwa hamtendei mwanamwali wake vipendezavyo, na ikiwa huyo amepita uzuri wa ujana wake, na ikiwapo haja, basi, afanye apendavyo, hatendi dhambi, na awaruhusu waoane. 1 Wakorintho 7:36

But if any man thinks that he is behaving inappropriately toward his virgin, if she is past the flower of her age, and if need so requires, let him do what he desires. He doesn't sin. Let them marry.

Lakini yeye aliyesimama kwa uthabiti wa moyo wake, hana sharti, lakini aweza kuyatawala mapenzi yake, tena amekusudia moyoni mwake kumlinda mwanamwali wake, atatenda vema. 1 Wakorintho 7:37

But he who stands steadfast in his heart, having no necessity, but has power over his own heart, to keep his own virgin, does well.

Basi, hivyo na amwozaye mwanamwali wake afanya vema; na yeye asiyemwoza atazidi kufanya vema. 1 Wakorintho 7:38

So then both he who gives his own virgin in marriage does well, and he who doesn't give her in marriage does better.

Mwanamke hufungwa maadamu mumewe yu hai, lakini ikiwa mumewe amefariki, yu huru kuolewa na mtu ye yote amtakaye; katika Bwana tu. 1 Wakorintho 7:39

A wife is bound by law for as long as her husband lives; but if the husband is dead, she is free to be married to whoever she desires, only in the Lord.

Lakini heri yeye zaidi akikaa kama alivyo; ndivyo nionavyo mimi, nami nadhani ya kuwa mimi nami nina Roho wa Mungu. 1 Wakorintho 7:40

But she is happier if she stays as she is, in my judgment, and I think that I also have God's Spirit.