Ezra 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ezra 2 (Swahili) Ezra 2 (English)

Basi hawa ndio wana wa wilaya, waliokwea kutoka katika ule uhamisho wa hao waliokuwa wamechukuliwa, ambao Nebukadneza, mfalme wa Babeli, aliwachukua mateka mpaka Babeli, nao wakarudi Yerusalemu na Yuda, kila mtu mjini kwake; Ezra 2:1

Now these are the children of the province, who went up out of the captivity of those who had been carried away, whom Nebuchadnezzar the king of Babylon had carried away to Babylon, and who returned to Jerusalem and Judah, everyone to his city;

ndio hawa waliokuja pamoja na Zerubabeli, Yoshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu, na Baana. Hii ndiyo hesabu ya wanaume wa watu wa Israeli; Ezra 2:2

who came with Zerubbabel, Jeshua, Nehemiah, Seraiah, Reelaiah, Mordecai, Bilshan, Mispar, Bigvai, Rehum, Baanah. The number of the men of the people of Israel:

wana wa Paroshi, elfu mbili mia moja sabini na wawili. Ezra 2:3

The children of Parosh, two thousand one hundred seventy-two.

Wana wa Shefatia, mia tatu sabini na wawili. Ezra 2:4

The children of Shephatiah, three hundred seventy-two.

Wana wa Ara, mia saba sabini na watano. Ezra 2:5

The children of Arah, seven hundred seventy-five.

Wana wa Pahath-Moabu, wa wana wa Yeshua na Yoabu, elfu mbili mia nane na kumi na wawili. Ezra 2:6

The children of Pahath-moab, of the children of Jeshua [and] Joab, two thousand eight hundred twelve.

Wana wa Elamu, elfu moja mia mbili hamsini na wanne. Ezra 2:7

The children of Elam, one thousand two hundred fifty-four.

Wana wa Zatu, mia kenda arobaini na watano. Ezra 2:8

The children of Zattu, nine hundred forty-five.

Wana wa Zakai, mia saba na sitini. Ezra 2:9

The children of Zaccai, seven hundred sixty.

Wana wa Binui, mia sita arobaini na wawili. Ezra 2:10

The children of Bani, six hundred forty-two.

Wana wa Bebai, mia sita ishirini na watatu. Ezra 2:11

The children of Bebai, six hundred twenty-three.

Wana wa Azgadi, elfu moja mia mbili ishirini na wawili. Ezra 2:12

The children of Azgad, one thousand two hundred twenty-two.

Wana wa Adonikamu, mia sita sitini na sita. Ezra 2:13

The children of Adonikam, six hundred sixty-six.

Wana wa Bigwai, elfu mbili hamsini na sita. Ezra 2:14

The children of Bigvai, two thousand fifty-six.

Wana wa Adini, mia nne hamsini na wanne. Ezra 2:15

The children of Adin, four hundred fifty-four.

Wana wa Ateri, wa wana wa Hezekia, tisini na wanane. Ezra 2:16

The children of Ater, of Hezekiah, ninety-eight.

Wana wa Besai, mia tatu ishirini na watatu. Ezra 2:17

The children of Bezai, three hundred twenty-three.

Wana wa Harifu, mia moja na kumi na wawili. Ezra 2:18

The children of Jorah, one hundred twelve.

Wana wa Hashumu, mia mbili ishirini na watatu. Ezra 2:19

The children of Hashum, two hundred Twenty-three.

Watu wa Gibeoni, tisini na watano. Ezra 2:20

The children of Gibbar, ninety-five.

Watu wa Bethlehemu, mia ishirini na watatu. Ezra 2:21

The children of Bethlehem, one hundred twenty-three.

Watu wa Netofa, hamsini na sita. Ezra 2:22

The men of Netophah, fifty-six.

Watu wa Anathothi, mia ishirini na wanane. Ezra 2:23

The men of Anathoth, one hundred twenty-eight.

Watu wa Beth-Azmawethi, arobaini na wawili. Ezra 2:24

The children of Azmaveth, forty-two.

Watu wa Kiriath-yearimu, na Kefira, na Beerothi, mia saba arobaini na watatu. Ezra 2:25

The children of Kiriath Arim, Chephirah, and Beeroth, seven hundred forty-three.

Watu wa Rama na Geba, mia sita ishirini na mmoja. Ezra 2:26

The children of Ramah and Geba, six hundred twenty-one.

Watu wa Mikmashi, mia moja ishirini na wawili. Ezra 2:27

The men of Michmas, one hundred twenty-two.

Watu wa Betheli, na Ai, mia mbili ishirini na watatu. Ezra 2:28

The men of Bethel and Ai, two hundred twenty-three.

Watu wa Nebo, hamsini na wawili. Ezra 2:29

The children of Nebo, fifty-two.

Watu wa Magbishi, mia moja hamsini na sita. Ezra 2:30

The children of Magbish, one hundred fifty-six.

Watu wa Elamu wa pili, elfu moja mia mbili hamsini na wanne. Ezra 2:31

The children of the other Elam, one thousand two hundred fifty-four.

Watu wa Harimu, mia tatu na ishirini. Ezra 2:32

The children of Harim, three hundred twenty.

Watu wa Lodi, na Hadidi, na Ono, mia saba ishirini na watano. Ezra 2:33

The children of Lod, Hadid, and Ono, seven hundred twenty-five.

Watu wa Yeriko, mia tatu arobaini na watano. Ezra 2:34

The children of Jericho, three hundred forty-five.

Watu wa Senaa, elfu tatu mia sita na thelathini. Ezra 2:35

The children of Senaah, three thousand six hundred thirty.

Makuhani; wana wa Yedaya, wa mbari ya Yeshua, mia kenda sabini na watatu. Ezra 2:36

The priests: the children of Jedaiah, of the house of Jeshua, nine hundred seventy-three.

Wana wa Imeri, elfu moja hamsini na wawili. Ezra 2:37

The children of Immer, one thousand fifty-two.

Wana wa Pashuri, elfu moja mia mbili arobaini na saba. Ezra 2:38

The children of Pashhur, one thousand two hundred forty-seven.

Wana wa Harimu, elfu moja na kumi na saba. Ezra 2:39

The children of Harim, one thousand seventeen.

Walawi; wana wa Yeshua, na wana wa Kadmieli wa wana wa Hodavia, sabini na wanne. Ezra 2:40

The Levites: the children of Jeshua and Kadmiel, of the children of Hodaviah, seventy-four.

Waimbaji; wana wa Asafu, mia moja ishirini na wanane. Ezra 2:41

The singers: the children of Asaph, one hundred twenty-eight.

Akina bawabu; wana wa Shalumu, wana wa Ateri, wana wa Talmoni, wana wa Akubu, wana wa Hatita, wana wa Shobai; jumla yao ni mia moja thelathini na kenda. Ezra 2:42

The children of the porters: the children of Shallum, the children of Ater, the children of Talmon, the children of Akkub, the children of Hatita, the children of Shobai, in all one hundred thirty-nine.

Wanethini; wana wa Siha, wana wa Hasufa, wana wa Tabaothi; Ezra 2:43

The Nethinim: the children of Ziha, the children of Hasupha, the children of Tabbaoth,

wana wa Kerosi, wana wa Siaha, wana wa Padoni; Ezra 2:44

the children of Keros, the children of Siaha, the children of Padon,

wana wa Lebana, wana wa Hagaba, wana wa Akubu; Ezra 2:45

the children of Lebanah, the children of Hagabah, the children of Akkub,

wana wa Hagabu, wana wa Salmai, wana wa Hanani; Ezra 2:46

the children of Hagab, the children of Shamlai, the children of Hanan,

wana wa Gideli, wana wa Gahari, wana wa Reaya; Ezra 2:47

the children of Giddel, the children of Gahar, the children of Reaiah,

wana wa Resini, wana wa Nekoda, wana wa Gazamu; Ezra 2:48

the children of Rezin, the children of Nekoda, the children of Gazzam,

wana wa Uza, wana wa Pasea, wana wa Besai; Ezra 2:49

the children of Uzza, the children of Paseah, the children of Besai,

wana wa Asna, wana wa Meunimu, wana wa Nefusimu; Ezra 2:50

the children of Asnah, the children of Meunim, the children of Nephisim,

wana wa Bakbuki, wana wa Hakufa, wana wa Harhuri; Ezra 2:51

the children of Bakbuk, the children of Hakupha, the children of Harhur,

wana wa Basluthi, wana wa Mehida, wana wa Harsha; Ezra 2:52

the children of Bazluth, the children of Mehida, the children of Harsha,

wana wa Barkosi, wana wa Sisera, wana wa Tema; Ezra 2:53

the children of Barkos, the children of Sisera, the children of Temah,

wana wa Nesia, wana wa Hatifa. Ezra 2:54

the children of Neziah, the children of Hatipha.

Wa watumwa wa Sulemani; wana wa Sotai, wana wa Soferethi, wana wa Peruda; Ezra 2:55

The children of Solomon's servants: the children of Sotai, the children of Hassophereth, the children of Peruda,

wana wa Yaala, wana wa Darkoni, wana wa Gideli; Ezra 2:56

the children of Jaalah, the children of Darkon, the children of Giddel,

wana wa Shefatia, wana wa Hatili, wana wa Pokereth-Sebaimu, wana wa Amoni. Ezra 2:57

the children of Shephatiah, the children of Hattil, the children of Pochereth-hazzebaim, the children of Ami.

Wanethini wote, pamoja na watumwa wa Sulemani, walikuwa mia tatu tisini na wawili. Ezra 2:58

All the Nethinim, and the children of Solomon's servants, were three hundred ninety-two.

Na hawa ndio watu waliokwea kutoka Tel-mela, na Tel-harsha, na Kerubu, na Adani, na Imeri; walakini hawakuweza kuonyesha mbari za baba zao, wala kizazi chao, kwamba walikuwa wa Israeli; Ezra 2:59

These were those who went up from Tel-melah, Tel Harsha, Cherub, Addan, [and] Immer; but they could not show their fathers' houses, and their seed, whether they were of Israel:

wana wa Delaya, wana wa Tobia, wana wa Nekoda, mia sita hamsini na wawili. Ezra 2:60

the children of Delaiah, the children of Tobiah, the children of Nekoda, six hundred fifty-two.

Tena wa makuhani; wana wa Habaya, wana wa Hakosi, wana wa Barzilai, yule aliyeoa mmojawapo wa binti Barzilai, Mgileadi, akaitwa kwa jina lao. Ezra 2:61

Of the children of the priests: the children of Habaiah, the children of Hakkoz, the children of Barzillai, who took a wife of the daughters of Barzillai the Gileadite, and was called after their name.

Hao waliitafuta orodha yao miongoni mwa wale waliohesabiwa kwa nasaba, wasionekane; kwa hiyo walihesabiwa kuwa na unajisi. Ezra 2:62

These sought their register [among] those who were reckoned by genealogy, but they were not found: therefore were they deemed polluted and put from the priesthood.

Na huyo Tirshatha akawaambia wasile katika vitu vitakatifu sana ,hata atakaposimama kuhani mwenye urimu na Thumimu. Ezra 2:63

The governor said to them, that they should not eat of the most holy things, until there stood up a priest with Urim and with Thummim.

Basi hilo kusanyiko lote zima, jumla yake ilikuwa watu arobaini na mbili elfu na mia tatu na sitini, Ezra 2:64

The whole assembly together was forty-two thousand three hundred sixty,

tena, zaidi ya hao, kulikuwa na watumishi wao waume kwa wake, ambao walikuwa saba elfu, na mia tatu na thelathini na saba; nao walikuwa na waimbaji waume kwa wake mia mbili. Ezra 2:65

besides their men-servants and their maid-servants, of whom there were seven thousand three hundred thirty-seven: and they had two hundred singing men and singing women.

Farasi zao walikuwa mia saba thelathini na sita; nyumbu zao, mia mbili arobaini na watano; Ezra 2:66

Their horses were seven hundred thirty-six; their mules, two hundred forty-five;

ngamia zao, mia nne thelathini na watano; punda zao elfu sita, na mia saba na ishirini. Ezra 2:67

their camels, four hundred thirty-five; [their] donkeys, six thousand seven hundred and twenty.

Na baadhi ya wakuu wa mbari za baba zao, hapo walipoifikilia nyumba ya Bwana, iliyoko Yerusalemu, walitoa mali kwa ukarimu kwa ajili ya nyumba ya Mungu, ili kuisimamisha mahali pake; Ezra 2:68

Some of the heads of fathers' [houses], when they came to the house of Yahweh which is in Jerusalem, offered willingly for the house of God to set it up in its place:

wakatoa kadiri walivyoweza, na kutia katika hazina ya kazi hiyo, darkoni za dhahabu sitini na moja elfu ,na nane za fedha elfu tano,na mavazi mia ya makuhani. Ezra 2:69

they gave after their ability into the treasury of the work sixty-one thousand darics of gold, and five thousand minas of silver, and one hundred priests' garments.

Hivyo makuhani, na Walawi, na baadhi ya watu, na waimbaji, na mabawabu, na Wanethini, wakakaa mijini mwao, naam, Israeli wote wakakaa mijini mwao. Ezra 2:70

So the priests, and the Levites, and some of the people, and the singers, and the porters, and the Nethinim, lived in their cities, and all Israel in their cities.