Waamuzi 12 Swahili & English

Listen/Download Audio
Waamuzi 12 (Swahili) Judges 12 (English)

Kisha watu wa Efraimu walikutana pamoja na kupita kwenda upande wa kaskazini; wakamwambia Yeftha, Kwa nini wewe kuvuka kwenda kupigana na wana wa Amoni, nawe hukutuita sisi kwenda pamoja nawe? Tutaipiga moto nyumba yako juu yako. Waamuzi 12:1

The men of Ephraim were gathered together, and passed northward; and they said to Jephthah, Why did you pass over to fight against the children of Ammon, and didn't call us to go with you? we will burn your house on you with fire.

Yeftha akawaambia, Mimi na watu wangu tulikuwa na matata makubwa na wana wa Amoni; nami hapo nilipowaita ninyi, hamkuniokoa na mikono yao. Waamuzi 12:2

Jephthah said to them, I and my people were at great strife with the children of Ammon; and when I called you, you didn't save me out of their hand.

Nami nilipoona ya kuwa ninyi hamniokoi, niliuhatirisha uhai wangu, na kuvuka ili nipigane na wana wa Amoni, Bwana naye akawatia mkononi mwangu; basi kwa nini ninyi kunijia hivi leo kutaka kupigana nami? Waamuzi 12:3

When I saw that you didn't save me, I put my life in my hand, and passed over against the children of Ammon, and Yahweh delivered them into my hand: why then are you come up to me this day, to fight against me?

Ndipo Yeftha akawakutanisha watu wote wa Gileadi, na kupigana na Efraimu; na hao watu wa Gileadi wakawapiga Efraimu, kwa sababu walisema, Ninyi Wagileadi ni watoro mliotoroka Efraimu, mnaokaa kati ya Efraimu, na kati ya Manase. Waamuzi 12:4

Then Jephthah gathered together all the men of Gilead, and fought with Ephraim; and the men of Gilead struck Ephraim, because they said, You are fugitives of Ephraim, you Gileadites, in the midst of Ephraim, [and] in the midst of Manasseh.

Nao Wagileadi wakavishika vivuko vya Yordani kinyume cha hao Waefraimu; kisha ilikuwa, hapo watoro waliotoroka Efraimu mmojawapo aliposema Niache nivuke, hao watu wa Gileadi wakamwambia, Je! Wewe u Mwefraimu? Kwamba alisema, La; Waamuzi 12:5

The Gileadites took the fords of the Jordan against the Ephraimites. It was so, that when [any of] the fugitives of Ephraim said, Let me go over, the men of Gilead said to him, Are you an Ephraimite? If he said, No;

ndipo wakamwambia, Haya, tamka sasa neno hili, Shibolethi; naye akasema, Sibolethi; kwa maana hakuweza kufanya midomo yake kutamka neno hilo sawasawa; ndipo wakamshika, na kumwua hapo penye vivuko vya Yordani; basi wakaanguka wakati huo watu arobaini na mbili elfu wa Efraimu. Waamuzi 12:6

then said they to him, Say now Shibboleth; and he said Sibboleth; for he couldn't manage to pronounce it right: then they laid hold on him, and killed him at the fords of the Jordan. There fell at that time of Ephraim forty-two thousand.

Huyo Yeftha akawa mwamuzi wa Israeli muda wa miaka sita. Ndipo akafa Yeftha, Mgileadi, akazikwa katika miji ya Gileadi mmojawapo. Waamuzi 12:7

Jephthah judged Israel six years. Then died Jephthah the Gileadite, and was buried in [one of] the cities of Gilead.

Baada yake huyo, Ibzani wa Bethlehemu akawa mwamuzi wa Israeli. Waamuzi 12:8

After him Ibzan of Bethlehem judged Israel.

Alikuwa na wana thelathini; na binti thelathini akawapeleka waende mahali pengine, kisha akaleta wanawake thelathini kutoka mahali pengine kwa ajili ya hao wanawe. Akawa mwamuzi wa Israeli muda wa miaka saba. Waamuzi 12:9

He had thirty sons; and thirty daughters he sent abroad, and thirty daughters he brought in from abroad for his sons. He judged Israel seven years.

Huyo Ibzani akafa, akazikwa huko Bethlehemu. Waamuzi 12:10

Ibzan died, and was buried at Bethlehem.

Baada yake huyo, Eloni, Mzabuloni, akawa mwamuzi wa Israeli akawaamua Israeli muda wa miaka kumi. Waamuzi 12:11

After him Elon the Zebulunite judged Israel; and he judged Israel ten years.

Huyo Eloni, Mzabuloni, akafa, akazikwa katika Aiyaloni katika nchi ya Zabuloni. Waamuzi 12:12

Elon the Zebulunite died, and was buried in Aijalon in the land of Zebulun.

Baada yake huyo, Abdoni mwana wa Hileli, Mpirathoni, akawa mwamuzi wa Israeli. Waamuzi 12:13

After him Abdon the son of Hillel the Pirathonite judged Israel.

Naye alikuwa na wana arobaini, na wajukuu thelathini, waliokuwa wakipanda wana-punda sabini; akawa mwamuzi wa Israeli muda wa miaka minane. Waamuzi 12:14

He had forty sons and thirty sons' sons, who rode on seventy donkey colts: and he judged Israel eight years.

Huyo Abdoni mwana wa Hileli, Mpirathoni, akafa, akazikwa huko Pirathoni katika nchi ya Efraimu, katika nchi ya vilima ya Waamaleki. Waamuzi 12:15

Abdon the son of Hillel the Pirathonite died, and was buried in Pirathon in the land of Ephraim, in the hill-country of the Amalekites.