Waamuzi 17 Swahili & English

Listen/Download Audio
Waamuzi 17 (Swahili) Judges 17 (English)

Wakati huo alikuwako mtu mmoja wa nchi ya vilima ya Efraimu, ambaye jina lake alikuwa akiitwa Mika. Waamuzi 17:1

There was a man of the hill-country of Ephraim, whose name was Micah.

Naye akamwambia mama yake, Hizo fedha elfu na mia moja ulizonyang'anywa, ambazo uliweka kiapo kwa ajili yake na kusema masikioni mwangu, tazama, ninazo mimi hizo fedha; ni mimi niliyezitwaa. Mama yake akasema, mwanangu na abarikiwe na Bwana. Waamuzi 17:2

He said to his mother, The eleven hundred [pieces] of silver that were taken from you, about which you did utter a curse, and did also speak it in my ears, behold, the silver is with me; I took it. His mother said, Blessed be my son of Yahweh.

Basi akamrudishia mama yake hizo fedha elfu na mia moja. Mama yake akasema, Mimi naziweka fedha hizi kabisa ziwe wakfu kwa Bwana, zitoke mkononi mwangu kwa ajili ya mwanangu, ili kufanya sanamu ya kuchonga, na sanamu ya kusubu; basi kwa hiyo nakurudishia wewe. Waamuzi 17:3

He restored the eleven hundred [pieces] of silver to his mother; and his mother said, I most assuredly dedicate the silver to Yahweh from my hand for my son, to make an engraved image and a molten image: now therefore I will restore it to you.

Basi hapo alipomrudishia mama yake hizo fedha, mama yake akatwaa fedha mia mbili, akampa fundi mwenye kusubu fedha, naye akafanya sanamu ya kuchonga kwazo, na sanamu ya kusubu; ambazo zilikuwa ndani ya nyumba ya Mika. Waamuzi 17:4

When he restored the money to his mother, his mother took two hundred [pieces] of silver, and gave them to the founder, who made of it an engraved image and a molten image: and it was in the house of Micah.

Basi mtu huyo Mika alikuwa na nyumba ya miungu, naye akafanya naivera, na kinyago, akamweka wakfu mmoja miongoni mwa wanawe, akawa kuhani wake. Waamuzi 17:5

The man Micah had a house of gods, and he made an ephod, and teraphim, and consecrated one of his sons, who became his priest.

Siku hizo hapakuwa na mfalme katika israeli; kila mtu alifanya hayo aliyoyaona kuwa ni mema machoni pake mwenyewe. Waamuzi 17:6

In those days there was no king in Israel: every man did that which was right in his own eyes.

Alikuwako mtu mmoja hirimu aliyetoka Bethlehemu-yuda, wa jamaa ya Yuda, aliyekuwa ni Mlawi, naye akakaa huko hali ya ugeni. Waamuzi 17:7

There was a young man out of Bethlehem Judah, of the family of Judah, who was a Levite; and he sojourned there.

Mtu huyo akatoka katika huo mji, katika Bethlehemu-yuda, ili aende kukaa hali ya ugeni hapo atakapoona mahali; akafikilia nchi ya vilima vilima ya Efraimu katika safari yake, hata nyumba ya huyo Mika. Waamuzi 17:8

The man departed out of the city, out of Bethlehem Judah, to sojourn where he could find [a place], and he came to the hill-country of Ephraim to the house of Micah, as he traveled.

Mika akamwuliza, Watoka wapi wewe? Akamwambia, Mimi ni Mlawi wa Bethlehemu-yuda, nami naenda kukaa hali ya ugeni po pote nitakapoona mahali. Waamuzi 17:9

Micah said to him, Whence come you? He said to him, I am a Levite of Bethlehem Judah, and I go to sojourn where I may find [a place].

Mika akamwambia, kaa pamoja nami, uwe kwangu baba, tena kuhani, nami nitakupa fedha kumi mwaka kwa mwaka, na nguo ya kuvaa, na vyakula. Basi huyo Mlawi akaingia ndani. Waamuzi 17:10

Micah said to him, Dwell with me, and be to me a father and a priest, and I will give you ten [pieces] of silver by the year, and a suit of clothing, and your food. So the Levite went in.

Huyo Mlawi aliridhika kukaa na mtu huyo; kisha huyo hirimu akawa kwake kama wanawe mmojawapo. Waamuzi 17:11

The Levite was content to dwell with the man; and the young man was to him as one of his sons.

Basi Mika akamweka wakfu huyo Mlawi, huyo hirimu, naye akawa kuhani wake, akakaa nyumbani mwa Mika. Waamuzi 17:12

Micah consecrated the Levite, and the young man became his priest, and was in the house of Micah.

Ndipo Mika akasema, Sasa najua ya kwamba Bwana atanitendea mema, kwa kuwa nina Mlawi kuwa kuhani wangu. Waamuzi 17:13

Then said Micah, Now know I that Yahweh will do me good, seeing I have a Levite to my priest.