Mathayo 19 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mathayo 19 (Swahili) Matthew 19 (English)

Ikawa Yesu alipomaliza maneno hayo, akatoka Galilaya akafika mipaka ya Uyahudi, ng'ambo ya Yordani. Mathayo 19:1

It happened when Jesus had finished these words, he departed from Galilee, and came into the borders of Judea beyond the Jordan.

Makutano mengi wakamfuata, akawaponya huko. Mathayo 19:2

Great multitudes followed him, and he healed them there.

Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu? Mathayo 19:3

Pharisees came to him, testing him, and saying, "Is it lawful for a man to divorce his wife for any reason?"

Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, Mathayo 19:4

He answered, "Haven't you read that he who made them from the beginning made them male and female,

akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja? Mathayo 19:5

and said, 'For this cause a man shall leave his father and mother, and shall join to his wife; and the two shall become one flesh?'

Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe. Mathayo 19:6

So that they are no more two, but one flesh. What therefore God has joined together, don't let man tear apart."

Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha? Mathayo 19:7

They asked him, "Why then did Moses command us to give her a bill of divorce, and divorce her?"

Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. Mathayo 19:8

He said to them, "Moses, because of the hardness of your hearts, allowed you to divorce your wives, but from the beginning it has not been so.

Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini. Mathayo 19:9

I tell you that whoever divorces his wife, except for sexual immorality, and marries another, commits adultery; and he who marries her when she is divorced commits adultery."

Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa. Mathayo 19:10

His disciples said to him, "If this is the case of the man with his wife, it is not expedient to marry."

Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa. Mathayo 19:11

But he said to them, "Not all men can receive this saying, but those to whom it is given.

Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee. Mathayo 19:12

For there are eunuchs who were born that way from their mother's womb, and there are eunuchs who were made eunuchs by men; and there are eunuchs who made themselves eunuchs for the Kingdom of Heaven's sake. He who is able to receive it, let him receive it."

Ndipo akaletewa watoto wadogo ili aweke mikono yake juu yao na kuwaombea; wanafunzi wake wakawakemea. Mathayo 19:13

Then little children were brought to him, that he should lay his hands on them and pray; and the disciples rebuked them.

Lakini Yesu akasema, Waacheni watoto wadogo waje kwangu; wala msiwazuie; kwa maana walio mfano wa hao, ufalme wa mbinguni ni wao. Mathayo 19:14

But Jesus said, "Allow the little children, and don't forbid them to come to me; for to such belongs the Kingdom of Heaven."

Akaweka mikono yake juu yao, akatoka huko. Mathayo 19:15

He laid his hands on them, and departed from there.

Na tazama, mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu, nitende jambo gani jema, ili nipate uzima wa milele? Mathayo 19:16

Behold, one came to him and said, "Good teacher, what good thing shall I do, that I may have eternal life?"

Akamwambia Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri. Mathayo 19:17

He said to him, "Why do you call me good? No one is good but one, that is, God. But if you want to enter into life, keep the commandments."

Akamwambia, Zipi? Yesu akasema, Ni hizi, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Mathayo 19:18

He said to him, "Which ones?" Jesus said, "'You shall not murder.' 'You shall not commit adultery.' 'You shall not steal.' 'You shall not offer false testimony.'

Waheshimu baba yako na mama yako, na, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Mathayo 19:19

'Honor your father and mother.' And, 'You shall love your neighbor as yourself.'"

Yule kijana akamwambia, Haya yote nimeyashika; nimepungukiwa na nini tena? Mathayo 19:20

The young man said to him, "All these things I have observed from my youth. What do I still lack?"

Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate. Mathayo 19:21

Jesus said to him, "If you want to be perfect, go, sell what you have, and give to the poor, and you will have treasure in heaven; and come, follow me."

Yule kijana alipolisikia neno lile, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi. Mathayo 19:22

But when the young man heard the saying, he went away sad, for he was one who had great possessions.

Yesu akawaambia wanafunzi wake, Amin, nawaambieni, ya kwamba itakuwa shida tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni. Mathayo 19:23

Jesus said to his disciples, "Most assuredly I say to you, a rich man will enter into the Kingdom of Heaven with difficulty.

Nawaambia tena, Ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu ya sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu. Mathayo 19:24

Again I tell you, it is easier for a camel to go through a needle's eye, than for a rich man to enter into the Kingdom of God."

Wanafunzi waliposikia, walishangaa mno, wakisema, Ni nani basi awezaye kuokoka? Mathayo 19:25

When the disciples heard it, they were exceedingly astonished, saying, "Who then can be saved?"

Yesu akawakazia macho, akawaambia, Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana. Mathayo 19:26

Looking at them, Jesus said, "With men this is impossible, but with God all things are possible."

Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi? Mathayo 19:27

Then Peter answered, "Behold, we have left everything, and followed you. What then will we have?"

Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli. Mathayo 19:28

Jesus said to them, "Most assuredly I tell you that you who have followed me, in the regeneration when the Son of Man will sit on the throne of his glory, you also will sit on twelve thrones, judging the twelve tribes of Israel.

Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele. Mathayo 19:29

Everyone who has left houses, or brothers, or sisters, or father, or mother, or wife, or children, or lands, for my name's sake, will receive one hundred times, and will inherit eternal life.

Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.

Mathayo 19:30

But many will be last who are first; and first who are last.