Mathayo 11 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mathayo 11 (Swahili) Matthew 11 (English)

Ikawa Yesu alipokwisha kuwaagiza wanafunzi wake kumi na wawili, alitoka huko kwenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao. Mathayo 11:1

It happened that when Jesus had finished directing his twelve disciples, he departed from there to teach and preach in their cities.

Naye Yohana aliposikia huko gerezani matendo yake Kristo, alituma wanafunzi wake, kumwuliza, Mathayo 11:2

Now when John heard in the prison the works of Christ, he sent two of his disciples

Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine? Mathayo 11:3

and said to him, "Are you he who comes, or should we look for another?"

Yesu akajibu akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana mnayoyasikia na kuyaona; Mathayo 11:4

Jesus answered them, "Go and tell John the things which you hear and see:

vipofu wanapata kuona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa habari njema. Mathayo 11:5

the blind receive their sight, the lame walk, the lepers are cleansed, the deaf hear, the dead are raised up, and the poor have good news preached to them.

Naye heri awaye yote asiyechukizwa nami. Mathayo 11:6

Blessed is he who finds no occasion for stumbling in me."

Na hao walipokwenda zao, Yesu alianza kuwaambia makutano habari za Yohana, Mlitoka kwenda nyikani kutazama nini? Unyasi ukitikiswa na upepo? Mathayo 11:7

As these went their way, Jesus began to say to the multitudes concerning John, "What did you go out into the wilderness to see? A reed shaken by the wind?

Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi mororo? Tazama, watu wavaao mavazi mororo wamo katika nyumba za wafalme. Mathayo 11:8

But what did you go out to see? A man in soft clothing? Behold, those who wear soft clothing are in king's houses.

Lakini kwa nini mlitoka? Ni kuona nabii? Naam, nawaambia, na aliye mkuu zaidi ya nabii. Mathayo 11:9

But why did you go out? To see a prophet? Yes, I tell you, and much more than a prophet.

Huyo ndiye aliyeandikiwa haya, Tazama, mimi namtuma mjumbe wangu Mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njia yako mbele yako. Mathayo 11:10

For this is he, of whom it is written, 'Behold, I send my messenger before your face, who will prepare your way before you.'

Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye. Mathayo 11:11

Most assuredly I tell you, among those who are born of women there has not arisen anyone greater than John the Baptizer; yet he who is least in the Kingdom of Heaven is greater than he.

Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka. Mathayo 11:12

From the days of John the Baptizer until now, the Kingdom of Heaven suffers violence, and the violent take it by force.

Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana. Mathayo 11:13

For all the prophets and the law prophesied until John.

Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja. Mathayo 11:14

If you are willing to receive it, this is Elijah, who is to come.

Mwenye masikio, na asikie. Mathayo 11:15

He who has ears to hear, let him hear.

Lakini nitakifananisha na nini kizazi hiki? Kimefanana na watoto wanaokaa sokoni, wanaowaita wenzao, wakisema, Mathayo 11:16

"But to what shall I compare this generation? It is like children sitting in the marketplaces, who call to their companions

Tuliwapigia filimbi, wala hamkucheza; tuliomboleza, wala hamkulia. Mathayo 11:17

and say, 'We played the flute for you, and you didn't dance. We mourned for you, and you didn't lament.'

Maana Yohana alikuja, hali wala hanywi, wakasema, Yuna pepo. Mathayo 11:18

For John came neither eating nor drinking, and they say, 'He has a demon.'

Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa kazi zake. Mathayo 11:19

The Son of Man came eating and drinking, and they say, 'Behold, a gluttonous man and a drunkard, a friend of tax collectors and sinners!' But wisdom is justified by her children."

Ndipo akaanza kuikemea miji ile ambamo ndani yake ilifanyika miujiza yake iliyo mingi, kwa sababu haikutubu. Mathayo 11:20

Then he began to denounce the cities in which most of his mighty works had been done, because they didn't repent.

Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na majivu. Mathayo 11:21

"Woe to you, Chorazin! Woe to you, Bethsaida! For if the mighty works had been done in Tyre and Sidon which were done in you, they would have repented long ago in sackcloth and ashes.

Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zao siku ya hukumu kuliko ninyi. Mathayo 11:22

But I tell you, it will be more tolerable for Tyre and Sidon on the day of judgment than for you.

Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo. Mathayo 11:23

You, Capernaum, who are exalted to Heaven, you will go down to Hades. For if the mighty works had been done in Sodom which were done in you, it would have remained until this day.

Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma kustahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe. Mathayo 11:24

But I tell you that it will be more tolerable for the land of Sodom, on the day of judgment, than for you."

Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Mathayo 11:25

At that time, Jesus answered, "I thank you, Father, Lord of heaven and earth, that you hid these things from the wise and understanding, and revealed them to infants.

Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako. Mathayo 11:26

Yes, Father, for so it was well-pleasing in your sight.

Akasema, Nimekabidhiwa vyote na baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia. Mathayo 11:27

All things have been delivered to me by my Father. No one knows the Son, except the Father; neither does anyone know the Father, except the Son, and he to whom the Son desires to reveal him.

Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Mathayo 11:28

"Come to me, all you who labor and are heavily burdened, and I will give you rest.

Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; Mathayo 11:29

Take my yoke upon you, and learn from me, for I am gentle and lowly in heart; and you will find rest for your souls.

kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi. Mathayo 11:30

For my yoke is easy, and my burden is light."