Sefania 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Sefania 2 (Swahili) Zephaniah 2 (English)

Jikusanyeni, naam, jikusanyeni, Ee taifa lisilo na haya; Sefania 2:1

Gather yourselves together, yes, gather together, you nation that has no shame,

kabla haijazaa hiyo amri, kabla haijapita siku ile kama makapi, kabla haijawajilia hasira kali ya Bwana, kabla haijawajilia siku ya hasira ya Bwana. Sefania 2:2

before the appointed time when the day passes as the chaff, before the fierce anger of Yahweh comes on you, before the day of Yahweh's anger comes on you.

Mtafuteni Bwana, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitenda hukumu zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya Bwana. Sefania 2:3

Seek Yahweh, all you humble of the land, who have kept his ordinances. Seek righteousness. Seek humility. It may be that you will be hidden in the day of Yahweh's anger.

Kwa kuwa Gaza utaachwa, na Ashkeloni utakuwa ukiwa; wataufukuzia mbali Ashdodi wakati wa adhuhuri, na Ekroni utang'olewa. Sefania 2:4

For Gaza will be forsaken, and Ashkelon a desolation. They will drive out Ashdod at noonday, and Ekron will be rooted up.

Ole wao wakaao karibu na pwani ya bahari, taifa la Wakerethi! Neno la Bwana li juu yenu, Ee Kanaani, nchi ya Wafilisti; mimi nitakuangamiza, asibaki mtu akaaye kwako. Sefania 2:5

Woe to the inhabitants of the sea coast, the nation of the Cherethites! The word of Yahweh is against you, Canaan, the land of the Philistines. I will destroy you, that there will be no inhabitant.

Na hiyo nchi ya pwani itakuwa malisho, yenye vibanda vya wachungaji, na mazizi ya makundi ya kondoo. Sefania 2:6

The sea coast will be pastures, with cottages for shepherds and folds for flocks.

Na hiyo nchi ya pwani itakuwa nchi ya watu wa nyumba ya Yuda waliosalia; watalisha makundi yao huko; watalala katika nyumba za Ashkeloni wakati wa jioni; kwa maana Bwana, Mungu wao, atawajilia na kuwarudisha wafungwa wao. Sefania 2:7

The coast will be for the remnant of the house of Judah. They will find pasture. In the houses of Ashkelon, they will lie down in the evening, for Yahweh, their God, will visit them, and restore them.

Mimi nimeyasikia matukano ya Moabu, na dhihaka za wana wa Amoni, ambazo kwa hizo wamewatukana watu wangu, na kujitukuza juu ya mpaka wao. Sefania 2:8

I have heard the reproach of Moab, and the insults of the children of Ammon, with which they have reproached my people, and magnified themselves against their border.

Basi kama niishivyo, asema Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, Hakika Moabu atakuwa kama Sodoma, na wana wa Amoni kama Gomora, yaani, milki ya upupu, na mashimo ya chumvi, ukiwa wa daima; watu wangu waliosalia watawateka nyara, na watu wa taifa langu waliobaki watawarithi. Sefania 2:9

Therefore as I live, says Yahweh of Hosts, the God of Israel, surely Moab will be as Sodom, and the children of Ammon as Gomorrah, a possession of nettles, and salt pits, and a perpetual desolation. The remnant of my people will plunder them, and the survivors of my nation will inherit them.

Mambo hayo yatawapata kwa sababu ya kiburi chao, kwa kuwa wamewatukana watu wa Bwana wa majeshi, na kujitukuza juu yao. Sefania 2:10

This they will have for their pride, because they have reproached and magnified themselves against the people of Yahweh of Hosts.

Bwana atakuwa mwenye kuwatisha sana; kwa maana atawafisha kwa njaa miungu yote ya dunia; na watu watamsujudia yeye, kila mtu toka mahali pake; naam, nchi zote za mataifa. Sefania 2:11

Yahweh will be awesome to them, for he will famish all the gods of the land. Men will worship him, everyone from his place, even all the shores of the nations.

Na ninyi Wakushi pia, mtauawa kwa upanga wangu. Sefania 2:12

You Cushites also, you will be killed by my sword.

Naye atanyosha mkono wake juu ya upande wa kaskazini, na kuiangamiza Ashuru; naye ataufanya Ninawi kuwa ukiwa, kuwa mahali pakavu kama jangwa. Sefania 2:13

He will stretch out his hand against the north, destroy Assyria, and will make Nineveh a desolation, and dry like the wilderness.

Na makundi ya wanyama watalala kati yake, wanyama wote wa mataifa; mwari-nyuni na nungu watakaa juu ya vichwa vya nguzo zake; sauti yao itasikiwa madirishani; vizingitini mwake mtakuwa ukiwa; kwa maana ameifunua kazi ya mierezi. Sefania 2:14

Herds will lie down in the midst of her, all the animals of the nations. Both the pelican and the porcupine will lodge in its capitals. Their calls will echo through the windows. Desolation will be in the thresholds, for he has laid bare the cedar beams.

Huu ndio mji ule wa furaha, Uliokaa pasipo kufikiri, Uliosema moyoni mwake, Mimi niko, Wala hapana mwingine ila mimi. Jinsi ulivyokuwa ukiwa, Mahali pa kulala pa wanyama wa bara! Kila mtu apitaye atazomea, Na kutikisa mkono wake. Sefania 2:15

This is the joyous city that lived carelessly, that said in her heart, "I am, and there is none besides me." How she has become a desolation, a place for animals to lie down in! Everyone who passes by her will hiss, and shake their fists.