1 Mambo ya Nyakati 16 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Mambo ya Nyakati 16 (Swahili) 1st Chronicles 16 (English)

Wakaliingiza sanduku la Mungu, na kuliweka katikati ya hema aliyoipiga Daudi kwa ajili yake; wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Mungu. 1 Mambo ya Nyakati 16:1

They brought in the ark of God, and set it in the midst of the tent that David had pitched for it: and they offered burnt offerings and peace-offerings before God.

Na Daudi alipokwisha kuitoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani, akawabariki watu kwa jina la Bwana. 1 Mambo ya Nyakati 16:2

When David had made an end of offering the burnt offering and the peace-offerings, he blessed the people in the name of Yahweh.

Kisha akawagawia kila mtu wa Israeli, waume kwa wake, kila mtu mkate wa ngano, na kipande cha nyama, na mkate wa zabibu. 1 Mambo ya Nyakati 16:3

He dealt to everyone of Israel, both man and woman, to every one a loaf of bread, and a portion [of flesh], and a cake of raisins.

Akawaagiza baadhi ya Walawi kwamba watumike mbele ya sanduku la Bwana, wamfanyie ukumbusho, na shukrani, na sifa, Bwana, Mungu wa Israeli; 1 Mambo ya Nyakati 16:4

He appointed certain of the Levites to minister before the ark of Yahweh, and to celebrate and to thank and praise Yahweh, the God of Israel:

Asafu mkuu wao, na wa pili wake Zekaria, na Yeieli, na Shemiramothi, na Yehieli, na Matithiya, na Eliabu, na Benaya, na Obed-edomu, na Yeieli, wenye vinanda na vinubi; naye Asafu mwenye kupiga matoazi; 1 Mambo ya Nyakati 16:5

Asaph the chief, and second to him Zechariah, Jeiel, and Shemiramoth, and Jehiel, and Mattithiah, and Eliab, and Benaiah, and Obed-edom, and Jeiel, with psalteries and with harps; and Asaph with cymbals, sounding aloud;

nao makuhani Benaya na Yahazieli wenye baragumu daima, mbele ya sanduku la agano la Mungu. 1 Mambo ya Nyakati 16:6

and Benaiah and Jahaziel the priests with trumpets continually, before the ark of the covenant of God.

Ndipo siku hiyo Daudi alipoagiza kwanza kumshukuru Bwana, kwa mkono wa Asafu na nduguze. 1 Mambo ya Nyakati 16:7

Then on that day David first ordained to give thanks to Yahweh, by the hand of Asaph and his brothers.

Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake; Wajulisheni watu matendo yake. 1 Mambo ya Nyakati 16:8

Oh give thanks to Yahweh, call on his name; Make known his doings among the peoples.

Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi; Zitafakarini ajabu zake zote. 1 Mambo ya Nyakati 16:9

Sing to him, sing praises to him; Talk you of all his marvelous works.

Jisifuni kwa jina lake takatifu; Na ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana. 1 Mambo ya Nyakati 16:10

Glory you in his holy name; Let the heart of them rejoice who seek Yahweh.

Mtakeni Bwana na nguvu zake; Utafuteni uso wake siku zote. 1 Mambo ya Nyakati 16:11

Seek you Yahweh and his strength; Seek his face forever more.

Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya; Miujiza yake na hukumu za kinywa chake; 1 Mambo ya Nyakati 16:12

Remember his marvelous works that he has done, His wonders, and the judgments of his mouth,

Enyi wazao wa Israeli, mtumishi wake, Enyi wana wa Yakobo, wateule wake. 1 Mambo ya Nyakati 16:13

You seed of Israel his servant, You children of Jacob, his chosen ones.

Yeye, Bwana, ndiye Mungu wetu; Duniani mwote mna hukumu zake. 1 Mambo ya Nyakati 16:14

He is Yahweh our God; His judgments are in all the earth.

Likumbukeni agano lake milele, Neno lile aliloviamuru vizazi elfu. 1 Mambo ya Nyakati 16:15

Remember his covenant forever, The word which he commanded to a thousand generations,

Agano alilofanya na Ibrahimu, Na uapo wake kwa Isaka; 1 Mambo ya Nyakati 16:16

[The covenant] which he made with Abraham, His oath to Isaac,

Alilomthibitishia Yakobo kuwa amri, Na Israeli liwe agano la milele. 1 Mambo ya Nyakati 16:17

Confirmed the same to Jacob for a statute, To Israel for an everlasting covenant,

Akisema, Nitakupa wewe nchi ya Kanaani, Iwe urithi wenu mliopimiwa; 1 Mambo ya Nyakati 16:18

Saying, To you will I give the land of Canaan, The lot of your inheritance;

Mlipokuwa watu wawezao kuhesabiwa; Naam, watu wachache na wageni ndani yake. 1 Mambo ya Nyakati 16:19

When you were but a few men in number, Yes, very few, and foreigners in it;

Wakatanga-tanga toka taifa hata taifa, Toka ufalme mmoja hata kwa watu wengine. 1 Mambo ya Nyakati 16:20

They went about from nation to nation, From one kingdom to another people.

Hakumwacha mtu awaonee; Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao; 1 Mambo ya Nyakati 16:21

He allowed no man to do them wrong; Yes, he reproved kings for their sakes,

Akisema, Msiwaguse masihi wangu, Wala msiwadhuru nabii zangu. 1 Mambo ya Nyakati 16:22

[Saying], Don't touch my anointed ones, Do my prophets no harm.

Mwimbieni Bwana, nchi yote; Tangazeni wokovu wake siku kwa siku. 1 Mambo ya Nyakati 16:23

Sing to Yahweh, all the earth; Show forth his salvation from day to day.

Wahubirini mataifa habari za utukufu wake, Na watu wote habari za maajabu yake. 1 Mambo ya Nyakati 16:24

Declare his glory among the nations, His marvelous works among all the peoples.

Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kusifiwa sana; Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote. 1 Mambo ya Nyakati 16:25

For great is Yahweh, and greatly to be praised: He also is to be feared above all gods.

Maana miungu yote ya watu si kitu; Lakini Bwana ndiye aliyezifanya mbingu. 1 Mambo ya Nyakati 16:26

For all the gods of the peoples are idols: But Yahweh made the heavens.

Heshima na adhama ziko mbele zake; Nguvu na furaha zipo mahali pake. 1 Mambo ya Nyakati 16:27

Honor and majesty are before him: Strength and gladness are in his place.

Mpeni Bwana, enyi jamaa za watu, Mpeni Bwana utukufu na nguvu. 1 Mambo ya Nyakati 16:28

Ascribe to Yahweh, you relatives of the peoples, Ascribe to Yahweh glory and strength;

Mpeni Bwana utukufu wa jina lake; Leteni sadaka, mje mbele zake; Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu; 1 Mambo ya Nyakati 16:29

Ascribe to Yahweh the glory due to his name: Bring an offering, and come before him: Worship Yahweh in holy array.

Tetemekeni mbele zake, nchi yote. 1 Mambo ya Nyakati 16:30

Tremble before him, all the earth: The world also is established that it can't be moved.

Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie; Na waseme katika mataifa, Bwana ametamalaki; 1 Mambo ya Nyakati 16:31

Let the heavens be glad, and let the earth rejoice; Let them say among the nations, Yahweh reigns.

Bahari na ivume na vyote viijazavyo; Mashamba na yashangilie na vyote vilivyomo; 1 Mambo ya Nyakati 16:32

Let the sea roar, and the fullness of it; Let the field exult, and all that is therein;

Ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha, 1 Mambo ya Nyakati 16:33

Then shall the trees of the wood sing for joy before Yahweh; For he comes to judge the earth.

Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 1 Mambo ya Nyakati 16:34

Oh give thanks to Yahweh; for he is good; For his loving kindness endures forever.

Nanyi mkaseme, Ee Mungu wa wokovu wetu, utuokoe, Utukusanye kwa kututoa katika mataifa, Tulishukuru jina lako takatifu, Tuzifanyie shangwe sifa zako. 1 Mambo ya Nyakati 16:35

Say you, Save us, God of our salvation, Gather us together and deliver us from the nations, To give thanks to your holy name, To triumph in your praise.

Na ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, tangu milele hata milele. Na watu wote wakasema, Amina; wakamhimidi Bwana. 1 Mambo ya Nyakati 16:36

Blessed be Yahweh, the God of Israel, From everlasting even to everlasting. All the people said, Amen, and praised Yahweh.

Basi akawaacha huko, mbele ya sanduku la agano la Bwana, Asafu na nduguze, ili watumike mbele ya sanduku daima, kila siku kama ilivyokuwa kazi yake. 1 Mambo ya Nyakati 16:37

So he left there, before the ark of the covenant of Yahweh, Asaph and his brothers, to minister before the ark continually, as every day's work required;

Naye Obed-edomu, pamoja na ndugu zao, sitini na wanane; Obed-edomu na mwana wa Yeduthuni, na Hosa, wawe mabawabu; 1 Mambo ya Nyakati 16:38

and Obed-edom with their brothers, sixty-eight; Obed-edom also the son of Jeduthun and Hosah to be doorkeepers;

na Sadoki kuhani, na nduguze makuhani, mbele ya maskani ya Bwana katika mahali pa juu palipokuwa huko Gibeoni, 1 Mambo ya Nyakati 16:39

and Zadok the priest, and his brothers the priests, before the tent of Yahweh in the high place that was at Gibeon,

ili kumtolea Bwana sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa daima asubuhi na jioni, naam, sawasawa na yote yaliyoandikwa katika torati ya Bwana, aliyowaamuru Israeli; 1 Mambo ya Nyakati 16:40

to offer burnt offerings to Yahweh on the altar of burnt offering continually morning and evening, even according to all that is written in the law of Yahweh, which he commanded to Israel;

na pamoja nao Hemani na Yeduthuni, na wale wengine waliochaguliwa, waliotajwa majina yao, ili kumshukuru Bwana, kwa kuwa fadhili zake ni za milele; 1 Mambo ya Nyakati 16:41

and with them Heman and Jeduthun, and the rest who were chosen, who were mentioned by name, to give thanks to Yahweh, because his loving kindness endures forever;

na pamoja nao Hemani na Yeduthuni wenye baragumu na matoazi, kwa hao watakaovumisha sauti, na vinanda kwa ajili ya hizo nyimbo za Mungu; na hao wana wa Yeduthuni wawepo mlangoni. 1 Mambo ya Nyakati 16:42

and with them Heman and Jeduthun [with] trumpets and cymbals for those that should sound aloud, and [with] instruments for the songs of God; and the sons of Jeduthun to be at the gate.

Kisha watu wote wakaenda zao kila mtu nyumbani kwake; naye Daudi akarudi ili awabariki watu wa nyumbani mwake. 1 Mambo ya Nyakati 16:43

All the people departed every man to his house: and David returned to bless his house.