1 Mambo ya Nyakati 18 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Mambo ya Nyakati 18 (Swahili) 1st Chronicles 18 (English)

Ikawa baadaye, Daudi akawapiga Wafilisti, akawashinda, akautwaa Gathi na vijiji vyake mikononi mwa Wafilisti. 1 Mambo ya Nyakati 18:1

After this it happened, that David struck the Philistines, and subdued them, and took Gath and its towns out of the hand of the Philistines.

Akapiga Moabu; na hao Wamoabi wakawa watumwa wa Daudi wakaleta zawadi. 1 Mambo ya Nyakati 18:2

He struck Moab; and the Moabites became servants to David, and brought tribute.

Tena Daudi akampiga Hadadezeri, mfalme wa Soba, mpaka Hamathi, alipokwenda kujisimamishia mamlaka yake kwenye mto wa Frati. 1 Mambo ya Nyakati 18:3

David struck Hadarezer king of Zobah to Hamath, as he went to establish his dominion by the river Euphrates.

Daudi akampokonya magari elfu, na wapanda farasi saba elfu, na askari waendao kwa miguu ishirini elfu; Daudi akawakata mshipa farasi wote wa magari, ila wa magari mia akawaweka. 1 Mambo ya Nyakati 18:4

David took from him one thousand chariots, and seven thousand horsemen, and twenty thousand footmen; and David hamstrung all the chariot horses, but reserved of them for one hundred chariots.

Na Washami wa Dameski walipokuja wamsaidie Hadadezeri, mfalme wa Soba, Daudi akapiga katika hao Washami watu ishirini na mbili elfu. 1 Mambo ya Nyakati 18:5

When the Syrians of Damascus came to help Hadarezer king of Zobah, David struck of the Syrians twenty-two thousand men.

Ndipo Daudi akaweka ngome katika Shamu ya Dameski; nao Washami wakawa watumwa wa Daudi, wakaleta zawadi. Naye Bwana akampa Daudi kushinda kila alikokwenda. 1 Mambo ya Nyakati 18:6

Then David put [garrisons] in Syria of Damascus; and the Syrians became servants to David, and brought tribute. Yahweh gave victory to David wherever he went.

Tena Daudi akazitwaa ngao za dhahabu zilizovaliwa na watumishi wa Hadadezeri akazileta Yerusalemu. 1 Mambo ya Nyakati 18:7

David took the shields of gold that were on the servants of Hadarezer, and brought them to Jerusalem.

Tena toka Tibhathi, na toka Berothai, miji ya Hadadezeri, Daudi akatwaa shaba nyingi mno, aliyofanyizia Sulemani ile bahari ya shaba, na zile nguzo, na vile vyombo vya shaba. 1 Mambo ya Nyakati 18:8

From Tibhath and from Cun, cities of Hadarezer, David took very much brass, with which Solomon made the brazen sea, and the pillars, and the vessels of brass.

Hata aliposikia Tou, mfalme wa Hamathi, ya kuwa Daudi amewapiga jeshi lote la Hadadezeri, mfalme wa Soba, 1 Mambo ya Nyakati 18:9

When Tou king of Hamath heard that David had struck all the host of Hadarezer king of Zobah,

akampeleka mwanawe Hadoramu kwa mfalme Daudi, ili kumsalimia, na kumbarikia, kwa sababu alikuwa amepigana na Hadadezeri, na kumpiga; kwa maana Hadadezeri alikuwa amepigana vita juu ya Tou; naye akaleta vyombo vya dhahabu, na fedha, na shaba, vya namna zote. 1 Mambo ya Nyakati 18:10

he sent Hadoram his son to king David, to Greet him, and to bless him, because he had fought against Hadarezer and struck him; (for Hadarezer had wars with Tou;) and [he had with him] all manner of vessels of gold and silver and brass.

Hivi pia mfalme Daudi akavifanya wakfu kwa Bwana, pamoja na hiyo fedha na dhahabu, aliyoteka nyara kwa mataifa yote; kwa Edomu, na kwa Moabu, na kwa wana wa Amoni, na kwa Wafilisti, na kwa Amaleki. 1 Mambo ya Nyakati 18:11

These also did king David dedicate to Yahweh, with the silver and the gold that he carried away from all the nations; from Edom, and from Moab, and from the children of Ammon, and from the Philistines, and from Amalek.

Tena Abishai, mwana wa Seruya, akawapiga wa Waedomi katika Bonde la Chumvi watu kumi na nane elfu. 1 Mambo ya Nyakati 18:12

Moreover Abishai the son of Zeruiah struck of the Edomites in the Valley of Salt eighteen thousand.

Akaweka ngome katika Edomu; na Waedomi wote wakawa watumwa wa Daudi. Naye Bwana akampa Daudi kushinda, kila alikokwenda. 1 Mambo ya Nyakati 18:13

He put garrisons in Edom; and all the Edomites became servants to David. Yahweh gave victory to David wherever he went.

Basi Daudi akatawala juu ya Israeli wote; akawafanyia hukumu na haki watu wake wote. 1 Mambo ya Nyakati 18:14

David reigned over all Israel; and he executed justice and righteousness to all his people.

Na Yoabu mwana wa Seruya akawa juu ya jeshi; na Yehoshafati mwana wa Ahiludi mwenye kuandika tarehe. 1 Mambo ya Nyakati 18:15

Joab the son of Zeruiah was over the host; and Jehoshaphat the son of Ahilud was recorder;

Na Sadoki mwana wa Ahitubu, na Ahimeleki mwana wa Abiathari, walikuwa makuhani; na Shausha mwandishi; 1 Mambo ya Nyakati 18:16

and Zadok the son of Ahitub, and Abimelech the son of Abiathar, were priests; and Shavsha was scribe;

na Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa juu ya Wakerethi na Wapelethi; na wana wa Daudi walikuwa wakuu kumzunguka mfalme. 1 Mambo ya Nyakati 18:17

and Benaiah the son of Jehoiada was over the Cherethites and the Pelethites; and the sons of David were chief about the king.