1 Wafalme 17 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wafalme 17 (Swahili) 1st Kings 17 (English)

Basi Eliya Mtishbi, wa wageni wa Gileadi, akamwambia Ahabu, Kama Bwana, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye ninasimama mbele zake, hakutakuwa na umande wala mvua miaka hii, ila kwa neno langu. 1 Wafalme 17:1

Elijah the Tishbite, who was of the foreigners of Gilead, said to Ahab, As Yahweh, the God of Israel, lives, before whom I stand, there shall not be dew nor rain these years, but according to my word.

Neno la Bwana likamjia, kusema, 1 Wafalme 17:2

The word of Yahweh came to him, saying,

Ondoka hapa, geuka, uende upande wa mashariki, ujifiche karibu na kijito cha Kerithi kinachokabili Yordani. 1 Wafalme 17:3

Get you hence, and turn you eastward, and hide yourself by the brook Cherith, that is before the Jordan.

Itakuwa utakunywa maji ya kile kijito; nami nimewaamuru kunguru wakulishe huko. 1 Wafalme 17:4

It shall be, that you shall drink of the brook; and I have commanded the ravens to feed you there.

Basi akaenda akafanya kama alivyosema Bwana; kwa kuwa akaenda akakaa karibu na kijito cha Kerithi, kinachokabili Yordani. 1 Wafalme 17:5

So he went and did according to the word of Yahweh; for he went and lived by the brook Cherith, that is before the Jordan.

Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, akanywa maji ya kile kijito. 1 Wafalme 17:6

The ravens brought him bread and flesh in the morning, and bread and flesh in the evening; and he drank of the brook.

Ikawa, baada ya siku kupita, kile kijito kikakatika, kwa sababu mvua haikunyesha katika nchi. 1 Wafalme 17:7

It happened after a while, that the brook dried up, because there was no rain in the land.

Neno la Bwana likamjia, kusema, 1 Wafalme 17:8

The word of Yahweh came to him, saying,

Ondoka, uende Sarepta, ulio mji wa Sidoni, ukae huko. Tazama, nimemwagiza mwanamke mjane wa huko akulishe. 1 Wafalme 17:9

Arise, get you to Zarephath, which belongs to Sidon, and dwell there: behold, I have commanded a widow there to sustain you.

Basi, akaondoka, akaenda Sarepta; hata alipofika langoni pa mji, kumbe! Mwanamke mjane alikuwako akiokota kuni; akamwita, akamwambia, Niletee, nakuomba, maji kidogo chomboni nipate kunywa. 1 Wafalme 17:10

So he arose and went to Zarephath; and when he came to the gate of the city, behold, a widow was there gathering sticks: and he called to her, and said, Please get me a little water in a vessel, that I may drink.

Alipokuwa akienda kuleta, akamwita akasema, Niletee, nakuomba, kipande cha mkate mkononi mwako. 1 Wafalme 17:11

As she was going to get it, he called to her, and said, Please bring me a morsel of bread in your hand.

Naye akasema, Kama Bwana, Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tuule tukafe. 1 Wafalme 17:12

She said, As Yahweh your God lives, I don't have a cake, but a handful of meal in the jar, and a little oil in the jar: and, behold, I am gathering two sticks, that I may go in and bake it for me and my son, that we may eat it, and die.

Eliya akamwambia, Usiogope; enenda ukafanye kama ulivyosema; lakini unifanyie kwanza mkate mdogo ukaniletee; kisha ujifanyie nafsi yako na mwanao. 1 Wafalme 17:13

Elijah said to her, Don't be afraid; go and do as you have said; but make me of it a little cake first, and bring it forth to me, and afterward make for you and for your son.

Kwa kuwa Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Lile pipa la unga halitapunguka, wala ile chupa ya mafuta haitaisha, hata siku ile Bwana atakapoleta mvua juu ya nchi. 1 Wafalme 17:14

For thus says Yahweh, the God of Israel, The jar of meal shall not empty, neither shall the jar of oil fail, until the day that Yahweh sends rain on the earth.

Basi akaenda, akafanya kama alivyosema Eliya; na yeye mwenyewe, na Eliya, na nyumba yake, wakala siku nyingi. 1 Wafalme 17:15

She went and did according to the saying of Elijah: and she, and he, and her house, ate [many] days.

Lile pipa la unga halikupunguka, wala ile chupa ya mafuta haikuisha, sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa kinywa cha Eliya. 1 Wafalme 17:16

The jar of meal didn't empty, neither did the jar of oil fail, according to the word of Yahweh, which he spoke by Elijah.

Ikawa, baada ya hayo, mwana wake yule mwanamke, bibi wa nyumba ile, akaugua; ugonjwa wake ukazidi hata akawa hana pumzi tena. 1 Wafalme 17:17

It happened after these things, that the son of the woman, the mistress of the house, fell sick; and his sickness was so sore, that there was no breath left in him.

Akamwambia Eliya, Nina nini nawe, Ee mtu wa Mungu? Je! Umenijia ili dhambi yangu ikumbukwe, ukamwue mwanangu? 1 Wafalme 17:18

She said to Elijah, What have I to do with you, you man of God? You have come to me to bring my sin to memory, and to kill my son!

Akamwambia, Nipe mwanao. Akamtoa katika kifua chake, akamchukua juu chumbani mle alimokaa mwenyewe, akamlaza kitandani pake. 1 Wafalme 17:19

He said to her, Give me your son. He took him out of her bosom, and carried him up into the chamber, where he abode, and laid him on his own bed.

Akamwomba Bwana, akanena, Ee Bwana, Mungu wangu, je! Umemtenda mabaya mjane huyu ninayekaa kwake hata kumfisha mwanawe. 1 Wafalme 17:20

He cried to Yahweh, and said, Yahweh my God, have you also brought evil on the widow with whom I sojourn, by killing her son?

Akajinyosha juu ya mtoto mara tatu, akamwomba Bwana, akanena, Ee Bwana, Mungu wangu, nakusihi, roho ya mtoto huyu imrudie ndani yake tena. 1 Wafalme 17:21

He stretched himself on the child three times, and cried to Yahweh, and said, Yahweh my God, please let this child's soul come into him again.

Bwana akaisikia sauti ya Eliya; na roho ya mtoto ikamrudia, akafufuka. 1 Wafalme 17:22

Yahweh listened to the voice of Elijah; and the soul of the child came into him again, and he revived.

Eliya akamtwaa mtoto, akamchukua toka orofani mpaka chini ya nyumba ile, akampa mama yake. Eliya akanena, Tazama, mwanao yu hai. 1 Wafalme 17:23

Elijah took the child, and brought him down out of the chamber into the house, and delivered him to his mother; and Elijah said, Behold, your son lives.

Mwanamke akamwambia Eliya, Sasa najua ya kuwa wewe ndiwe mtu wa Mungu, na ya kuwa neno la Bwana kinywani mwako ni kweli. 1 Wafalme 17:24

The woman said to Elijah, Now I know that you are a man of God, and that the word of Yahweh in your mouth is truth.