1 Wafalme 20 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wafalme 20 (Swahili) 1st Kings 20 (English)

Basi, Ben-hadadi mfalme wa Shamu akakusanya jeshi lake lote; nao walikuwapo wafalme thelathini na wawili pamoja naye, na farasi, na magari: akakwea akauhusuru Samaria, akaupiga vita. 1 Wafalme 20:1

Ben Hadad the king of Syria gathered all his host together; and there were thirty-two kings with him, and horses and chariots: and he went up and besieged Samaria, and fought against it.

Akatuma wajumbe kwa Ahabu mfalme wa Israeli, mjini, akamwambia, Ndivyo asemavyo Ben-hadadi. 1 Wafalme 20:2

He sent messengers to Ahab king of Israel, into the city, and said to him, Thus says Ben Hadad,

Fedha yako na dhahabu yako ni zangu mimi; na wakezo na wanao, walio wema, ni wangu. 1 Wafalme 20:3

Your silver and your gold is mine; your wives also and your children, even the best, are mine.

Mfalme wa Israeli akajibu, akasema, Ni kama ulivyosema, bwana wangu, mfalme; mimi ni wako, na vyote nilivyo navyo. 1 Wafalme 20:4

The king of Israel answered, It is according to your saying, my lord, O king; I am yours, and all that I have.

Wajumbe wakarudi tena, wakasema, Ndivyo asemavyo Ben-hadadi, Hakika nimetuma kwako kusema, Fedha yako, na dhahabu yako, na wake zako, na wanao, utanitolea mimi; 1 Wafalme 20:5

The messengers came again, and said, Thus speaks Ben Hadad, saying, I sent indeed to you, saying, You shall deliver me your silver, and your gold, and your wives, and your children;

lakini kesho kama wakati huu nitatuma kwako watumwa wangu, ili watazame-tazame nyumba yako na nyumba za watumwa wako; na itakuwa kila kipendezacho machoni pako watakitia mikononi mwao,na kukichukua. 1 Wafalme 20:6

but I will send my servants to you tomorrow about this time, and they shall search your house, and the houses of your servants; and it shall be, that whatever is pleasant in your eyes, they shall put it in their hand, and take it away.

Ndipo mfalme wa Israeli, akawaita wazee wote wa nchi, akasema, Angalieni, nawaomba, mwone, kwamba huyu ataka madhara; maana ametuma kwangu kutaka wake zangu na watoto wangu; na fedha yangu na dhahabu yangu, sikumkatalia. 1 Wafalme 20:7

Then the king of Israel called all the elders of the land, and said, Please notice how this man seeks mischief: for he sent to me for my wives, and for my children, and for my silver, and for my gold; and I didn't deny him.

Wakamwambia wazee wote na watu wote, Usisikie, wala usikubali. 1 Wafalme 20:8

All the elders and all the people said to him, Don't you listen, neither consent.

Kwa hiyo akawaambia wale wajumbe wa Ben-hadadi, Mwambieni bwana wangu mfalme, Kila uliyotuma kumtakia mtumwa wako kwanza, nitafanya, ila neno hili siwezi kulifanya. Basi wajumbe wakaenda zao, wakamrudishia maneno hayo. 1 Wafalme 20:9

Therefore he said to the messengers of Ben Hadad, Tell my lord the king, All that you did send for to your servant at the first I will do; but this thing I may not do. The messengers departed, and brought him word again.

Ndipo Ben-hadadi akatuma kwake, akasema, Miungu wanifanyie hivi na kuzidi, yakiwa mavumbi ya Samaria yatatosha makonzi ya watu wote walio miguuni pangu. 1 Wafalme 20:10

Ben Hadad sent to him, and said, The gods do so to me, and more also, if the dust of Samaria shall suffice for handfuls for all the people who follow me.

Mfalme wa Israeli akajibu, akasema, Mwambieni, Avaaye asijisifu kama avuaye. 1 Wafalme 20:11

The king of Israel answered, Tell him, Don't let him who girds on [his armor] boast himself as he who puts it off.

Ikawa, Ben-hadadi alipolisikia neno hilo, naye alikuwa akinywa, yeye na wafalme, mabandani, aliwaambia watumwa wake, Jipangeni. Wakajipanga juu ya mji. 1 Wafalme 20:12

It happened, when [Ben Hadad] heard this message, as he was drinking, he and the kings, in the pavilions, that he said to his servants, Set [yourselves in array]. They set [themselves in array] against the city.

Na tazama, nabii akamjia Ahabu mfalme wa Israeli, akasema, Bwana asema hivi, Je! Umeona makutano haya yote walio wengi? Angalia, nitawatia leo mkononi mwako; nawe utajua ya kuwa ndimi Bwana. 1 Wafalme 20:13

Behold, a prophet came near to Ahab king of Israel, and said, Thus says Yahweh, Have you seen all this great multitude? behold, I will deliver it into your hand this day; and you shall know that I am Yahweh.

Ahabu akanena, Kwa nani? Akasema, Bwana asema hivi, Kwa vijana wa maliwali wa majimbo. Ndipo akanena, Ni nani atakayepanga vita? Naye akajibu, Ni wewe. 1 Wafalme 20:14

Ahab said, By whom? He said, Thus says Yahweh, By the young men of the princes of the provinces. Then he said, Who shall begin the battle? He answered, You.

Ndipo akawaandika vijana wa maliwali wa majimbo, nao walikuwa mia mbili thelathini na wawili; kisha baada ya hao akawaandika watu wote, wana wa Israeli wote, nao walikuwa elfu saba. 1 Wafalme 20:15

Then he mustered the young men of the princes of the provinces, and they were two hundred and thirty-two: and after them he mustered all the people, even all the children of Israel, being seven thousand.

Wakatoka wakati wa adhuhuri. Lakini Ben-hadadi alikuwa akinywa hata kulewa mabandani, yeye na wale wafalme thelathini na wawili waliomsaidia. 1 Wafalme 20:16

They went out at noon. But Ben Hadad was drinking himself drunk in the pavilions, he and the kings, the thirty-two kings who helped him.

Wakatoka wale vijana wa maliwali wa majimbo wakitangulia; na Ben-hadadi akatuma watu, nao wakamwambia, Wako watu wametoka katika Samaria. 1 Wafalme 20:17

The young men of the princes of the provinces went out first; and Ben Hadad sent out, and they told him, saying, There are men come out from Samaria.

Akasema, Kwamba wametoka kwa amani, wakamateni wa hai; au kwamba wametoka kwa vita, wakamateni wa hai. 1 Wafalme 20:18

He said, Whether they are come out for peace, take them alive, or whether they are come out for war, taken them alive.

Basi wakatoka mjini hao vijana wa maliwali wa majimbo, na jeshi nyuma yao. 1 Wafalme 20:19

So these went out of the city, the young men of the princes of the provinces, and the army which followed them.

Wakapiga kila mmoja mtu wake; Washami wakakimbia, na Israeli wakawafuatia; Ben-hadadi mfalme wa Shamu akaokoka amepanda farasi, pamoja na wapandao farasi. 1 Wafalme 20:20

They killed everyone his man; and the Syrians fled, and Israel pursued them: and Ben Hadad the king of Syria escaped on a horse with horsemen.

Mfalme wa Israeli akatoka, akawapiga farasi na magari, akawapiga Washami pigo kubwa. 1 Wafalme 20:21

The king of Israel went out, and struck the horses and chariots, and killed the Syrians with a great slaughter.

Naye yule nabii akamjia mfalme wa Israeli, akamwambia, Enenda, kusanya nguvu zako, ujue, na kuangalia ufanyavyo; kwa maana mwakani mfalme wa Shamu atakuja juu yako. 1 Wafalme 20:22

The prophet came near to the king of Israel, and said to him, Go, strengthen yourself, and mark, and see what you do; for at the return of the year the king of Syria will come up against you.

Basi watumwa wake mfalme wa Shamu wakamwambia, Mungu wao ni mungu wa milima; ndiyo sababu ya kutushinda sisi; lakini na tupigane nao katika nchi tambarare, na hakika tutawashinda wao. 1 Wafalme 20:23

The servants of the king of Syria said to him, Their god is a god of the hills; therefore they were stronger than we: but let us fight against them in the plain, and surely we shall be stronger than they.

Ufanye neno hili; uwaondoe hao wafalme, kila mtu atoke mahali pake, ukaweke majemadari mahali pao. 1 Wafalme 20:24

Do this thing: take the kings away, every man out of his place, and put captains in their room;

Kisha ujihesabie jeshi, kama jeshi lililokupotea, farasi kwa farasi na gari kwa gari; nasi tutapigana nao katika nchi tambarare, na bila shaka tutawashinda. Akaisikiliza sauti yao, akafanya kama hivyo. 1 Wafalme 20:25

and number you an army, like the army that you have lost, horse for horse, and chariot for chariot; and we will fight against them in the plain, and surely we shall be stronger than they. He listened to their voice, and did so.

Basi ikawa mwakani, Ben-hadadi akawahesabu Washami, akakwea mpaka Afeki ili apigane na Israeli. 1 Wafalme 20:26

It happened at the return of the year, that Ben Hadad mustered the Syrians, and went up to Aphek, to fight against Israel.

Wana wa Israeli nao wakahesabiwa, wakapewa vyakula, wakaenda kupigana nao; wakatua wana wa Israeli mbele yao kama vikundi viwili vya wana-mbuzi; bali Washami wakaijaza nchi. 1 Wafalme 20:27

The children of Israel were mustered, and were provisioned, and went against them: and the children of Israel encamped before them like two little flocks of kids; but the Syrians filled the country.

Akaja yule mtu wa Mungu, akamwambia mfalme wa Israeli, akasema, Bwana asema hivi, Kwa sababu Washami wamesema, Bwana ni Mungu wa milima wala si Mungu wa nchi tambarare; basi nitawatia makutano haya yote walio wengi mkononi mwako, nanyi mtajua ya kuwa ndimi Bwana. 1 Wafalme 20:28

A man of God came near and spoke to the king of Israel, and said, Thus says Yahweh, Because the Syrians have said, Yahweh is a god of the hills, but he is not a god of the valleys; therefore will I deliver all this great multitude into your hand, and you shall know that I am Yahweh.

Wakatua kuelekeana muda wa siku saba. Ikawa siku ya saba vikapangwa vita; wana wa Israeli wakawapiga miongoni mwa Washami siku moja watu mia elfu waendao kwa miguu. 1 Wafalme 20:29

They encamped one over against the other seven days. So it was, that in the seventh day the battle was joined; and the children of Israel killed of the Syrians one hundred thousand footmen in one day.

Lakini waliosalia wakakimbia mpaka Afeki, mjini; na ukuta ukaanguka juu ya watu ishirini na saba elfu waliosalia. Ben-hadadi naye akakimbia, akaingia mjini, katika chumba cha ndani. 1 Wafalme 20:30

But the rest fled to Aphek, into the city; and the wall fell on twenty-seven thousand men who were left. Ben Hadad fled, and came into the city, into an inner chamber.

Watumwa wake wakamwambia, Angalia sasa, tumesikia ya kuwa wafalme wa nyumba ya Israeli ni wafalme wenye rehema; tafadhali, tuvae magunia viunoni, na kamba vichwani, tumtokee mfalme wa Israeli; labda atakuokoa roho yako. 1 Wafalme 20:31

His servants said to him, See now, we have heard that the kings of the house of Israel are merciful kings: let us, we pray you, put sackcloth on our loins, and ropes on our heads, and go out to the king of Israel: peradventure he will save your life.

Basi wakajifungia magunia viunoni, na kamba vichwani, wakamjia mfalme wa Israeli, wakasema, Mtumwa wako Ben-hadadi asema Roho yangu, nakusihi, iishi. Akasema, Je! Yu hai bado? Ni ndugu yangu yeye. 1 Wafalme 20:32

So they girded sackcloth on their loins, and [put] ropes on their heads, and came to the king of Israel, and said, Your servant Ben Hadad says, please let me live. He said, Is he yet alive? he is my brother.

Wale watu wakaangalia sana, wakafanya haraka kulishika neno hilo kama ni nia yake, wakasema, Ndugu yako, Ben-hadadi. Akasema, Haya! Nendeni mkamlete. Ndipo Ben-hadadi akamtokea, naye akampandisha garini. 1 Wafalme 20:33

Now the men observed diligently, and hurried to catch whether it were his mind; and they said, Your brother Ben Hadad. Then he said, Go you, bring him. Then Ben Hadad came forth to him; and he caused him to come up into the chariot.

Na Ben-hadadi akamwambia, Miji ile baba yangu aliyomnyang'anya baba yako nitairudisha; nawe utajifanyia njia huko Dameski, kama baba yangu aliyoifanya huko Samaria. Ahabu akasema, Nami nitakuacha kwa mapatano haya. Akafanya mapatano naye, akamwacha. 1 Wafalme 20:34

[Ben Hadad] said to him, The cities which my father took from your father I will restore; and you shall make streets for you in Damascus, as my father made in Samaria. I, [said Ahab], will let you go with this covenant. So he made a covenant with him, and let him go.

Basi, mtu mmoja wa wana wa manabii akamwambia mwenzake kwa neno la Bwana, Nipige, nakusihi. Akakataa yule kumpiga. 1 Wafalme 20:35

A certain man of the sons of the prophets said to his fellow by the word of Yahweh, Please strike me. The man refused to strike him.

Akamwambia, Kwa sababu hukuisikiliza sauti ya Bwana, angalia, mara ukitoka kwangu simba atakuua. Na mara alipotoka kwake, simba alimwona, akamwua. 1 Wafalme 20:36

Then said he to him, Because you have not obeyed the voice of Yahweh, behold, as soon as you are departed from me, a lion shall kill you. As soon as he was departed from him, a lion found him, and killed him.

Ndipo akaona mtu mwingine, akasema, Nipige, nakusihi. Yule mtu akampiga, hata kumpiga na kumtia jeraha. 1 Wafalme 20:37

Then he found another man, and said, Please strike me. The man struck him, smiting and wounding him.

Basi yule nabii akaenda akamngoja mfalme njiani, amejibadilisha kwa kilemba juu ya macho yake. 1 Wafalme 20:38

So the prophet departed, and waited for the king by the way, and disguised himself with his headband over his eyes.

Ikawa mfalme alipopita, alimwita mfalme; akasema, Mtumwa wako aliingia katikati ya pigano; na tazama, mtu mmoja akanigeukia akaniletea mtu, akaniambia, Umlinde mtu huyu; akipotea kwa njia yo yote, roho yako itakuwa mahali pa roho yake, au utatoa talanta ya fedha. 1 Wafalme 20:39

As the king passed by, he cried to the king; and he said, Your servant went out into the midst of the battle; and, behold, a man turned aside, and brought a man to me, and said, Keep this man: if by any means he be missing, then shall your life be for his life, or else you shall pay a talent of silver.

Ikawa mtumishi wako alipokuwa akitenda haya na haya, yule akaenda zake. Mfalme wa Israeli akamwambia, Ndivyo itakavyokuwa hukumu yako; umejihukumu mwenyewe. 1 Wafalme 20:40

As your servant was busy here and there, he was gone. The king of Israel said to him, So shall your judgment be; yourself have decided it.

Akafanya haraka akakiondoa kilemba machoni mwake, mfalme wa Israeli akamtambua kuwa ni mmoja wao manabii. 1 Wafalme 20:41

He hurried, and took the headband away from his eyes; and the king of Israel discerned him that he was of the prophets.

Akamwambia, Bwana asema hivi, Kwa sababu umemwachilia atoke mkononi mwako mtu niliyemweka ili aangamizwe kabisa, roho yako itakuwa mahali pa roho yake, na watu wako mahali pa watu wake. 1 Wafalme 20:42

He said to him, Thus says Yahweh, Because you have let go out of your hand the man whom I had devoted to destruction, therefore your life shall go for his life, and your people for his people.

Mfalme wa Israeli akaenda nyumbani kwake na moyo mzito, mwenye hasira, akaja Samaria.

1 Wafalme 20:43

The king of Israel went to his house sullen and angry, and came to Samaria.