2 Wakorintho 4 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wakorintho 4 (Swahili) 2nd Corinthians 4 (English)

Kwa sababu hiyo, kwa kuwa tuna huduma hii, kwa jinsi tulivyopata rehema, hatulegei; 2 Wakorintho 4:1

Therefore seeing we have this ministry, even as we obtained mercy, we don't faint.

lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la Mungu na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za Mungu. 2 Wakorintho 4:2

But we have renounced the hidden things of shame, not walking in craftiness, nor handling the word of God deceitfully; but by the manifestation of the truth commending ourselves to every man's conscience in the sight of God.

Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; 2 Wakorintho 4:3

Even if our Gospel is veiled, it is veiled in those who perish;

ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu. 2 Wakorintho 4:4

in whom the god of this world has blinded the minds of the unbelieving, that the light of the Gospel of the glory of Christ, who is the image of God, should not dawn on them.

Kwa maana hatujihubiri wenyewe, bali Kristo Yesu ya kuwa ni Bwana; na sisi wenyewe kuwa tu watumishi wenu kwa ajili ya Yesu. 2 Wakorintho 4:5

For we don't preach ourselves, but Christ Jesus as Lord, and ourselves as your servants for Jesus' sake;

Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itang'aa toka gizani, ndiye aliyeng'aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo. 2 Wakorintho 4:6

seeing it is God who said, "Light will shine out of darkness," who has shone in our hearts, to give the light of the knowledge of the glory of God in the face of Jesus Christ.

Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, ili adhama kuu ya uwezo iwe ya Mungu, wala si kutoka kwetu. 2 Wakorintho 4:7

But we have this treasure in clay vessels, that the exceeding greatness of the power may be of God, and not from ourselves.

Pande zote twadhikika, bali hatusongwi; twaona shaka, bali hatukati tamaa; 2 Wakorintho 4:8

We are pressed on every side, yet not crushed; perplexed, yet not to despair;

twaudhiwa, bali hatuachwi; twatupwa chini, bali hatuangamizwi; 2 Wakorintho 4:9

pursued, yet not forsaken; struck down, yet not destroyed;

siku zote twachukua katika mwili kuuawa kwake Yesu, ili uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu. 2 Wakorintho 4:10

always carrying in the body the putting to death of the Lord Jesus, that the life of Jesus may also be revealed in our body.

Kwa maana sisi tulio hai, siku zote twatolewa tufe kwa ajili ya Yesu, ili uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu ipatikanayo na mauti. 2 Wakorintho 4:11

For we who live are always delivered to death for Jesus' sake, that the life also of Jesus may be revealed in our mortal flesh.

Basi hapo mauti hufanya kazi ndani yetu, bali uzima ndani yenu. 2 Wakorintho 4:12

So then death works in us, but life in you.

Lakini kwa kuwa tuna roho ile ile ya imani; kama ilivyoandikwa, Naliamini, na kwa sababu hiyo nalinena; sisi nasi twaamini, na kwa sababu hiyo twanena; 2 Wakorintho 4:13

But having the same spirit of faith, according to that which is written, "I believed, and therefore I spoke." We also believe, and therefore also we speak;

tukijua ya kwamba yeye aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua sisi nasi pamoja na Yesu, na kutuhudhurisha pamoja nanyi. 2 Wakorintho 4:14

knowing that he who raised the Lord Jesus will raise us also with Jesus, and will present us with you.

Kwa maana mambo yote ni kwa ajili yenu, ili neema hiyo ikiongezwa sana, kwa hao walio wengi shukrani izidishwe, na Mungu atukuzwe. 2 Wakorintho 4:15

For all things are for your sakes, that the grace, being multiplied through the many, may cause the thanksgiving to abound to the glory of God.

Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. 2 Wakorintho 4:16

Therefore we don't faint, but though our outward man is decaying, yet our inward man is renewed day by day.

Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana; 2 Wakorintho 4:17

For our light affliction, which is for the moment, works for us more and more exceedingly an eternal weight of glory;

tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele. 2 Wakorintho 4:18

while we don't look at the things which are seen, but at the things which are not seen. For the things which are seen are temporal, but the things which are not seen are eternal.