2 Wakorintho 6 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wakorintho 6 (Swahili) 2nd Corinthians 6 (English)

Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure. 2 Wakorintho 6:1

Working together, we entreat also that you not receive the grace of God in vain,

(Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa) 2 Wakorintho 6:2

for he says, "At an acceptable time I listened to you, In a day of salvation I helped you." Behold, now is the acceptable time. Behold, now is the day of salvation.

Tusiwe kwazo la namna yo yote katika jambo lo lote, ili utumishi wetu usilaumiwe; 2 Wakorintho 6:3

We give no occasion of stumbling in anything, that our service may not be blamed,

bali katika kila neno tujipatie sifa njema, kama watumishi wa Mungu; katika saburi nyingi, katika dhiki, katika misiba, katika shida; 2 Wakorintho 6:4

but in everything commending ourselves, as servants of God, in great endurance, in afflictions, in hardships, in distresses,

katika mapigo, katika vifungo, katika fitina, katika taabu, katika kukesha, katika kufunga; 2 Wakorintho 6:5

in beatings, in imprisonments, in riots, in labors, in watchings, in fastings;

katika kuwa safi, katika elimu, katika uvumilivu, katika utu wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo usio unafiki; 2 Wakorintho 6:6

in pureness, in knowledge, in patience, in kindness, in the Holy Spirit, in sincere love,

katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto; 2 Wakorintho 6:7

in the word of truth, in the power of God; by the armor of righteousness on the right hand and on the left,

kwa utukufu na aibu; kwa kunenwa vibaya na kunenwa vema; kama wadanganyao, bali tu watu wa kweli; 2 Wakorintho 6:8

by glory and dishonor, by evil report and good report; as deceivers, and yet true;

kama wasiojulikana, bali wajulikanao sana; kama wanaokufa, kumbe tu hai; kama wanaorudiwa, bali wasiouawa; 2 Wakorintho 6:9

as unknown, and yet well known; as dying, and behold, we live; as punished, and not killed;

kama wenye huzuni, bali siku zote tu wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali tu wenye vitu vyote. 2 Wakorintho 6:10

as sorrowful, yet always rejoicing; as poor, yet making many rich; as having nothing, and yet possessing all things.

Vinywa vyetu vimefumbuliwa kwenu, enyi Wakorintho; mioyo yetu imekunjuliwa. 2 Wakorintho 6:11

Our mouth is open to you, Corinthians. Our heart is enlarged.

Hamsongwi ndani yetu, bali mwasongwa katika mioyo yenu. 2 Wakorintho 6:12

You are not restricted by us, but you are restricted by your own affections.

Basi, ili mlipe kadiri ile mliyopewa (nasema nanyi kama na watoto), nanyi pia mkunjuliwe mioyo. 2 Wakorintho 6:13

Now in return, I speak as to my children, you also be open wide.

Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? 2 Wakorintho 6:14

Don't be unequally yoked with unbelievers, for what fellowship have righteousness and iniquity? Or what communion has light with darkness?

Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? 2 Wakorintho 6:15

What agreement has Christ with Belial? Or what portion has a believer with an unbeliever?

Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 2 Wakorintho 6:16

What agreement has a temple of God with idols? For you are a temple of the living God. Even as God said, "I will dwell in them, and walk in them; and I will be their God, and they will be my people."

Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. 2 Wakorintho 6:17

Therefore, "'Come out from among them, And be separate,' says the Lord, 'Touch no unclean thing. I will receive you.

Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, 2 Wakorintho 6:18

I will be to you a Father. You will be to me sons and daughters,' says the Lord Almighty."