2 Wakorintho 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wakorintho 1 (Swahili) 2nd Corinthians 1 (English)

Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu; kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, pamoja na watakatifu wote walioko katika nchi yote ya Akaya. 2 Wakorintho 1:1

Paul, an apostle of Christ Jesus through the will of God, and Timothy our brother, to the assembly of God which is at Corinth, with all the saints who are in the whole of Achaia:

Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo. 2 Wakorintho 1:2

Grace to you and peace from God our Father and the Lord Jesus Christ.

Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote; 2 Wakorintho 1:3

Blessed be the God and Father of our Lord Jesus Christ, the Father of mercies and God of all comfort;

atufarijiye katika dhiki zetu zote ili nasi tupate kuwafariji wale walio katika dhiki za namna zote, kwa faraja hizo, tunazofarijiwa na Mungu. 2 Wakorintho 1:4

who comforts us in all our affliction, that we may be able to comfort those who are in any affliction, through the comfort with which we ourselves are comforted by God.

Kwa kuwa kama vile mateso ya Kristo yanavyozidi kwetu, vivyo hivyo faraja yetu inazidi kwa njia ya Kristo. 2 Wakorintho 1:5

For as the sufferings of Christ abound to us, even so our comfort also abounds through Christ.

Lakini ikiwa sisi tu katika dhiki, ni kwa ajili ya faraja yenu na wokovu wenu; au ikiwa twafarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu; ambayo hutenda kazi yake kwa kustahimili mateso yale yale tuteswayo na sisi. 2 Wakorintho 1:6

But if we are afflicted, it is for your comfort and salvation. If we are comforted, it is for your comfort, which produces in you the patient enduring of the same sufferings which we also suffer.

Na tumaini letu kwa ajili yenu ni imara, tukijua ya kuwa kama vile mlivyo washiriki wa yale mateso, vivyo hivyo mmekuwa washiriki wa zile faraja. 2 Wakorintho 1:7

Our hope for you is steadfast, knowing that, since you are partakers of the sufferings, so also are you of the comfort.

Maana ndugu, hatupendi, msijue habari ya dhiki ile iliyotupata katika Asia, ya kwamba tulilemewa mno kuliko nguvu zetu, hata tukakata tamaa ya kuishi. 2 Wakorintho 1:8

For we don't desire to have you uninformed, brothers,{The word for "brothers" here and where context allows may also be correctly translated "brothers and sisters" or "siblings."} concerning our affliction which happened to us in Asia, that we were weighed down exceedingly, beyond our power, so much that we despaired even of life.

Naam, sisi wenyewe tulikuwa na hukumu ya mauti katika nafsi zetu ili tusijitumainie nafsi zetu, bali tumtumaini Mungu, awafufuaye wafu, 2 Wakorintho 1:9

Yes, we ourselves have had the sentence of death within ourselves, that we should not trust in ourselves, but in God who raises the dead,

aliyetuokoa sisi katika mauti kuu namna ile; tena atatuokoa; ambaye tumemtumaini kwamba atazidi kutuokoa; 2 Wakorintho 1:10

who delivered us out of so great a death, and does deliver; on whom we have set our hope that he will also still deliver us;

ninyi nanyi mkisaidiana nasi kwa ajili yetu katika kuomba, ili, kwa sababu ya ile karama tupewayo sisi kwa msaada wa watu wengi, watu wengi watoe shukrani kwa ajili yetu. 2 Wakorintho 1:11

you also helping together on our behalf by your supplication; that, for the gift bestowed on us by means of many, thanks may be given by many persons on your behalf.

Kwa maana kujisifu kwetu ni huku, ushuhuda wa dhamiri yetu, ya kwamba kwa utakatifu na weupe wa moyo utokao kwa Mungu; si kwa hekima ya mwili, bali kwa neema ya Mungu; tulienenda katika dunia, na hasa kwenu ninyi. 2 Wakorintho 1:12

For our boasting is this: the testimony of our conscience, that in holiness and sincerity of God, not in fleshly wisdom but in the grace of God we behaved ourselves in the world, and more abundantly toward you.

Maana hatuwaandikii ninyi neno, ila yale msomayo, au kuyakiri; nami nataraji ya kuwa mtayakiri hayo hata mwisho; 2 Wakorintho 1:13

For we write no other things to you, than what you read or even acknowledge, and I hope you will acknowledge to the end;

vile vile kama mlivyotukiri kwa sehemu, ya kwamba sisi tu sababu ya kujisifu kwenu, kama ninyi mlivyo kwetu sisi, katika siku ile ya Bwana wetu Yesu. 2 Wakorintho 1:14

as also you acknowledged us in part, that we are your boasting, even as you also are ours, in the day of our Lord Jesus.

Nami nikiwa na tumaini hilo nalitaka kufika kwenu hapo kwanza, ili mpate karama ya pili; 2 Wakorintho 1:15

In this confidence, I was determined to come first to you, that you might have a second benefit;

na kupita kwenu na kuendelea mpaka Makedonia; na tena toka Makedonia kurudi kwenu na kusafirishwa nanyi kwenda Uyahudi. 2 Wakorintho 1:16

and by you to pass into Macedonia, and again from Macedonia to come to you, and to be sent forward by you on my journey to Judea.

Basi, nilipokusudia hayo, je! Nalitumia kigeugeu? Au hayo niyakusudiayo, nayakusudia kwa jinsi ya mwili kwamba iwe hivi kwangu, kusema Ndiyo, ndiyo, na Siyo, siyo? 2 Wakorintho 1:17

When I therefore was thus determined, did I show fickleness? Or the things that I purpose, do I purpose according to the flesh, that with me there should be the "Yes, yes" and the "No, no?"

Lakini kama Mungu alivyo mwaminifu, neno letu kwenu si Ndiyo na siyo. 2 Wakorintho 1:18

But as God is faithful, our word toward you was not "Yes and no."

Maana Mwana wa Mungu, Kristo Yesu, aliyehubiriwa katikati yenu na sisi, yaani, mimi na Silwano na Timotheo, hakuwa Ndiyo na siyo; bali katika yeye ni Ndiyo. 2 Wakorintho 1:19

For the Son of God, Jesus Christ, who was preached among you by us, by me, Silvanus, and Timothy, was not "Yes and no," but in him is "Yes."

Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni Amin; Mungu apate kutukuzwa kwa sisi. 2 Wakorintho 1:20

For however many are the promises of God, in him is the "Yes." Therefore also through him is the "Amen," to the glory of God through us.

Basi Yeye atufanyaye imara pamoja nanyi katika Kristo, na kututia mafuta, ni Mungu, 2 Wakorintho 1:21

Now he who establishes us with you in Christ, and anointed us, is God;

naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu. 2 Wakorintho 1:22

who also sealed us, and gave us the down payment of the Spirit in our hearts.

Lakini mimi namwita Mungu awe shahidi juu ya roho yangu, ya kwamba, kwa kuwahurumia sijafika Korintho. 2 Wakorintho 1:23

But I call God for a witness to my soul, that I didn't come to Corinth to spare you.

Si kwamba tunatawala imani yenu; bali tu wasaidizi wa furaha yenu; maana kwa imani yenu mnasimama. 2 Wakorintho 1:24

Not that we have lordship over your faith, but are fellow workers with you for your joy. For you stand firm in faith.