Isaya 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 2 (Swahili) Isaiah 2 (English)

Hili ni neno aliloliona Isaya mwana wa Amozi katika habari za Yuda na Yerusalemu. Isaya 2:1

This is what Isaiah the son of Amoz saw concerning Judah and Jerusalem.

Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi. Isaya 2:2

It shall happen in the latter days, that the mountain of Yahweh's house shall be established on the top of the mountains, And shall be raised above the hills; And all nations shall flow to it.

Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana katika Yerusalemu. Isaya 2:3

Many peoples shall go and say, "Come, let's go up to the mountain of Yahweh, To the house of the God of Jacob; And he will teach us of his ways, And we will walk in his paths. For out of Zion the law shall go forth, And the word of Yahweh from Jerusalem.

Naye atafanya hukumu katika mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe. Isaya 2:4

He will judge between the nations, And will decide concerning many peoples; And they shall beat their swords into plowshares, And their spears into pruning-hooks. Nation shall not lift up sword against nation, Neither shall they learn war any more.

Enyi wa nyumba ya Israeli, njoni, twende katika nuru ya Bwana. Isaya 2:5

House of Jacob, come, and let us walk in the light of Yahweh.

Maana wewe umewaacha watu wako, nyumba ya Israeli, kwa sababu wamejaa kawaida za mashariki, nao ni wapiga ramli kama Wafilisti, na wanapana mikono na wana wa wageni. Isaya 2:6

For you have forsaken your people, the house of Jacob, Because they are filled from the east, With those who practice divination like the Philistines, And they clasp hands with the children of foreigners.

Tena nchi yao imejaa fedha na dhahabu, wala hapana mwisho wa hazina zao; tena nchi yao imejaa farasi, wala hapana mwisho wa magari yao. Isaya 2:7

Their land is full of silver and gold, Neither is there any end of their treasures. Their land also is full of horses, Neither is there any end of their chariots.

Tena nchi yao imejaa sanamu; huabudu kazi ya mikono yao, vitu vilivyofanywa kwa vidole vyao wenyewe. Isaya 2:8

Their land also is full of idols. They worship the work of their own hands, That which their own fingers have made.

Mtu mnyonge huinama, na mtu mkubwa hujidhili; kwa hiyo usiwasamehe. Isaya 2:9

Man is brought low, And mankind is humbled; Therefore don't forgive them.

Ingia ndani ya jabali; ukajifiche mavumbini mbele za utisho wa Bwana, mbele za utukufu wa enzi yake. Isaya 2:10

Enter into the rock, And hide in the dust, From before the terror of Yahweh, And from the glory of his majesty.

Macho ya mwanadamu yaliyoinuka yatashushwa chini, na kiburi cha mwanadamu kitainamishwa, naye Bwana, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo. Isaya 2:11

The lofty looks of man will be brought low, The haughtiness of men will be bowed down, And Yahweh alone will be exalted in that day.

Kwa maana kutakuwa siku ya Bwana wa majeshi juu ya watu wote wenye kiburi na majivuno, na juu ya yote yaliyoinuka; nayo yatashushwa chini. Isaya 2:12

For there will be a day of Yahweh of Hosts for all that is proud and haughty, And for all that is lifted up; And it shall be brought low:

Na juu ya mierezi yote ya Lebanoni iliyo mirefu na kuinuka, na juu ya mialoni yote ya Bashani; Isaya 2:13

For all the cedars of Lebanon, that are high and lifted up, For all the oaks of Bashan,

na juu ya milima mirefu yote, na juu ya vilima vyote vilivyoinuka; Isaya 2:14

For all the high mountains, For all the hills that are lifted up,

na juu ya kila mnara mrefu, na juu ya kila ukuta ulio na boma; Isaya 2:15

For every lofty tower, For every fortified wall,

na juu ya merikebu zote za Tarshishi, na juu ya kila taswira ipendezayo. Isaya 2:16

For all the ships of Tarshish, And for all pleasant imagery.

Na majivuno ya mwanadamu yatainamishwa, na kiburi cha watu kitashushwa; naye Bwana, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo. Isaya 2:17

The loftiness of man shall be bowed down, And the haughtiness of men shall be brought low; And Yahweh alone shall be exalted in that day.

Nazo sanamu zitatoweka kabisa. Isaya 2:18

The idols shall utterly pass away.

Na watu wataingia ndani ya pango za majabali, na ndani ya mashimo ya nchi, mbele za utisho wa Bwana na utukufu wa enzi yake, atakapoondoka ili aitetemeshe mno dunia. Isaya 2:19

Men shall go into the caves of the rocks, And into the holes of the earth, From before the terror of Yahweh, And from the glory of his majesty, When he arises to shake the earth mightily.

Siku hiyo kila mtu atazitupilia mbali sanamu zake za fedha, na sanamu zake za dhahabu, walizojifanyia ili kuziabudu, kwa fuko na popo; Isaya 2:20

In that day, men shall cast away their idols of silver, And their idols of gold, Which have been made for themselves to worship, To the moles and to the bats;

ili aingie ndani ya pango za majabali, na ndani ya tundu za miamba iliyopasuka, mbele za utisho wa Bwana na utukufu wa enzi yake, atakapoondoka ili aitetemeshe mno dunia. Isaya 2:21

To go into the caverns of the rocks, And into the clefts of the ragged rocks, From before the terror of Yahweh, And from the glory of his majesty, When he arises to shake the earth mightily.

Mwacheni mwanadamu ambaye pumzi yake i katika mianzi ya pua yake; kwa maana hudhaniwaje kuwa ni kitu? Isaya 2:22

Stop trusting in man, whose breath is in his nostrils; For of what account is he?