Isaya 42 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 42 (Swahili) Isaiah 42 (English)

Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu. Isaya 42:1

Behold, my servant, whom I uphold; my chosen, in whom my soul delights: I have put my Spirit on him; he will bring forth justice to the Gentiles.

Hatalia, wala hatapaza sauti yake, wala kuifanya isikiwe katika njia kuu. Isaya 42:2

He will not cry, nor lift up his voice, nor cause it to be heard in the street.

Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi utokao moshi hatauzima; atatokeza hukumu kwa kweli. Isaya 42:3

A bruised reed will he not break, and a dimly burning wick will he not quench: he will bring forth justice in truth.

Hatazimia, wala hatakata tamaa, hata atakapoweka hukumu duniani; na visiwa vitaingojea sheria yake. Isaya 42:4

He will not fail nor be discouraged, until he have set justice in the earth; and the isles shall wait for his law.

Mungu Bwana anena, yeye aliyeziumba mbingu, na kuzitanda; yeye aliyeitandaza nchi na mazao yake; yeye awapaye pumzi watu walio juu yake; yeye awapaye roho wao waendao ndani yake. Isaya 42:5

Thus says God Yahweh, he who created the heavens, and stretched them forth; he who spread abroad the earth and that which comes out of it; he who gives breath to the people on it, and spirit to those who walk therein:

Mimi, Bwana, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa; Isaya 42:6

I, Yahweh, have called you in righteousness, and will hold your hand, and will keep you, and give you for a covenant of the people, for a light of the Gentiles;

kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa. Isaya 42:7

to open the blind eyes, to bring out the prisoners from the dungeon, and those who sit in darkness out of the prison-house.

Mimi ni Bwana; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu. Isaya 42:8

I am Yahweh, that is my name; and my glory will I not give to another, neither my praise to engraved images.

Tazama, mambo ya kwanza yamekuwa, nami nayahubiri mambo mapya; kabla hayajatokea nawapasheni habari zake. Isaya 42:9

Behold, the former things have happened, and new things do I declare. Before they spring forth I tell you of them.

Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Na sifa zake tokea mwisho wa dunia; Ninyi mshukao baharini, na vyote vilivyomo, Na visiwa, nao wakaao humo. Isaya 42:10

Sing to Yahweh a new song, and his praise from the end of the earth; you who go down to the sea, and all that is therein, the isles, and the inhabitants of it.

Jangwa na miji yake na ipaze sauti zao, Vijiji vinavyokaliwa na Kedari; Na waimbe wenyeji wa Sela, Wapige kelele toka vilele vya milima. Isaya 42:11

Let the wilderness and the cities of it lift up [their voice], the villages that Kedar does inhabit; let the inhabitants of Sela sing, let them shout from the top of the mountains.

Na wamtukuze Bwana, Na kutangaza sifa zake visiwani. Isaya 42:12

Let them give glory to Yahweh, and declare his praise in the islands.

Bwana atatokea kama shujaa; Ataamsha wivu kama mtu wa vita; Atalia, naam, atapiga kelele; Atawatenda adui zake mambo makuu. Isaya 42:13

Yahweh will go forth as a mighty man; he will stir up [his] zeal like a man of war: he will cry, yes, he will shout aloud; he will do mightily against his enemies.

Siku nyingi nimenyamaza kimya; nimenyamaza, nikajizuia; sasa nitapiga kelele kama mwanamke aliye katika kuzaa; nitaugua na kutweta pamoja. Isaya 42:14

I have long time held my peace; I have been still, and refrained myself: [now] will I cry out like a travailing woman; I will gasp and pant together.

Nitaharibu milima na vilima, nitavikausha vyote vimeavyo; nitaifanya mito ya maji kuwa visiwa, na kuyakausha maziwa ya maji. Isaya 42:15

I will lay waste mountains and hills, and dry up all their herbs; and I will make the rivers islands, and will dry up the pools.

Nitawaleta vipofu kwa njia wasiyoijua; katika mapito wasiyoyajua nitawaongoza; nitafanya giza kuwa nuru mbele yao; na mahali palipopotoka kuwa pamenyoka. Haya nitayatenda, wala sitawaacha. Isaya 42:16

I will bring the blind by a way that they don't know; in paths that they don't know will I lead them; I will make darkness light before them, and crooked places straight. These things will I do, and I will not forsake them.

Watarudishwa nyuma, wataaibishwa sana, hao wanaotumainia sanamu za mawe, na kuziambia sanamu za madini, Ninyi ndinyi miungu yetu. Isaya 42:17

They shall be turned back, they shall be utterly disappointed, who trust in engraved images, who tell molten images, You are our gods.

Sikilizeni, enyi viziwi; tazameni, enyi vipofu, mpate kuona. Isaya 42:18

Hear, you deaf; and look, you blind, that you may see.

Ni nani aliye kipofu, ila mtumishi wangu? Au aliye kiziwi, kama mjumbe wangu nimtumaye? Ni nani aliye kipofu, kama yeye aliye na amani? Naam, kipofu kama mtumishi wa Bwana? Isaya 42:19

Who is blind, but my servant? or deaf, as my messenger whom I send? Who is blind as he who is at peace, and blind as Yahweh's servant?

Unaona mambo mengi, lakini huyatii moyoni; masikio yake ya wazi, lakini hasikii. Isaya 42:20

You see many things, but don't observe. His ears are open, but he doesn't hear.

Bwana akapendezwa, kwa ajili ya haki yake, kuitukuza sheria, na kuiadhimisha. Isaya 42:21

It pleased Yahweh, for his righteousness' sake, to magnify the law, and make it honorable.

Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha. Isaya 42:22

But this is a people robbed and plundered; they are all of them snared in holes, and they are hid in prison-houses: they are for a prey, and none delivers; for a spoil, and none says, Restore.

Ni nani miongoni mwenu atakayetega sikio lake kuyasikia hayo? Atakayesikiliza na kusikia kwa wakati ujao? Isaya 42:23

Who is there among you who will give ear to this? who will listen and hear for the time to come?

Ni nani aliyemtoa Yakobo awe mateka, aliyemtia Israeli katika mikono ya wanyang'anyi? Si yeye, Bwana? Yeye tuliyemkosa, ambaye hawakutaka kwenda katika njia zake, wala hawakuitii sheria yake. Isaya 42:24

Who gave Jacob for a spoil, and Israel to the robbers? Didn't Yahweh? he against whom we have sinned, and in whose ways they would not walk, neither were they obedient to his law.

Kwa sababu hiyo alimwaga ukali wa hasira yake juu yake, na nguvu za vita; ukawasha moto wa kumzunguka pande zote, wala hakujua; ukamteketeza, wala hakuyatia hayo moyoni mwake. Isaya 42:25

Therefore he poured on him the fierceness of his anger, and the strength of battle; and it set him on fire round about, yet he didn't know; and it burned him, yet he didn't lay it to heart.