Isaya 9 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 9 (Swahili) Isaiah 9 (English)

Lakini yeye aliyekuwa katika dhiki hatakosa changamko. Hapo kwanza aliiingiza nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali katika hali ya kudharauliwa, lakini zamani za mwisho ameifanya kuwa tukufu, karibu na njia ya bahari; ng'ambo ya Yordani, Galilaya ya mataifa. Isaya 9:1

But there shall be no gloom to her who was in anguish. In the former time he brought into contempt the land of Zebulun and the land of Naphtali; but in the latter time has he made it glorious, by the way of the sea, beyond the Jordan, Galilee of the nations.

Watu wale waliokwenda katika giza Wameona nuru kuu; Wale waliokaa katika nchi ya uvuli wa mauti, Nuru imewaangaza. Isaya 9:2

The people who walked in darkness have seen a great light: those who lived in the land of the shadow of death, on them has the light shined.

Umeliongeza taifa, umezidisha furaha yao; Wanafurahi mbele zako, Kama furaha ya wakati wa mavuno, Kama watu wafurahivyo wagawanyapo nyara. Isaya 9:3

You have multiplied the nation, you have increased their joy: they joy before you according to the joy in harvest, as men rejoice when they divide the spoil.

Kwa maana umeivunja nira ya mzigo wake, na gongo la bega lake, na fimbo yake yeye aliyemwonea, kama katika siku ya Midiani. Isaya 9:4

For the yoke of his burden, and the staff of his shoulder, the rod of his oppressor, you have broken as in the day of Midian.

Maana silaha zote za mtu mwenye silaha wakati wa mshindo, na mavazi yaliyofingirishwa katika damu, yatakuwa tayari kuteketezwa, yatakuwa kuni za kutiwa motoni. Isaya 9:5

For all the armor of the armed man in the tumult, and the garments rolled in blood, shall be for burning, for fuel of fire.

Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani. Isaya 9:6

For to us a child is born, to us a son is given; and the government shall be on his shoulder: and his name shall be called Wonderful, Counselor, Mighty God, Everlasting Father, Prince of Peace.

Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana wa majeshi ndio utakaotenda hayo. Isaya 9:7

Of the increase of his government and of peace there shall be no end, on the throne of David, and on his kingdom, to establish it, and to uphold it with justice and with righteousness from henceforth even forever. The zeal of Yahweh of Hosts will perform this.

Bwana alimpelekea Yakobo neno, likamfikilia Israeli. Isaya 9:8

The Lord sent a word into Jacob, and it has lighted on Israel.

Nao watu wote watajua, yaani, Efraimu na yeye akaaye Samaria, wasemao kwa kiburi na kwa kujisifu nafsi zao, Isaya 9:9

All the people shall know, [even] Ephraim and the inhabitant of Samaria, who say in pride and in arrogance of heart,

Matofali yameanguka, lakini sisi tutajenga kwa mawe yaliyochongwa; mikuyu imekatwa lakini sisi tutaweka mierezi badala yake. Isaya 9:10

The bricks are fallen, but we will build with hewn stone; the sycamores are cut down, but we will put cedars in their place.

Kwa sababu hiyo Bwana atawainua adui wa Resini juu yake, naye atawachochea adui zake; Isaya 9:11

Therefore Yahweh will set up on high against him the adversaries of Rezin, and will stir up his enemies,

Waashuri upande wa mbele, na Wafilisti upande wa nyuma, nao watamla Israeli kwa kinywa kilicho wazi. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa. Isaya 9:12

the Syrians before, and the Philistines behind; and they shall devour Israel with open mouth. For all this his anger is not turned away, but his hand is stretched out still.

Lakini watu hao hawakumwelekea yeye aliyewapiga, wala kumtafuta Bwana wa majeshi. Isaya 9:13

Yet the people have not turned to him who struck them, neither have they sought Yahweh of Hosts.

Kwa sababu hiyo Bwana atakata katika Israeli kichwa na mkia, kuti na nyasi, katika siku moja. Isaya 9:14

Therefore Yahweh will cut off from Israel head and tail, palm-branch and rush, in one day.

Mzee mwenye kuheshimiwa ndiye kichwa, na nabii afundishaye uongo ndiye mkia. Isaya 9:15

The elder and the honorable man, he is the head; and the prophet who teaches lies, he is the tail.

Kwa maana wawaongozao watu hawa ndio wawakoseshao, na hao walioongozwa na watu hao wameangamia. Isaya 9:16

For those who lead this people cause them to err; and those who are led of them are destroyed.

Kwa sababu hiyo Bwana hatawafurahia vijana wao, wala hatawahurumia yatima zao wala wajane wao; maana kila mtu ni mnajisi, dhalimu, na kila ulimi hunena upumbavu. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa. Isaya 9:17

Therefore the Lord will not rejoice over their young men, neither will he have compassion on their fatherless and widows; for everyone is profane and an evil-doer, and every mouth speaks folly. For all this his anger is not turned away, but his hand is stretched out still.

Kwa maana uovu huteketeza kama moto; huila mibigili na miiba, naam, huwaka katika vichaka vya mwitu, nao hupaa juu katika mawingu mazito ya moshi. Isaya 9:18

For wickedness burns as the fire; it devours the briers and thorns; yes, it kindles in the thickets of the forest, and they roll upward in a column of smoke.

Kwa sababu ya hasira ya Bwana wa majeshi nchi hii inateketea kabisa; watu hawa nao ni kama kuni zitiwazo motoni; hapana mtu amhurumiaye ndugu yake. Isaya 9:19

Through the wrath of Yahweh of hosts is the land burnt up; and the people are as the fuel of fire: no man spares his brother.

Hupokonya upande wa mkono wa kuume, nao huona njaa! Hula upande wa mkono wa kushoto, wala hawashibi! Watakula kila mtu nyama ya mkono wake mwenyewe. Isaya 9:20

One shall snatch on the right hand, and be hungry; and he shall eat on the left hand, and they shall not be satisfied: they shall eat every man the flesh of his own arm:

Manase anamla Efraimu, naye Efraimu anamla Manase; nao wawili pamoja watakuwa juu ya Yuda. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa. Isaya 9:21

Manasseh, Ephraim; and Ephraim, Manasseh; and they together shall be against Judah. For all this his anger is not turned away, but his hand is stretched out still.