Hesabu 20 Swahili & English

Listen/Download Audio
Hesabu 20 (Swahili) Numbers 20 (English)

Kisha wana wa Israeli, mkutano wote, wakaingia bara ya Sini, katika mwezi wa kwanza, watu wakakaa Kadeshi; Miriamu akafa huko, akazikwa huko. Hesabu 20:1

The children of Israel, even the whole congregation, came into the wilderness of Zin in the first month: and the people abode in Kadesh; and Miriam died there, and was buried there.

Na hapo hapakuwa na maji kwa ule mkutano; wakajikusanya juu ya Musa na juu ya Haruni. Hesabu 20:2

There was no water for the congregation: and they assembled themselves together against Moses and against Aaron.

Watu wakashindana na Musa, wakanena, wakisema, Ingalikuwa heri kama tungalikufa wakati ule ndugu zetu walipokufa mbele za Bwana! Hesabu 20:3

The people strove with Moses, and spoke, saying, Would that we had died when our brothers died before Yahweh!

Mbona mmewaleta kusanyiko la Bwana hata jangwa hili ili tufe huku, sisi na wanyama wetu? Hesabu 20:4

Why have you brought the assembly of Yahweh into this wilderness, that we should die there, we and our animals?

Na mbona mmetupandisha kutoka Misri ili kutuleta hata mahali hapa pabaya? Si mahali pa mbegu, wala tini, wala mizabibu, wala makomamanga; wala hapana maji ya kunywa. Hesabu 20:5

Why have you made us to come up out of Egypt, to bring us in to this evil place? it is no place of seed, or of figs, or of vines, or of pomegranates; neither is there any water to drink.

Musa na Haruni wakatoka pale palipokuwa mkutano, wakaenda hata mlangoni pa hema ya kukutania, wakaanguka kifudifudi; utukufu wa Bwana ukawatokea. Hesabu 20:6

Moses and Aaron went from the presence of the assembly to the door of the tent of meeting, and fell on their faces: and the glory of Yahweh appeared to them.

Bwana akasema na Musa, akinena, Hesabu 20:7

Yahweh spoke to Moses, saying,

Twaa ile fimbo, ukawakusanye mkutano, wewe na Haruni ndugu yako, ukauambie mwamba mbele ya macho yao utoe maji yake, nawe utawatokezea maji katika mwamba, na hivyo utawanywesha maji mkutano na wanyama wao. Hesabu 20:8

Take the rod, and assemble the congregation, you, and Aaron your brother, and speak you to the rock before their eyes, that it give forth its water; and you shall bring forth to them water out of the rock; so you shall give the congregation and their cattle drink.

Musa akaitwaa hiyo fimbo kutoka mbele za Bwana kama alivyomwamuru. Hesabu 20:9

Moses took the rod from before Yahweh, as he commanded him.

Musa na Haruni wakawakusanya kusanyiko mbele ya mwamba, akawaambia, Sikieni sasa, enyi waasi; je! Tuwatokezee maji katika mwamba huu? Hesabu 20:10

Moses and Aaron gathered the assembly together before the rock, and he said to them, Hear now, you rebels; shall we bring you forth water out of this rock?

Musa akainua mkono wake akaupiga ule mwamba kwa fimbo yake mara mbili; maji yakatoka mengi, mkutano wakanywa na wanyama wao pia. Hesabu 20:11

Moses lifted up his hand, and struck the rock with his rod twice: and water came forth abundantly, and the congregation drank, and their cattle.

Bwana akamwambia Musa na Haruni, Kwa kuwa hamkuniamini mimi, ili kunistahi mbele ya macho ya wana wa Israeli, basi kwa sababu hiyo, hamtawaingiza kusanyiko hili katika ile nchi niliyowapa. Hesabu 20:12

Yahweh said to Moses and Aaron, Because you didn't believe in me, to sanctify me in the eyes of the children of Israel, therefore you shall not bring this assembly into the land which I have given them.

Maji haya ni maji ya Meriba; kwa sababu wana wa Israeli waliteta na Bwana, naye alijionyesha kuwa mtakatifu kati yao. Hesabu 20:13

These are the waters of Meribah; because the children of Israel strove with Yahweh, and he was sanctified in them.

Kisha Musa akatuma wajumbe kutoka Kadeshi wamwendee mfalme wa Edomu, na kusema, Ndugu yako Israeli asema, Wewe wazijua taabu zote zilizotupata; Hesabu 20:14

Moses sent messengers from Kadesh to the king of Edom, Thus says your brother Israel, You know all the travail that has happened to us:

jinsi baba zetu walivyotelemkia Misri, nasi tulikaa Misri muda mwingi, nao Wamisri walitutenda vibaya sana, na baba zetu pia; Hesabu 20:15

how our fathers went down into Egypt, and we lived in Egypt a long time; and the Egyptians dealt ill with us, and our fathers:

tena tulipomlilia Bwana, akatusikiza sauti yetu, akamtuma malaika, na kututoa tutoke Misri; nasi tupo hapa Kadeshi, mji wa mpakani mwako mwa mwisho; Hesabu 20:16

and when we cried to Yahweh, he heard our voice, and sent an angel, and brought us forth out of Egypt: and, behold, we are in Kadesh, a city in the uttermost of your border.

tafadhali utupe ruhusa tupite katika nchi yako; hatutapita katika mashamba, wala katika mashamba ya mizabibu, wala hatutakunywa maji ya visimani; tutaifuata njia kuu ya mfalme, tusigeuke kwenda upande wa kuume, wala upande wa kushoto, hata tutakapopita mpaka wako. Hesabu 20:17

Please let us pass through your land: we will not pass through field or through vineyard, neither will we drink of the water of the wells: we will go along the king's highway; we will not turn aside to the right hand nor to the left, until we have passed your border.

Edomu akamwambia, Hutapita katika nchi yangu, nisije nikakutokea kupigana nawe kwa upanga. Hesabu 20:18

Edom said to him, You shall not pass through me, lest I come out with the sword against you.

Wana wa Israeli wakamwambia, Tutakwea kwa njia kuu; tena kama tukinywa maji yako, mimi na wanyama wangu wa mifugo, ndipo nitakulipa thamani yake; nipe ruhusa nipite kwa miguu yangu wala sitaki neno lingine lo lote. Hesabu 20:19

The children of Israel said to him, We will go up by the highway; and if we drink of your water, I and my cattle, then will I give the price of it: let me only, without [doing] anything [else], pass through on my feet.

Akamwambia, Hutapita katika nchi yangu. Kisha Edomu akamtokea ili kupigana naye, na watu wengi, na kwa mkono wa nguvu. Hesabu 20:20

He said, You shall not pass through. Edom came out against him with much people, and with a strong hand.

Basi hivyo Edomu akakataa kumpa Israeli ruhusa kupita katika mipaka yake; kwa hivyo Israeli akageuka na kumwacha. Hesabu 20:21

Thus Edom refused to give Israel passage through his border: why Israel turned away from him.

Kisha wakasafiri kutoka Kadeshi; wana wa Israeli, mkutano mzima, wakafikilia mlima wa Hori. Hesabu 20:22

They traveled from Kadesh: and the children of Israel, even the whole congregation, came to Mount Hor.

Bwana akanena na Musa na Haruni katika mlima wa Hori, karibu na mpaka wa nchi ya Edomu, akawaambia, Hesabu 20:23

Yahweh spoke to Moses and Aaron in Mount Hor, by the border of the land of Edom, saying,

Haruni atakusanywa awe pamoja na watu wake; kwa kuwa hataingia katika nchi niliyowapa wana wa Israeli, kwa sababu mliasi kinyume cha neno langu hapo penye maji ya Meriba. Hesabu 20:24

Aaron shall be gathered to his people; for he shall not enter into the land which I have given to the children of Israel, because you rebelled against my word at the waters of Meribah.

Uwatwae Haruni na mwanawe Eleazari uwalete juu ya mlima wa Hori; Hesabu 20:25

Take Aaron and Eleazar his son, and bring them up to Mount Hor;

umvue Haruni mavazi yake, ukamvike Eleazari mwanawe mavazi hayo; kisha Haruni atakusanywa kwa watu wake, naye atakufa huko. Hesabu 20:26

and strip Aaron of his garments, and put them on Eleazar his son: and Aaron shall be gathered [to his people], and shall die there.

Musa akafanya kama Bwana alivyomwagiza; wakakwea katika mlima wa Hori mbele ya macho ya mkutano wote. Hesabu 20:27

Moses did as Yahweh commanded: and they went up into Mount Hor in the sight of all the congregation.

Kisha Musa akamvua Haruni mavazi yake, akamvika mwanawe Eleazari mavazi hayo; Haruni akafa huko katika kilele cha mlima; Musa na Eleazari wakatelemka mlimani. Hesabu 20:28

Moses stripped Aaron of his garments, and put them on Eleazar his son; and Aaron died there on the top of the mountain: and Moses and Eleazar came down from the mountain.

Na mkutano wote ulipoona ya kuwa Haruni amekufa, wakamwombolea Haruni muda wa siku thelathini, maana, nyumba yote ya Israeli ikamwombolea. Hesabu 20:29

When all the congregation saw that Aaron was dead, they wept for Aaron thirty days, even all the house of Israel.