2 Mambo ya Nyakati 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Mambo ya Nyakati 1 (Swahili) 2nd Chronicles 1 (English)

Basi Sulemani, mwana wa Daudi, alithibitishwa katika ufalme wake, naye Bwana, Mungu wake, alikuwa pamoja naye, akamtukuza mno. 2 Mambo ya Nyakati 1:1

Solomon the son of David was strengthened in his kingdom, and Yahweh his God was with him, and magnified him exceedingly.

Sulemani akasema na Israeli wote, na maakida wa maelfu, na wa mamia, na waamuzi, na kila shehe wa Israeli wote, wakuu wa nyumba za mababa. 2 Mambo ya Nyakati 1:2

Solomon spoke to all Israel, to the captains of thousands and of hundreds, and to the judges, and to every prince in all Israel, the heads of the fathers' [houses].

Basi Sulemani akaenda mahali pa juu pa Gibeoni, na kusanyiko lote naye; kwani ndipo ilipokuwako hema ya kukutania ya Mungu, aliyoifanya Musa mtumishi wa Bwana jangwani. 2 Mambo ya Nyakati 1:3

So Solomon, and all the assembly with him, went to the high place that was at Gibeon; for there was the tent of meeting of God, which Moses the servant of Yahweh had made in the wilderness.

Lakini sanduku la Mungu, Daudi alikuwa amelipandisha kutoka Kiriath-yearimu mpaka mahali Daudi alipolitengenezea; maana amelitandia hema katika Yerusalemu. 2 Mambo ya Nyakati 1:4

But David had brought the ark of God up from Kiriath Jearim to [the place] that David had prepared for it; for he had pitched a tent for it at Jerusalem.

Tena madhabahu ya shaba, aliyoifanyiza Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, ilikuwako huko mbele ya maskani ya Bwana; Sulemani na kusanyiko wakaiendea. 2 Mambo ya Nyakati 1:5

Moreover the brazen altar, that Bezalel the son of Uri, the son of Hur, had made, was there before the tent of Yahweh: and Solomon and the assembly sought to it.

Sulemani akaipandia huko madhabahu ya shaba mbele za Bwana, iliyokuwako hemani pa kukutania, akatoa sadaka elfu za kuteketezwa juu yake. 2 Mambo ya Nyakati 1:6

Solomon went up there to the brazen altar before Yahweh, which was at the tent of meeting, and offered one thousand burnt offerings on it.

Usiku ule Mungu akamtokea Sulemani, akamwambia, Omba utakalo nikupe. 2 Mambo ya Nyakati 1:7

In that night did God appear to Solomon, and said to him, Ask what I shall give you.

Sulemani akamwambia Mungu, Umemfanyia baba yangu Daudi fadhili kuu, nawe umenimilikisha mimi badala yake. 2 Mambo ya Nyakati 1:8

Solomon said to God, You have shown great loving kindness to David my father, and have made me king in his place.

Basi sasa, Ee Bwana Mungu, na limyakinie baba yangu Daudi neno lako; maana umenitawaza niwe mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya nchi. 2 Mambo ya Nyakati 1:9

Now, Yahweh God, let your promise to David my father be established; for you have made me king over a people like the dust of the earth in multitude.

Basi sasa nipe hekima na maarifa, nijue kutoka na kuingia mbele ya watu hawa; kwa kuwa ni nani awezaye kuwahukumu watu wako hawa walio wengi? 2 Mambo ya Nyakati 1:10

Give me now wisdom and knowledge, that I may go out and come in before this people; for who can judge this your people, that is so great?

Naye Mungu akamwambia Sulemani, Kwa sababu neno hili lilikuwamo moyoni mwako, wala hukujitakia mali, wala utajiri, wala utukufu, wala maisha za wakuchukiao, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; bali umejitakia hekima na maarifa, upate kuwahukumu watu wangu, niliokutawaza juu yao; 2 Mambo ya Nyakati 1:11

God said to Solomon, Because this was in your heart, and you have not asked riches, wealth, or honor, nor the life of those who hate you, neither yet have asked long life; but have asked wisdom and knowledge for yourself, that you may judge my people, over whom I have made you king:

basi hekima na maarifa umepewa; nami nitakupa mali, na utajiri, na utukufu, kupita walivyokuwa navyo wafalme wote waliokuwa kabla yako, wala baada yako hapatakuwa na mtu atakayekuwa navyo. 2 Mambo ya Nyakati 1:12

wisdom and knowledge is granted to you; and I will give you riches, and wealth, and honor, such as none of the kings have had who have been before you; neither shall there any after you have the like.

Akaja Sulemani kutoka mahali pa juu pa Gibeoni, toka mbele ya hema ya kukutania, mpaka Yerusalemu; akatawala juu ya Israeli. 2 Mambo ya Nyakati 1:13

So Solomon came from the high place that was at Gibeon, from before the tent of meeting, to Jerusalem; and he reigned over Israel.

Sulemani akakusanya magari na wapandao farasi; naye alikuwa na magari elfu na mia nne, na wapandao farasi kumi na mbili elfu, aliowaweka katika miji ya magari, na pamoja na mfalme huko Yerusalemu. 2 Mambo ya Nyakati 1:14

Solomon gathered chariots and horsemen: and he had one thousand four hundred chariots, and twelve thousand horsemen, that he placed in the chariot cities, and with the king at Jerusalem.

Mfalme akafanya fedha na dhahabu kuwa kama mawe humo Yerusalemu, na mierezi akaifanya kuwa kama mikuyu iliyomo Shefela, kwa kuwa mingi. 2 Mambo ya Nyakati 1:15

The king made silver and gold to be in Jerusalem as stones, and cedars made he to be as the sycamore trees that are in the lowland, for abundance.

Nao farasi, aliokuwa nao Sulemani wakaletwa toka Misri; wakapewa wafanya biashara wake mfalme kwa makundi; kila kundi na thamani yake. 2 Mambo ya Nyakati 1:16

The horses which Solomon had were brought out of Egypt and from Kue; the king's merchants purchased them from Kue.

Nao hupandisha, na kuleta kutoka Misri gari kwa shekeli mia sita za fedha, na farasi kwa mia na hamsini, vivyo watu wakawaletea wafalme wote wa Wahiti, na wafalme wa Shamu, mikononi mwao.

2 Mambo ya Nyakati 1:17

They brought up and brought out of Egypt a chariot for six hundred pieces of silver, and a horse for one hundred fifty: and so for all the kings of the Hittites, and the kings of Syria, did they bring them out by their means.