2 Mambo ya Nyakati 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Mambo ya Nyakati 5 (Swahili) 2nd Chronicles 5 (English)

Hivyo ikaisha kazi yote Sulemani aliyoifanyia nyumba ya Bwana. Sulemani akaviingiza vitu alivyovitakasa baba yake Daudi; fedha, na dhahabu, na vyombo vyote, akavitia ndani ya hazina za nyumba ya Mungu. 2 Mambo ya Nyakati 5:1

Thus all the work that Solomon did for the house of Yahweh was finished. Solomon brought in the things that David his father had dedicated, even the silver, and the gold, and all the vessels, and put them in the treasuries of the house of God.

Ndipo Sulemani alipowakusanya wazee wa Israeli, na wakuu wote wa kabila, wakuu wa mbari za mababa wa wana wa Israeli, huko Yerusalemu, ili walipandishe sanduku la agano la Bwana kutoka mji wa Daudi, yaani, Sayuni. 2 Mambo ya Nyakati 5:2

Then Solomon assembled the elders of Israel, and all the heads of the tribes, the princes of the fathers' [houses] of the children of Israel, to Jerusalem, to bring up the ark of the covenant of Yahweh out of the city of David, which is Zion.

Wakakutana watu wote wa Israeli mbele ya mfalme wakati wa sikukuu, katika mwezi wa saba. 2 Mambo ya Nyakati 5:3

And all the men of Israel assembled themselves to the king at the feast, which was [in] the seventh month.

Wakaja wazee wote wa Israeli, nao Walawi wakajitwika sanduku. 2 Mambo ya Nyakati 5:4

All the elders of Israel came: and the Levites took up the ark;

Wakalipandisha sanduku, na ile hema ya kukutania, na vyombo vitakatifu vyote vilivyokuwamo Hemani, vitu hivyo makuhani Walawi wakavipandisha. 2 Mambo ya Nyakati 5:5

and they brought up the ark, and the tent of meeting, and all the holy vessels that were in the Tent; these did the priests the Levites bring up.

Mfalme Sulemani, na mkutano wote wa Israeli, waliokutanika kwake, walikuwako mbele ya sanduku, wakichinja dhabihu za kondoo na ng'ombe, wasiohesabika wala kujumlishwa kwa kuwa wengi. 2 Mambo ya Nyakati 5:6

King Solomon and all the congregation of Israel, that were assembled to him, were before the ark, sacrificing sheep and oxen, that could not be counted nor numbered for multitude.

Makuhani wakaliingiza sanduku la agano la Bwana mahali pake katika chumba cha ndani cha nyumba, patakatifu pa patakatifu, yaani, chini ya mabawa ya makerubi. 2 Mambo ya Nyakati 5:7

The priests brought in the ark of the covenant of Yahweh to its place, into the oracle of the house, to the most holy place, even under the wings of the cherubim.

Kwa maana makerubi yalinyosha mabawa yao juu ya mahali pa sanduku, makerubi yakalifunika lile sanduku na miti yake kwa juu. 2 Mambo ya Nyakati 5:8

For the cherubim spread forth their wings over the place of the ark, and the cherubim covered the ark and the poles of it above.

Na ile miti ilikuwa mirefu, hata ncha za miti zilionekana sandukuni mbele ya chumba cha ndani, lakini hazikuonekana nje; nayo iko kuko huko hata leo. 2 Mambo ya Nyakati 5:9

The poles were so long that the ends of the poles were seen from the ark before the oracle; but they were not seen outside: and there it is to this day.

Hamkuwa na kitu ndani ya sanduku, ila zile mbao mbili alizozitia Musa huko Horebu, Bwana alipofanya agano na wana wa Israeli, hapo walipotoka Misri. 2 Mambo ya Nyakati 5:10

There was nothing in the ark save the two tables which Moses put [there] at Horeb, when Yahweh made a covenant with the children of Israel, when they came out of Egypt.

Ikawa makuhani walipokwisha kutoka katika patakatifu; (kwani makuhani wote waliokuwapo, walikuwa wamejitakasa, wala hawakuzishika zamu zao; 2 Mambo ya Nyakati 5:11

It happened, when the priests were come out of the holy place, (for all the priests who were present had sanctified themselves, and did not keep their divisions;

tena Walawi waimbaji, wote pia, yaani Asafu, na Hemani, na Yeduthuni, na wana wao, na ndugu zao, hali wamevaa kitani safi, wenye matoazi na vinanda na vinubi, wamesimama upande wa mashariki wa madhabahu, na pamoja nao makuhani mia na ishirini wakipiga panda;) 2 Mambo ya Nyakati 5:12

also the Levites who were the singers, all of them, even Asaph, Heman, Jeduthun, and their sons and their brothers, arrayed in fine linen, with cymbals and psalteries and harps, stood at the east end of the altar, and with them one hundred twenty priests sounding with trumpets;)

hata ikawa, wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti moja ya kumsifu na kumshukuru Bwana nao wakipaza sauti pamoja na panda na matoazi na vinanda, wakimsifu Bwana, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele; ndipo nyumba ikajawa na wingu, naam, nyumba ya Bwana, 2 Mambo ya Nyakati 5:13

it happened, when the trumpeters and singers were as one, to make one sound to be heard in praising and thanking Yahweh; and when they lifted up their voice with the trumpets and cymbals and instruments of music, and praised Yahweh, [saying], For he is good; for his loving kindness endures forever; that then the house was filled with a cloud, even the house of Yahweh,

hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya lile wingu; kwa kuwa nyumba ya Mungu imejaa utukufu wa Bwana. 2 Mambo ya Nyakati 5:14

so that the priests could not stand to minister by reason of the cloud: for the glory of Yahweh filled the house of God.