2 Mambo ya Nyakati 7 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Mambo ya Nyakati 7 (Swahili) 2nd Chronicles 7 (English)

Basi Sulemani alipokwisha maombi hayo, moto ukashuka kutoka mbinguni, ukateketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu; utukufu wa Bwana ukaijaza nyumba. 2 Mambo ya Nyakati 7:1

Now when Solomon had made an end of praying, the fire came down from heaven, and consumed the burnt offering and the sacrifices; and the glory of Yahweh filled the house.

Wala makuhani hawakuweza kuingia nyumbani mwa Bwana, kwa kuwa utukufu wa Bwana umeijaza nyumba ya Bwana. 2 Mambo ya Nyakati 7:2

The priests could not enter into the house of Yahweh, because the glory of Yahweh filled Yahweh's house.

Wakatazama wana wa Israeli wote, uliposhuka ule moto, utukufu wa Bwana ulipokuwapo juu ya nyumba; wakasujudu kifulifuli hata nchi sakafuni, wakaabudu, wakamshukuru Bwana, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele. 2 Mambo ya Nyakati 7:3

All the children of Israel looked on, when the fire came down, and the glory of Yahweh was on the house; and they bowed themselves with their faces to the ground on the pavement, and worshiped, and gave thanks to Yahweh, [saying], For he is good; for his loving kindness endures for ever.

Ndipo mfalme na watu wote wakatoa dhabihu mbele za Bwana. 2 Mambo ya Nyakati 7:4

Then the king and all the people offered sacrifice before Yahweh.

Mfalme Sulemani akatoa sadaka ya ng'ombe ishirini na mbili elfu, na kondoo mia na ishirini elfu. Ndivyo mfalme na watu wote walivyoifanya wakfu nyumba ya Mungu. 2 Mambo ya Nyakati 7:5

King Solomon offered a sacrifice of twenty-two thousand oxen, and a hundred and twenty thousand sheep. So the king and all the people dedicated the house of God.

Wakasimama makuhani sawasawa na malinzi yao; Walawi nao pamoja na vinanda vya Bwana, alivyovifanya Daudi mfalme, ili kumshukuru Bwana, kwa maana fadhili zake ni za milele, hapo aliposifu Daudi kwa mikono yao; nao makuhani wakapiga panda mbele yao; nao Israeli wote wakasimama. 2 Mambo ya Nyakati 7:6

The priests stood, according to their offices; the Levites also with instruments of music of Yahweh, which David the king had made to give thanks to Yahweh, (for his loving kindness endures for ever), when David praised by their ministry: and the priests sounded trumpets before them; and all Israel stood.

Tena Sulemani akaitakasa behewa katikati, iliyokuwa mbele ya nyumba ya Bwana; kwa kuwa hapo ndipo alipotoa sadaka za kuteketezwa, na mafuta ya sadaka za amani; kwa sababu ile madhabahu ya shaba aliyoifanya Sulemani haikutosha kuzipokea sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya unga, na mafuta. 2 Mambo ya Nyakati 7:7

Moreover Solomon made the middle of the court holy that was before the house of Yahweh; for there he offered the burnt offerings, and the fat of the peace-offerings, because the brazen altar which Solomon had made was not able to receive the burnt offering, and the meal-offering, and the fat.

Basi, wakati ule Sulemani akafanya sikukuu, na Israeli wote pamoja naye, kusanyiko kubwa sana, toka maingilio ya Hamathi mpaka kijito cha Misri, muda wa siku saba. 2 Mambo ya Nyakati 7:8

So Solomon held the feast at that time seven days, and all Israel with him, a very great assembly, from the entrance of Hamath to the brook of Egypt.

Hata siku ya nane wakaita kusanyiko la makini; kwa maana walishika kuitakasa madhabahu siku saba, na sikukuu siku saba. 2 Mambo ya Nyakati 7:9

On the eighth day they held a solemn assembly: for they kept the dedication of the altar seven days, and the feast seven days.

Akawaruhusu watu waende hemani kwao siku ya ishirini na tatu, ya mwezi wa saba, wakifurahi na kuchangamka mioyoni kwa wema wote Bwana aliomfanyia Daudi, na Sulemani, na Israeli watu wake. 2 Mambo ya Nyakati 7:10

On the three and twentieth day of the seventh month he sent the people away to their tents, joyful and glad of heart for the goodness that Yahweh had shown to David, and to Solomon, and to Israel his people.

Hivyo Sulemani akaimaliza nyumba ya Bwana, na nyumba ya mfalme; na yote yaliyomwingia Sulemani moyoni ayafanye nyumbani mwa Bwana, na nyumbani mwake mwenyewe, akayafanikisha. 2 Mambo ya Nyakati 7:11

Thus Solomon finished the house of Yahweh, and the king's house: and all that came into Solomon's heart to make in the house of Yahweh, and in his own house, he prosperously effected.

Bwana akamtokea Sulemani usiku, akamwambia, Nimesikia uliyoyaomba, na mahali hapa nimejichagulia kuwa nyumba ya dhabihu. 2 Mambo ya Nyakati 7:12

Yahweh appeared to Solomon by night, and said to him, I have heard your prayer, and have chosen this place to myself for a house of sacrifice.

Nikizifunga mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, au nikiwapelekea watu wangu tauni; 2 Mambo ya Nyakati 7:13

If I shut up the sky so that there is no rain, or if I command the locust to devour the land, or if I send pestilence among my people;

ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao. 2 Mambo ya Nyakati 7:14

if my people, who are called by my name, shall humble themselves, and pray, and seek my face, and turn from their wicked ways; then will I hear from heaven, and will forgive their sin, and will heal their land.

Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa. 2 Mambo ya Nyakati 7:15

Now my eyes shall be open, and my ears attentive, to the prayer that is made in this place.

Maana sasa nimeichagua nyumba hii na kuitakasa, ili kwamba jina langu lipate kuwako huko milele; yatakuwako na macho yangu, na moyo wangu daima. 2 Mambo ya Nyakati 7:16

For now have I chosen and made this house holy, that my name may be there forever; and my eyes and my heart shall be there perpetually.

Nawe, ukienda mbele yangu kama alivyokwenda Daudi baba yako, ufanye sawasawa na yote niliyokuamuru, na kuzishika sheria zangu na hukumu zangu; 2 Mambo ya Nyakati 7:17

As for you, if you will walk before me as David your father walked, and do according to all that I have commanded you, and will keep my statutes and my ordinances;

ndipo nitakithibitisha kiti cha enzi cha ufalme wako, kama nilivyoagana na Daudi baba yako, nikisema, Hutakosa kuwa na mtu wa kutawala katika Israeli. 2 Mambo ya Nyakati 7:18

then I will establish the throne of your kingdom, according as I covenanted with David your father, saying, There shall not fail you a man to be ruler in Israel.

Lakini mkigeuka, na kuziacha sheria zangu na amri zangu nilizoweka mbele yenu, mkienda, na kuitumikia miungu mingine, na kuiabudu; 2 Mambo ya Nyakati 7:19

But if you turn away, and forsake my statutes and my commandments which I have set before you, and shall go and serve other gods, and worship them;

ndipo nitawang'oa katika nchi yangu niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaiondosha itoke mbele zangu, nami nitaifanya kuwa mithali na tukano katikati ya watu wote. 2 Mambo ya Nyakati 7:20

then will I pluck them up by the roots out of my land which I have given them; and this house, which I have made holy for my name, will I cast out of my sight, and I will make it a proverb and a byword among all peoples.

Na nyumba hii, iliyo juu, kila apitaye ataona ushangao, atasema, Mbona Bwana ameitendea hivi nchi hii, na nyumba hii? 2 Mambo ya Nyakati 7:21

This house, which is so high, everyone who passes by it shall be astonished, and shall say, Why has Yahweh done thus to this land, and to this house?

Nao watajibu, Kwa sababu walimwacha Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka nchi ya Misri, wakashikamana na miungu mingine, wakaiabudu, na kuitumikia; kwa hiyo ameyaleta mabaya haya yote juu yao. 2 Mambo ya Nyakati 7:22

They shall answer, Because they forsook Yahweh, the God of their fathers, who brought them forth out of the land of Egypt, and laid hold on other gods, and worshiped them, and served them: therefore has he brought all this evil on them.