Kumbukumbu la Torati 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kumbukumbu la Torati 3 (Swahili) Deuteronomy 3 (English)

Ndipo tukageuka, tukakwea njia ya Bashani; na Ogu, mfalme wa Bashani, akatutokea juu yetu, yeye na watu wake wote, kuja kupigana huko Edrei. Kumbukumbu la Torati 3:1

Then we turned, and went up the way to Bashan: and Og the king of Bashan came out against us, he and all his people, to battle at Edrei.

Bwana akaniambia, Usimwogope; kwa kuwa nimemtia mkononi mwako, yeye na watu wake wote na nchi yake; nawe utamtenda mfano wa ulivyomtenda Sihoni, mfalme wa Waamori, aliyekuwa akikaa Heshboni. Kumbukumbu la Torati 3:2

Yahweh said to me, Don't fear him; for I have delivered him, and all his people, and his land, into your hand; and you shall do to him as you did to Sihon king of the Amorites, who lived at Heshbon.

Basi Bwana, Mungu wetu, akamtia mikononi mwetu na Ogu mfalme wa Bashani, na watu wake wote; tukampiga, asisaziwe cho chote. Kumbukumbu la Torati 3:3

So Yahweh our God delivered into our hand Og also, the king of Bashan, and all his people: and we struck him until none was left to him remaining.

Tukatwaa miji yake yote wakati huo; hapakuwa na mji tusiotwaa kwao miji sitini, nchi yote ya Argobu, ndio ufalme wa Ogu ulio katika Bashani. Kumbukumbu la Torati 3:4

We took all his cities at that time; there was not a city which we didn't take from them; sixty cities, all the region of Argob, the kingdom of Og in Bashan.

Miji hiyo yote ilikuwa yenye maboma marefu, na malango, na makomeo, pamoja na miji isiyokuwa na maboma, mingi sana. Kumbukumbu la Torati 3:5

All these were cities fortified with high walls, gates, and bars; besides the unwalled towns a great many.

Tukaiharibu kabisa, kama tulivyomfanya huyo Sihoni, mfalme wa Heshboni, kwa kuharibu kabisa kila mji uliokuwa na watu, pamoja na wanawake na watoto. Kumbukumbu la Torati 3:6

We utterly destroyed them, as we did to Sihon king of Heshbon, utterly destroying every inhabited city, with the women and the little ones.

Lakini wanyama wote wa mji, na nyara za miji, tulitwaa kuwa mawindo yetu. Kumbukumbu la Torati 3:7

But all the cattle, and the spoil of the cities, we took for a prey to ourselves.

Tukaitwaa na nchi wakati huo, katika mikono ya hao wafalme wawili wa Waamori waliokuwa ng'ambo ya Yordani, tokea bonde la Arnoni mpaka kilima cha Hermoni; Kumbukumbu la Torati 3:8

We took the land at that time out of the hand of the two kings of the Amorites who were beyond the Jordan, from the valley of the Arnon to Mount Hermon;

(na hiyo Hermoni Wasidoni huiita Sirioni, na Waamori huiita Seniri); Kumbukumbu la Torati 3:9

([which] Hermon the Sidonians call Sirion, and the Amorites call it Senir;)

miji yote ya nchi tambarare, na Gileadi yote, na Bashani yote, mpaka Saleka na Edrei, nayo ni miji ya ufalme wa Ogu katika Bashani. Kumbukumbu la Torati 3:10

all the cities of the plain, and all Gilead, and all Bashan, to Salecah and Edrei, cities of the kingdom of Og in Bashan.

(Kwani aliyesalia katika mabaki ya Warefai ni Ogu pekee, mfalme wa Bashani; tazama, kitanda chake kilikuwa kitanda cha chuma; kitanda hicho je! Hakiko Raba kwa wana wa Amoni? Urefu wake ulikuwa ni mikono kenda,na upana wake mikono minne,kwa mfano wa mkono wa mtu) Kumbukumbu la Torati 3:11

(For only Og king of Bashan remained of the remnant of the Rephaim; behold, his bedstead was a bedstead of iron; isn't it in Rabbah of the children of Ammon? nine cubits was the length of it, and four cubits the breadth of it, after the cubit of a man.)

Na nchi hiyo tuliitwaa ikawa milki yetu, wakati huo; tokea Aroeri iliyo kwenye bonde la Arnoni, na nusu ya nchi ya milima ya Gileadi, na miji iliyokuwamo, niliwapa Wareubeni na Wagadi; Kumbukumbu la Torati 3:12

This land we took in possession at that time: from Aroer, which is by the valley of the Arnon, and half the hill-country of Gilead, and the cities of it, gave I to the Reubenites and to the Gadites:

na nchi ya Gileadi iliyobaki, na Bashani yote, maana huo ufalme wa Ogu niliwapa nusu ya kabila ya Manase; nchi yote ya Argobu, nayo ndiyo Bashani yote. (Na nchi hii yaitwa nchi ya Warefai. Kumbukumbu la Torati 3:13

and the rest of Gilead, and all Bashan, the kingdom of Og, gave I to the half-tribe of Manasseh; all the region of Argob, even all Bashan. (The same is called the land of Rephaim.

Yairi, mwana wa Manase, alitwaa nchi yote ya Argobu, hata mpaka wa Wageshuri na Wamaaka; akaziita nchi hizo Hawoth-yairi, kwa jina lake mwenyewe, hata hivi leo, maana, hizo nchi za Bashani.) Kumbukumbu la Torati 3:14

Jair the son of Manasseh took all the region of Argob, to the border of the Geshurites and the Maacathites, and called them, even Bashan, after his own name, Havvoth Jair, to this day.)

Na Makiri nilimpa Gileadi. Kumbukumbu la Torati 3:15

I gave Gilead to Machir.

Na Wareubeni na Wagadi niliwapa tokea Gileadi mpaka bonde la Arnoni, katikati ya bonde, na mpaka wake; mpaka mto wa Yaboki, nao ni mpaka wa wana wa Amoni; Kumbukumbu la Torati 3:16

To the Reubenites and to the Gadites I gave from Gilead even to the valley of the Arnon, the middle of the valley, and the border [of it], even to the river Jabbok, which is the border of the children of Ammon;

na nchi ya Araba nayo, na mto wa Yordani, na mpaka wake, tokea Kinerethi mpaka bahari ya hiyo Araba, nayo ni Bahari ya Chumvi, chini ya matelemko ya Pisga, upande wa mashariki. Kumbukumbu la Torati 3:17

the Arabah also, and the Jordan and the border [of it], from Chinnereth even to the sea of the Arabah, the Salt Sea, under the slopes of Pisgah eastward.

Nikawaamuru wakati huo, nikawaambia, Bwana, Mungu wenu, amewapa ninyi nchi hii mwimiliki, basi vukeni ng'ambo wenye silaha mbele ya ndugu zenu, wana wa Israeli, nyote mlio mashujaa. Kumbukumbu la Torati 3:18

I commanded you at that time, saying, Yahweh your God has given you this land to possess it: you shall pass over armed before your brothers the children of Israel, all the men of valor.

Lakini wake wenu na watoto wenu, na wanyama wenu wa mji, (nawajua kwamba mna wanyama wengi), na wakae katika miji yenu niliyowapa; Kumbukumbu la Torati 3:19

But your wives, and your little ones, and your cattle, (I know that you have much cattle), shall abide in your cities which I have given you,

hata Bwana awapumzishe ndugu zenu kama ninyi, nao pia waimiliki nchi wapewayo na Bwana, Mungu wenu, ng'ambo ya Yordani; ndipo mtakaporudi kila mmoja aende katika milki yake niliyowapa. Kumbukumbu la Torati 3:20

until Yahweh give rest to your brothers, as to you, and they also possess the land which Yahweh your God gives them beyond the Jordan: then shall you return every man to his possession, which I have given you.

Nikamwamuru Yoshua wakati huo, nikamwambia, Macho yako yameona yote aliyowatenda Bwana, Mungu wenu, wale wafalme wawili, navyo ndivyo atakavyoutenda Bwana kila ufalme huko uvukiako. Kumbukumbu la Torati 3:21

I commanded Joshua at that time, saying, Your eyes have seen all that Yahweh your God has done to these two kings: so shall Yahweh do to all the kingdoms where you go over.

Msiwache, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye awapiganiaye. Kumbukumbu la Torati 3:22

You shall not fear them; for Yahweh your God, he it is who fights for you.

Nikamnyenyekea Bwana wakati huo, nikamwambia, Kumbukumbu la Torati 3:23

I begged Yahweh at that time, saying,

Ee Bwana Mungu, umeanza kumwonyesha mtumishi wako ukubwa wako, na mkono wako wa nguvu; kwani kuna mungu gani mbinguni au duniani awezaye kufanya mfano wa kazi zako, na mfano wa matendo yako yenye nguvu? Kumbukumbu la Torati 3:24

Lord Yahweh, you have begun to show your servant your greatness, and your strong hand: for what god is there in heaven or in earth, that can do according to your works, and according to your mighty acts?

Nami nakuomba nivuke, nikaione hiyo nchi nzuri iliyoko ng'ambo ya Jordani, mlima ule mzuri, na Lebanoni. Kumbukumbu la Torati 3:25

Please let me go over and see the good land that is beyond the Jordan, that goodly mountain, and Lebanon.

Lakini Bwana alikuwa amenikasirikia kwa ajili yenu, asinisikize; Bwana akaniambia, Na ikutoshe, usinene nami zaidi jambo hili. Kumbukumbu la Torati 3:26

But Yahweh was angry with me for your sakes, and didn't listen to me; and Yahweh said to me, Let it suffice you; speak no more to me of this matter.

Kwea katika kilele cha Pisga ukainue macho yako upande wa magharibi, na kaskazini, na kusini, na mashariki, ukatazame kwa macho yako, kwa maana huuvuki mto huu wa Yordani. Kumbukumbu la Torati 3:27

Go up to the top of Pisgah, and lift up your eyes westward, and northward, and southward, and eastward, and see with your eyes: for you shall not go over this Jordan.

Lakini mwagize Yoshua umtie moyo mkuu, umtie na nguvu; kwani ndiye atakayevuka mbele ya watu hawa, na nchi utakayoiona atawarithisha yeye. Kumbukumbu la Torati 3:28

But charge Joshua, and encourage him, and strengthen him; for he shall go over before this people, and he shall cause them to inherit the land which you shall see.

Basi tukakaa katika bonde lililoelekea Beth-peori. Kumbukumbu la Torati 3:29

So we abode in the valley over against Beth Peor.