Kutoka 37 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kutoka 37 (Swahili) Exodus 37 (English)

Kisha Bezaleli akalifanya lile sanduku la mti wa mshita, urefu wake ulikuwa dhiraa mbili na nusu, na upana wake ulikuwa dhiraa moja na nusu, na kwenda juu kwake kulikuwa ni dhiraa moja na nusu; Kutoka 37:1

Bezalel made the ark of acacia wood. Its length was two and a half cubits, and its breadth a cubit and a half, and a cubit and a half its height.

akalifunika dhahabu safi, ndani na nje, akafanya na ukingo wa dhahabu kulizunguka pande zote. Kutoka 37:2

He overlaid it with pure gold inside and outside, and made a molding of gold for it round about.

Naye akasubu pete nne za dhahabu kwa ajili yake, katika miguu yake minne; pete mbili upande wake mmoja na pete mbili upande wake wa pili. Kutoka 37:3

He cast four rings of gold for it, in its four feet; even two rings on its one side, and two rings on its other side.

Akafanya na miti ya kulichukulia, ya mti wa mshita akaifunika dhahabu. Kutoka 37:4

He made poles of acacia wood, and overlaid them with gold.

Naye akaitia hiyo miti katika zile pete zilizokuwa ubavuni mwa sanduku, ili kulichukua hilo sanduku. Kutoka 37:5

He put the poles into the rings on the sides of the ark, to bear the ark.

Kisha akafanya kiti cha rehema cha dhahabu safi; urefu wake ulikuwa dhiraa mbili na nusu na upana wake ulikuwa dhiraa moja na nusu. Kutoka 37:6

He made a mercy seat of pure gold. Its length was two and a half cubits, and a cubit and a half its breadth.

Kisha akafanya makerubi mawili ya dhahabu; akayafanya ya kazi ya kufua, yawe katika miisho miwili ya kiti cha rehema; Kutoka 37:7

He made two cherubim of gold. He made them of beaten work them, at the two ends of the mercy seat;

kerubi moja mwisho huu, na kerubi moja mwisho huu; alifanya hayo makerubi mawili ya kitu kimoja na hicho kiti cha rehema katika miisho yake miwili. Kutoka 37:8

one cherub at the one end, and one cherub at the other end. He made the cherubim of one piece with the mercy seat at its two ends.

Na hayo makerubi yakayanyosha mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zilikuwa zaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zilikuwa zikielekea kiti cha rehema. Kutoka 37:9

The cherubim spread out their wings on high, covering the mercy seat with their wings, with their faces toward one another. The faces of the cherubim were toward the mercy seat.

Kisha akafanya hiyo meza ya mti wa mshita; urefu wake ulikuwa ni dhiraa mbili, na upana wake ulikuwa ni dhiraa moja, na kwenda juu kwake kulikuwa ni dhiraa moja na nusu; Kutoka 37:10

He made the table of acacia wood. Its length was two cubits, and its breadth was a cubit, and its height was a cubit and a half.

naye akaifunika dhahabu safi, akaifanyia ukingo wa dhahabu kuizunguka pande zote. Kutoka 37:11

He overlaid it with pure gold, and made a gold molding around it.

Kisha akaifanyia upapi wa upana wa shibiri kuizunguka pande zote, akauzungushia ukingo wa urembo wa dhahabu ule upapi. Kutoka 37:12

He made a border of a handbreadth around it, and made a golden molding on its border around it.

Naye akasubu vikuku vinne vya dhahabu kwa ajili yake, akavitia vile vikuku katika pembe nne, katika miguu yake minne. Kutoka 37:13

He cast four rings of gold for it, and put the rings in the four corners that were on its four feet.

Vile vikuku vilikuwa karibu na ule upapi, ili viwe mahali pa kutilia ile miti, ya kuichukulia meza. Kutoka 37:14

The rings were close by the border, the places for the poles to carry the table.

Naye akaifanya hiyo miti ya kuichukulia, ya mti wa mshita, akaifunika dhahabu, ili kuichukua hiyo meza. Kutoka 37:15

He made the poles of acacia wood, and overlaid them with gold, to carry the table.

Kisha, vile vyombo vilivyokuwa juu ya meza, sahani zake, na miiko yake, na bakuli zake, na makopo yake ya kumiminia, akavifanya vya dhahabu safi. Kutoka 37:16

He made the vessels which were on the table, its dishes, its spoons, its bowls, and its pitchers with which to pour out, of pure gold.

Kisha akakifanya kile kinara cha taa cha dhahabu safi, akakifanya kile kinara cha taa cha kazi ya kufua, tako lake, na mti wake; vikombe vyake, na matovu yake, na maua yake, vyote vilikuwa vya kitu kimoja nacho, Kutoka 37:17

He made the lampstand of pure gold. He made the lampstand of beaten work. Its base, its shaft, its cups, its buds, and its flowers were of one piece with it.

nacho kilikuwa na matawi sita yaliyotoka ubavuni mwake; matawi matatu ya kinara yalikuwa upande huu, na matawi matatu ya kinara yalikuwa upande huu; Kutoka 37:18

There were six branches going out of its sides: three branches of the lampstand out of its one side, and three branches of the lampstand out of its other side:

vikombe vitatu, vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi vilikuwa katika tawi moja, tovu na ua; na vikombe vitatu, vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi, katika tawi la pili, tovu na ua; yalikuwa ni vivyo hivyo yale matawi sita yaliyokuwa katika hicho kinara. Kutoka 37:19

three cups made like almond-blossoms in one branch, a bud and a flower, and three cups made like almond-blossoms in the other branch, a bud and a flower: so for the six branches going out of the lampstand.

Katika kinara mlikuwa na vikombe vinne, vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi, matovu yake na maua yake; Kutoka 37:20

In the lampstand were four cups made like almond-blossoms, its buds and its flowers;

kisha chini ya matawi mawili mlikuwa na tovu iliyokuwa ya kitu kimoja nacho, na chini ya matawi mawili mengine mlikuwa na tovu ya kitu kimoja nacho, tena chini ya matawi mawili hayo mengine mlikuwa na tovu ya kitu kimoja nacho; kwa ajili ya hayo matawi sita, yaliyotokana nacho. Kutoka 37:21

and a bud under two branches of one piece with it, and a bud under two branches of one piece with it, and a bud under two branches of one piece with it, for the six branches going out of it.

Hayo matovu yake na matawi yake yalikuwa ya kitu kimoja nacho; kinara hicho kizima chote pia ni kazi moja ya kufua ya dhahabu safi. Kutoka 37:22

Their buds and their branches were of one piece with it. The whole thing was one beaten work of pure gold.

Kisha akafanya taa zake saba, na makoleo yake, na visahani vyake, vya dhahabu safi. Kutoka 37:23

He made its seven lamps, and its snuffers, and its snuff dishes, of pure gold.

Akakifanya cha talanta moja ya dhahabu safi, pamoja na vyombo vyake vyote. Kutoka 37:24

He made it of a talent of pure gold, with all its vessels.

Kisha akafanya hiyo madhabahu ya kufukizia uvumba ya mti wa mshita; urefu wake ulikuwa ni dhiraa moja, na upana wake ulikuwa ni dhiraa moja, ilikuwa mraba; na kwenda juu kwake kulikuwa ni dhiraa mbili; na pembe zake zilikuwa za kitu kimoja nayo. Kutoka 37:25

He made the altar of incense of acacia wood. It was square: its length was a cubit, and its breadth a cubit. Its height was two cubits. Its horns were of one piece with it.

Naye akaifunika dhahabu safi, upande wa juu, na mbavu zake pande zote, na hizo pembe zake; akaifanyia na ukingo wa dhahabu kuizunguka pande zote. Kutoka 37:26

He overlaid it with pure gold, its top, its sides around it, and its horns. He made a gold molding around it.

Naye akaifanyia vikuku viwili vya dhahabu na kuvitia chini ya ukingo wake, katika mbavu zake mbili, katika pande zake mbili, viwe ni mahali pa hiyo miti ya kuichukulia. Kutoka 37:27

He made two golden rings for it under its molding crown, on its two ribs, on its two sides, for places for poles with which to carry it.

Kisha akafanya hiyo miti kwa mti wa mshita, na kuifunika dhahabu. Kutoka 37:28

He made the poles of acacia wood, and overlaid them with gold.

Kisha akayafanya hayo mafuta matakatifu ya kutiwa, na ule uvumba safi wa viungo vya manukato vizuri, kwa kuandama kazi ya mtengezaji manukato. Kutoka 37:29

He made the holy anointing oil and the pure incense of sweet spices, after the art of the perfumer.