Kutoka 9 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kutoka 9 (Swahili) Exodus 9 (English)

Ndipo Bwana akamwambia Musa, Ingia wewe kwa Farao, umwambie, Bwana, Mungu wa Waebrania, yuasema, Wape ruhusa watu wangu ili waende wanitumikie. Kutoka 9:1

Then Yahweh said to Moses, "Go in to Pharaoh, and tell him, 'This is what Yahweh, the God of the Hebrews, says: "Let my people go, that they may serve me.

Kwani ukikataa kuwapa ruhusa waende, na kuzidi kuwazuia, Kutoka 9:2

For if you refuse to let them go, and hold them still,

tazama, mkono wa Bwana u juu ya wanyama wako wa mifugo walioko kondeni, juu ya farasi, na juu ya punda, na juu ya ngamia, na juu ya ng'ombe, na juu ya kondoo; kutakuwa na tauni nzito sana. Kutoka 9:3

behold, the hand of Yahweh is on your cattle which are in the field, on the horses, on the donkeys, on the camels, on the herds, and on the flocks with a very grievous pestilence.

Kisha Bwana atawatenga wanyama wa Israeli na wanyama wa Misri; wala hakitakufa kitu cho chote cha wana wa Israeli. Kutoka 9:4

Yahweh will make a distinction between the cattle of Israel and the cattle of Egypt; and there shall nothing die of all that belongs to the children of Israel."'"

Naye Bwana akaweka muda, akasema, Kesho Bwana atalifanya jambo hili katika nchi. Kutoka 9:5

Yahweh appointed a set time, saying, "Tomorrow Yahweh shall do this thing in the land."

Bwana akalifanya jambo hilo siku ya pili, na wanyama wote wa kufugwa wa Misri wakafa; lakini katika wanyama wa wana wa Israeli hakufa hata mmoja. Kutoka 9:6

Yahweh did that thing on the next day; and all the cattle of Egypt died, but of the cattle of the children of Israel, not one died.

Farao akatuma watu, na tazama, hapana mmoja aliyekufa katika wanyama wa wana wa Israeli. Lakini moyo wa Farao ulikuwa mzito, wala hakuwapa hao watu ruhusa waende zao. Kutoka 9:7

Pharaoh sent, and, behold, there was not so much as one of the cattle of the Israelites dead. But the heart of Pharaoh was stubborn, and he didn't let the people go.

Bwana akawaambia Musa na Haruni, Jitwalieni konzi za majivu ya tanuuni, kisha Musa na ayarushe juu kuelekea mbinguni mbele ya Farao. Kutoka 9:8

Yahweh said to Moses and to Aaron, "Take to you handfuls of ashes of the furnace, and let Moses sprinkle it toward the sky in the sight of Pharaoh.

Nayo yatakuwa ni mavumbi membamba juu ya nchi yote ya Misri, nayo yatakuwa majipu yenye kufura na kutumbuka juu ya wanadamu na juu ya wanyama, katika nchi yote ya Misri. Kutoka 9:9

It shall become small dust over all the land of Egypt, and shall be a boil breaking forth with boils on man and on animal, throughout all the land of Egypt."

Basi wakatwaa majivu ya tanuuni, na kusimama mbele ya Farao; na Musa akayarusha juu mbinguni nayo yakawa ni majipu yenye kufura na kutumbuka juu ya wanadamu na juu ya wanyama. Kutoka 9:10

They took ashes of the furnace, and stood before Pharaoh; and Moses sprinkled it up toward the sky; and it became a boil breaking forth with boils on man and on animal.

Nao wale waganga hawakuweza kusimama mbele ya Musa kwa sababu ya hayo majipu, kwa maana hao waganga walikuwa na majipu, na Wamisri wote walikuwa nayo. Kutoka 9:11

The magicians couldn't stand before Moses because of the boils; for the boils were on the magicians, and on all the Egyptians.

Bwana akaufanya mgumu moyo wa Farao, asiwasikize; vile vile kama Bwana alivyomwambia Musa. Kutoka 9:12

Yahweh hardened the heart of Pharaoh, and he didn't listen to them, as Yahweh had spoken to Moses.

Bwana akamwambia Musa, Ondoka asubuhi na mapema, ukasimame mbele ya Farao, umwambie, Bwana, Mungu wa Waebrania, asema, Wape watu wangu ruhusa waende ili wanitumikie. Kutoka 9:13

Yahweh said to Moses, "Rise up early in the morning, and stand before Pharaoh, and tell him, 'This is what Yahweh, the God of the Hebrews, says: "Let my people go, that they may serve me.

Kwani wakati huu nitaleta mapigo yangu yote juu ya moyo wako, na juu ya watumishi wako, na juu ya watu wako; ili upate kujua ya kuwa hapana mmoja mfano wa mimi ulimwenguni mwote. Kutoka 9:14

For this time I will send all my plagues against your heart, against your officials, and against your people; that you may know that there is none like me in all the earth.

Kwa kuwa wakati huu ningekwisha kuunyosha mkono wangu, na kukupiga wewe na watu wako, kwa tauni, nawe ungekatiliwa mbali na kuondolewa katika nchi; Kutoka 9:15

For now I would have put forth my hand, and struck you and your people with pestilence, and you would have been cut off from the earth;

lakini, nilikusimamisha wewe kwa sababu hii hii, ili nikuonyeshe uweza wangu, tena kwamba jina langu litangazwe katika dunia yote. Kutoka 9:16

but indeed for this cause I have made you stand: to show you my power, and that my name may be declared throughout all the earth;

Nawe, je! Hata sasa wajitukuza juu ya watu wangu, usiwape ruhusa waende zao? Kutoka 9:17

as you still exalt yourself against my people, that you won't let them go.

Tazama, kesho wakati kama huu, nitanyesha mvua ya mawe nzito sana, ambayo mfano wake haujakuwa huko Misri tangu siku ile ilipoanza kuwa hata hivi sasa. Kutoka 9:18

Behold, tomorrow about this time I will cause it to rain a very grievous hail, such as has not been in Egypt since the day it was founded even until now.

Basi sasa tuma wahimize waingie ndani wanyama wako na hayo yote uliyo nayo mashambani; kwani kila mtu na kila mnyama apatikanaye mashambani, wasioletwa nyumbani, hiyo mvua ya mawe itanyesha juu yao, nao watakufa. Kutoka 9:19

Now therefore command that all of your cattle and all that you have in the field be brought into shelter. Every man and animal that is found in the field, and isn't brought home, the hail shall come down on them, and they shall die."'"

Yeye aliyelicha neno la Bwana miongoni mwa watumishi wa Farao aliwakimbiza watumishi wake na wanyama wake waingie nyumbani; Kutoka 9:20

Those who feared the word of Yahweh among the servants of Pharaoh made their servants and their cattle flee into the houses.

na yeye asiyelitia moyoni neno la Bwana akawaacha watumishi wake na wanyama wake mashambani. Kutoka 9:21

Whoever didn't regard the word of Yahweh left his servants and his cattle in the field.

Bwana akamwambia Musa, Nyosha mkono wako kuelekea mbinguni, ili iwe mvua ya mawe katika nchi yote ya Misri, juu ya wanadamu na juu ya wanyama, na juu ya mboga zote za mashamba, katika nchi yote ya Misri. Kutoka 9:22

Yahweh said to Moses, "Stretch forth your hand toward the sky, that there may be hail in all the land of Egypt, on man, and on animal, and on every herb of the field, throughout the land of Egypt."

Musa akaunyosha mkono wake kuelekea mbinguni; na Bwana akaleta ngurumo na mvua ya mawe, na moto ukashuka juu ya nchi; Bwana akanyesha mvua ya mawe juu ya nchi yote ya Misri. Kutoka 9:23

Moses stretched forth his rod toward the heavens, and Yahweh sent thunder, hail, and lightning flashed down to the earth. Yahweh rained hail on the land of Egypt.

Basi palikuwa na mvua ya mawe, na moto uliochanganyikana na ile mvua ya mawe, nzito sana, ambayo mfano wake haukuwapo katika nchi yote ya Misri tangu ilipoanza kuwa taifa. Kutoka 9:24

So there was very severe hail, and lightning mixed with the hail, such as had not been in all the land of Egypt since it became a nation.

Na ile mvua ya mawe ikapiga kila kilichokuwako mashambani, binadamu na mnyama, katika nchi yote ya Misri; hiyo mvua ya mawe ikapiga kila mmea wa mashambani, na kuuvunja kila mti wa mashamba. Kutoka 9:25

The hail struck throughout all the land of Egypt all that was in the field, both man and animal; and the hail struck every herb of the field, and broke every tree of the field.

Katika nchi ya Gosheni peke yake, walikokaa wana wa Israeli, haikuwako mvua ya mawe. Kutoka 9:26

Only in the land of Goshen, where the children of Israel were, there was no hail.

Farao akatuma watu, na kuwaita Musa na Haruni, na kuwaambia, Mimi nimekosa wakati huu; Bwana ni mwenye haki, na mimi na watu wangu tu waovu. Kutoka 9:27

Pharaoh sent, and called for Moses and Aaron, and said to them, "I have sinned this time. Yahweh is righteous, and I and my people are wicked.

Mwombeni Bwana; kwa kuwa zimekuwa za kutosha ngurumo hizo kuu na hii mvua ya mawe; nami nitawapa ninyi ruhusa mwende zenu, msikae zaidi. Kutoka 9:28

Pray to Yahweh; for there has been enough of mighty thunderings and hail. I will let you go, and you shall stay no longer."

Musa akamwambia, Mara nitakapotoka mjini nitamwinulia Bwana mikono yangu; na hizo ngurumo zitakoma, wala haitanyesha mvua ya mawe tena; ili upate kujua ya kuwa dunia hii ni ya Bwana. Kutoka 9:29

Moses said to him, "As soon as I have gone out of the city, I will spread abroad my hands to Yahweh. The thunders shall cease, neither shall there be any more hail; that you may know that the earth is Yahweh's.

Lakini, wewe na watumishi wako, najua ya kuwa ninyi hamtamcha Bwana Mungu bado. Kutoka 9:30

But as for you and your servants, I know that you don't yet fear Yahweh God."

Kitani na shayiri zilipigwa; maana shayiri zilikuwa na masuke na kitani zilikuwa katika kutoa maua. Kutoka 9:31

The flax and the barley were struck, for the barley was in the ear, and the flax was in bloom.

Lakini ngano na kusemethu hazikupigwa; maana, zilikuwa hazijakua bado. Kutoka 9:32

But the wheat and the spelt were not struck, for they had not grown up.

Musa akatoka mjini, kutoka kwa Farao, akamwinulia Bwana mikono yake; na zile ngurumo na ile mvua ya mawe zikakoma, wala mvua haikunyesha juu ya nchi. Kutoka 9:33

Moses went out of the city from Pharaoh, and spread abroad his hands to Yahweh; and the thunders and hail ceased, and the rain was not poured on the earth.

Farao alipoona ya kwamba mvua na mvua ya mawe na ngurumo zimekoma, akazidi kufanya dhambi, na kuufanya moyo wake mzito, yeye na watumishi wake. Kutoka 9:34

When Pharaoh saw that the rain and the hail and the thunders were ceased, he sinned yet more, and hardened his heart, he and his servants.

Moyo wa Farao ukawa ni mgumu naye hakuwapa wana wa Israeli ruhusa waende zao; kama Bwana alivyonena kwa kinywa cha Musa.

Kutoka 9:35

The heart of Pharaoh was hardened, and he didn't let the children of Israel go, just as Yahweh had spoken through Moses.