Kutoka 28 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kutoka 28 (Swahili) Exodus 28 (English)

Nawe umlete Haruni ndugu yako karibu nami, na wanawe pamoja naye, miongoni mwa wana wa Israeli, ili anitumikie katika kazi ya ukuhani. Haruni, na Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari, wana wa Haruni. Kutoka 28:1

"Bring Aaron your brother, and his sons with him, near to you from among the children of Israel, that he may minister to me in the priest's office, even Aaron, Nadab and Abihu, Eleazar and Ithamar, Aaron's sons.

Nawe utamfanyia Haruni ndugu yako mavazi matakatifu, kwa utukufu na kwa uzuri. Kutoka 28:2

You shall make holy garments for Aaron your brother, for glory and for beauty.

Nawe utawaambia watu wote wenye moyo wa hekima, niliowajaza na roho ya hekima wamfanyie Haruni mavazi ili kumtakasa anitumikie katika kazi ya ukuhani. Kutoka 28:3

You shall speak to all who are wise-hearted, whom I have filled with the spirit of wisdom, that they make Aaron's garments to sanctify him, that he may minister to me in the priest's office.

Na mavazi watakayoyafanya ni haya; kifuko cha kifuani, na naivera, na joho, na kanzu ya kazi ya urembo; na kilemba, na mshipi; nao watawafanyia Haruni nduguyo, na wanawe, mavazi matakatifu ili anitumikie katika kazi ya ukuhani. Kutoka 28:4

These are the garments which they shall make: a breastplate, and an ephod, and a robe, and a coat of checker work, a turban, and a sash: and they shall make holy garments for Aaron your brother, and his sons, that he may minister to me in the priest's office.

Nao wataitwaa dhahabu, na nguo ya rangi ya samawi, na ya rangi ya zambarau, na ya rangi nyekundu, na nguo ya kitani nzuri. Kutoka 28:5

They shall take the gold, and the blue, and the purple, and the scarlet, and the fine linen.

Nao waifanye naivera kwa nyuzi za dhahabu, na za samawi, na za zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa kwa kazi ya mstadi. Kutoka 28:6

"They shall make the ephod of gold, of blue, and purple, scarlet, and fine twined linen, the work of the skillful workman.

Itakuwa na vipande viwili vya mabegani, vilivyoungana kwenye ncha zake mbili; ili ipate kuunganywa. Kutoka 28:7

It shall have two shoulder-pieces joined to the two ends of it, that it may be joined together.

Na mshipi wa kazi ya ustadi ulio juu yake, ili kuifunga mahali pake; utakuwa wa kazi kama ile ya naivera, ya vitu vile vile ya nyuzi za dhahabu, na za rangi ya samawi, na ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa. Kutoka 28:8

The skillfully woven band, which is on it, that is on him, shall be like its work and of the same piece; of gold, of blue, and purple, and scarlet, and fine twined linen.

Nawe utatwaa vito viwili vya shohamu, ya rangi ya chani-kiwiti, nawe utachora juu yake majina ya wana wa Israeli; Kutoka 28:9

You shall take two onyx stones, and engrave on them the names of the children of Israel:

majina yao sita katika kito kimoja, na majina sita yaliyosalia katika kile kito cha pili, kwa utaratibu wa kuzaliwa kwao. Kutoka 28:10

six of their names on the one stone, and the names of the six that remain on the other stone, in the order of their birth.

Kwa kazi mtu mwenye kuchora mawe kama vile muhuri ichorwavyo, utavichora hivi vito viwili, sawasawa na majina ya wana wa Israeli, nawe utavitia katika vijalizo vya dhahabu. Kutoka 28:11

With the work of an engraver in stone, like the engravings of a signet, shall you engrave the two stones, according to the names of the children of Israel: you shall make them to be enclosed in settings of gold.

Nawe utavitia vile vito viwili juu ya vipande vya mabegani vya hiyo naivera, viwe vito vya ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli; naye Haruni atayachukua majina yao mbele za Bwana juu ya mabega yake mawili ili kuwa ukumbusho. Kutoka 28:12

You shall put the two stones on the shoulder-pieces of the ephod, to be stones of memorial for the children of Israel: and Aaron shall bear their names before Yahweh on his two shoulders for a memorial.

Nawe fanya vijalizo viwili vya dhahabu; Kutoka 28:13

You shall make settings of gold,

na mikufu miwili ya dhahabu safi; utaifanya iwe mfano wa kamba, ya kazi ya kusokotwa; nawe uitie ile mikufu ya kazi ya kusokotwa katika vile vijalizo. Kutoka 28:14

and two chains of pure gold; you make them like cords shall, of braided work: and you shall put the braided chains on the settings.

Nawe utafanya kifuko cha kifuani cha hukumu, kazi ya fundi stadi; utakifanya kwa kuiandama ile kazi ya hiyo naivera; ya nyuzi za dhahabu, na za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani safi yenye kusokotwa, ndivyo utakavyokifanya. Kutoka 28:15

"You shall make a breastplate of judgment, the work of the skillful workman; like the work of the ephod you shall make it; of gold, of blue, and purple, and scarlet, and fine twined linen, shall you make it.

Kitakuwa mraba, tena cha kukunjwa; urefu wake utakuwa shibiri moja, na upana wake shibiri moja. Kutoka 28:16

It shall be square and folded double; a span{A span is the length from the tip of the thumb to the tip of the little finger when the hand is stretched out (about 9 inches or 22.8 cm.)} shall be its length of it, and a span its breadth.

Nawe ukijaze viweko vya vito, safu nne za vito; safu moja itakuwa ni akiki, na yakuti ya rangi ya manjano, na baharamani, hivi vitakuwa safu ya kwanza; Kutoka 28:17

You shall set in it settings of stones, four rows of stones: a row of ruby, topaz, and beryl shall be the first row;

na safu ya pili itakuwa zumaridi, na yakuti samawi, na almasi; Kutoka 28:18

and the second row a turquoise, a sapphire{or, lapis lazuli}, and an emerald;

na safu ya tatu itakuwa hiakintho, na akiki nyekundu, na amethisto; Kutoka 28:19

and the third row a jacinth, an agate, and an amethyst;

na safu ya nne itakuwa ni zabarajadi, na shohamu, na yaspi; vito hivyo vitakazwa ndani ya dhahabu kwa kujaa mahali pake. Kutoka 28:20

and the fourth row a chrysolite, an onyx, and a jasper: they shall be enclosed in gold in their settings.

Na vile vito vitakuwa sawasawa na majina ya wana wa Israeli, kumi na viwili, sawasawa na majina yao; mfano wa kuchora kwa muhuri kila kimoja sawasawa na jina lake, vitakuwa vya hizo kabila kumi na mbili. Kutoka 28:21

The stones shall be according to the names of the children of Israel, twelve, according to their names; like the engravings of a signet, everyone according to his name, they shall be for the twelve tribes.

Nawe utie katika kile kifuko cha kifuani mikufu mfano wa kamba, ya kazi ya kusokotwa, ya dhahabu safi. Kutoka 28:22

You shall make on the breastplate chains like cords, of braided work of pure gold.

Nawe utie pete mbili za dhahabu katika kile kifuko cha kifuani, na kuzitia hizo pete mbili katika ncha mbili za kifuko cha kifuani. Kutoka 28:23

You shall make on the breastplate two rings of gold, and shall put the two rings on the two ends of the breastplate.

Nawe utie hiyo mikufu miwili ya dhahabu iliyosokotwa katika zile pete mbili zilizo katika ncha za kifuko cha kifuani. Kutoka 28:24

You shall put the two braided chains of gold in the two rings at the ends of the breastplate.

Na ncha zile nyingine za hiyo mikufu miwili ya kusokotwa utazitia katika vile vijalizo viwili, na kuvitia katika vile vipande vya mabegani vya naivera upande wa mbele. Kutoka 28:25

The other two ends of the two braided chains you shall put on the two settings, and put them on the shoulder-pieces of the ephod in the forepart of it.

Nawe utafanya pete mbili za dhahabu, uzitie katika hizo ncha mbili za kifuko cha kifuani, katika ukingo wake, ulio upande wa naivera ulio ndani. Kutoka 28:26

You shall make two rings of gold, and you shall put them on the two ends of the breastplate, on its edge, which is toward the side of the ephod inward.

Nawe fanya pete mbili za dhahabu, na kuzitia katika vile vipande viwili vya mabegani vya ile naivera chini yake, upande wa mbele, karibu na kifungo chake, juu ya huo mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi. Kutoka 28:27

You shall make two rings of gold, and shall put them on the two shoulder-pieces of the ephod underneath, in the forepart of it, close by the coupling of it, above the skillfully woven band of the ephod.

Nao watakikaza kile kileso kwa zile pete zake kwenye pete za naivera kwa ukanda wa rangi ya samawi, ili kwamba kikae pale juu ya ule mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi, ili kwamba kifuko cha kifuani kisiachane na naivera. Kutoka 28:28

They shall bind the breastplate by the rings of it to the rings of the ephod with a lace of blue, that it may be on the skillfully woven band of the ephod, and that the breastplate may not swing out from the ephod.

Na Haruni atayachukua majina ya wana wa Israeli katika kile kifuko cha kifuani cha hukumu juu ya moyo wake, hapo atakapoingia ndani ya mahali patakatifu, kuwa ukumbusho mbele ya Bwana daima. Kutoka 28:29

Aaron shall bear the names of the children of Israel in the breastplate of judgment on his heart, when he goes in to the holy place, for a memorial before Yahweh continually.

Nawe utie hizo Urimu na Thumimu katika kile kifuko cha kifuani cha hukumu; nazo zitakuwa juu ya moyo wa Haruni, hapo atakapoingia ndani mbele ya Bwana; na Haruni atachukua hukumu ya hao wana wa Israeli juu ya moyo wake mbele ya Bwana daima. Kutoka 28:30

You shall put in the breastplate of judgment the Urim and the Thummim; and they shall be on Aaron's heart, when he goes in before Yahweh: and Aaron shall bear the judgment of the children of Israel on his heart before Yahweh continually.

Nawe fanya hiyo joho ya naivera ya rangi ya samawi yote. Kutoka 28:31

"You shall make the robe of the ephod all of blue.

Nayo itakuwa na tundu katikati yake kwa kupitisha kichwa; itakuwa na utepe wa kazi ya kusokotwa kuzunguka hilo tundu lake, mfano wa tundu lililo katika kanzu ya chuma, ili lisipasuke. Kutoka 28:32

It shall have a hole for the head in the midst of it: it shall have a binding of woven work round about the hole of it, as it were the hole of a coat of mail, that it not be torn.

Nawe katika pindo zake utatia makomamanga ya rangi ya samawi, na ya rangi ya zambarau, na ya rangi nyekundu, kuzunguka pindo zake kotekote; na njuga za dhahabu kati ya hayo makomamanga pande zote; Kutoka 28:33

On its hem you shall make pomegranates of blue, and of purple, and of scarlet, around its hem; and bells of gold between them round about:

njuga ya dhahabu na komamanga, njuga ya dhahabu na komamanga, katika pindo za joho kuizunguka pande zote. Kutoka 28:34

a golden bell and a pomegranate, a golden bell and a pomegranate, on the hem of the robe round about.

Nayo itakuwa juu ya Haruni akitumika; na sauti ya hizo njuga itasikilikana hapo aingiapo ndani ya mahali patakatifu mbele ya Bwana na hapo atokapo nje, ili kwamba asife. Kutoka 28:35

It shall be on Aaron to minister: and the sound of it shall be heard when he goes in to the holy place before Yahweh, and when he comes out, that he not die.

Nawe fanya bamba la dhahabu safi na kuchora juu yake, mfano wa machoro ya muhuri, MTAKATIFU KWA Bwana. Kutoka 28:36

"You shall make a plate of pure gold, and engrave on it, like the engravings of a signet, 'HOLY TO YAHWEH.'

Nawe ulitie hilo bamba katika ukanda wa rangi ya samawi, nalo litakuwa katika kile kilemba; litakuwa upande wa mbele wa kile kilemba. Kutoka 28:37

You shall put it on a lace of blue, and it shall be on the sash; on the front of the sash it shall be.

Nalo litakuwa katika kipaji cha uso cha Haruni, na Haruni atauchukua uovu wa vile vitu vitakatifu, watakavyovitakasa hao wana wa Israeli katika vipawa vyao vyote vitakatifu, nalo litakuwa katika kipaji chake cha uso sikuzote, ili kwamba vipate kukubaliwa mbele za Bwana. Kutoka 28:38

It shall be on Aaron's forehead, and Aaron shall bear the iniquity of the holy things, which the children of Israel shall make holy in all their holy gifts; and it shall be always on his forehead, that they may be accepted before Yahweh.

Na hiyo kanzu utaifuma ya kitani nzuri ya kazi ya urembo, ufanye na kilemba cha nguo ya kitani nzuri, nawe utafanya mshipi wa kazi ya mwenye kutia taraza. Kutoka 28:39

You shall weave the coat in checker work of fine linen, and you shall make a turban of fine linen, and you shall make a sash, the work of the embroiderer.

Kisha utafanya kanzu kwa ajili ya wana wa Haruni, nawe wafanyie mishipi, wafanyie na kofia kwa utukufu na uzuri. Kutoka 28:40

"You shall make coats for Aaron's sons, and you shall make sashes for them and headbands shall you make for them, for glory and for beauty.

Nawe mvike huyo nduguyo Haruni na wanawe nao mavazi hayo; nawe watie mafuta, na kuwaweka kwa kazi takatifu, na kuwatakasa, ili wapate kunitumikia mimi katika kazi ya ukuhani. Kutoka 28:41

You shall put them on Aaron your brother, and on his sons with him, and shall anoint them, and consecrate them, and sanctify them, that they may minister to me in the priest's office.

Nawe wafanyie suruali za nguo ya kitani, ili kufunika tupu ya miili yao; suruali hizo zitafika tangu kiunoni hata mapajani; Kutoka 28:42

You shall make them linen breeches to cover the flesh of their nakedness; from the loins even to the thighs they shall reach:

na Haruni na wanawe watazivaa, hapo watakapoingia katika hema ya kukutania, au hapo watakapoikaribia madhabahu ili watumike katika mahali patakatifu; wasije wakachukua uovu, wakafa; hii itakuwa ni amri ya milele kwake yeye, na kwa wazao wake.

Kutoka 28:43

They shall be on Aaron, and on his sons, when they go in to the tent of meeting, or when they come near to the altar to minister in the holy place; that they don't bear iniquity, and die: it shall be a statute forever to him and to his descendants after him.