Kutoka 11 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kutoka 11 (Swahili) Exodus 11 (English)

Bwana akamwambia Musa, Liko pigo moja bado, nitakaloleta juu ya Farao na juu ya Misri; baadaye atawapa ninyi ruhusa mtoke huku; naye hapo atakapowapa ruhusa, atawafukuza mtoke huku kabisa kabisa. Kutoka 11:1

Yahweh said to Moses, "Yet one plague more will I bring on Pharaoh, and on Egypt; afterwards he will let you go. When he lets you go, he will surely thrust you out altogether.

Basi nena wewe masikioni mwa watu hawa, na kila mtu mume na atake kwa jirani yake, na kila mwanamke atake kwa jirani yake, vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu. Kutoka 11:2

Speak now in the ears of the people, and let them ask every man of his neighbor, and every woman of her neighbor, jewels of silver, and jewels of gold."

Bwana akawapa watu hao kibali machoni pa Wamisri. Zaidi ya hayo, huyo Musa alikuwa ni mkuu sana katika nchi ya Misri, machoni pa watumishi wa Farao, na machoni pa watu wake. Kutoka 11:3

Yahweh gave the people favor in the sight of the Egyptians. Moreover the man Moses was very great in the land of Egypt, in the sight of Pharaoh's servants, and in the sight of the people.

Musa akasema, Bwana asema hivi, Kama usiku wa manane mimi nitatoka nipite kati ya Misri; Kutoka 11:4

Moses said, "This is what Yahweh says: 'About midnight I will go out into the midst of Egypt,

na wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri watakufa, tangu yule mzaliwa wa kwanza wa Farao aketiye katika kiti chake cha enzi, hata mzaliwa wa kwanza wa huyo kijakazi aliye pale nyuma ya jiwe la kusagia; na wazaliwa wa kwanza wote wa wanyama. Kutoka 11:5

and all the firstborn in the land of Egypt shall die, from the firstborn of Pharaoh who sits on his throne, even to the firstborn of the maid-servant who is behind the mill; and all the firstborn of cattle.

Ndipo kutakuwa na kilio kikuu katika nchi yote ya Misri, ambacho mfano wake haujakuwa bado majira yo yote, wala hautakuwako mfano wake tena kabisa. Kutoka 11:6

There shall be a great cry throughout all the land of Egypt, such as there has not been, nor shall be any more.

Lakini katika wana wa Israeli hapana hata mbwa atakayetoa ulimi juu yao, juu ya mtu wala juu ya mnyama; ili kwamba mpate kujua jinsi Bwana anavyowatenga Wamisri na Waisraeli. Kutoka 11:7

But against any of the children of Israel a dog won't even bark or move its tongue, against man or animal; that you may know that Yahweh makes a distinction between the Egyptians and Israel.

Tena hao watumishi wako wote watanitelemkia kwangu mimi, nao watanisujudia, wakisema, Toka wewe, na hawa watu wote wakufuatao; na baada ya hayo nitatoka. Basi akatoka kwa Farao na hasira kuu. Kutoka 11:8

All these your servants shall come down to me, and bow down themselves to me, saying, 'Get out, and all the people who follow you; and after that I will go out.'" He went out from Pharaoh in hot anger.

Bwana akamwambia Musa, Farao hatawasikiza ninyi; kusudi ajabu zangu ziongezeke katika nchi ya Misri. Kutoka 11:9

Yahweh said to Moses, "Pharaoh won't listen to you, that my wonders may be multiplied in the land of Egypt."

Musa na Haruni walifanya ajabu hizo zote mbele ya Farao; Bwana akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, asiwape wana wa Israeli ruhusa watoke nchi yake.

Kutoka 11:10

Moses and Aaron did all these wonders before Pharaoh, and Yahweh hardened Pharaoh's heart, and he didn't let the children of Israel go out of his land.