Ayabu 19 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ayabu 19 (Swahili) Job 19 (English)

Ndipo Ayubu akajibu, na kusema, Ayabu 19:1

Then Job answered,

Je! Mtanichukiza nafsi yangu hata lini, Na kunivunja-vunja kwa maneno? Ayabu 19:2

"How long will you torment me, And crush me with words?

Mara kumi hizi mmenishutumu; Hamwoni haya kunifanyia mambo magumu. Ayabu 19:3

You have reproached me ten times. You aren't ashamed that you attack me.

Ingawaje nimekosa, Kosa langu hukaa kwangu mwenyewe. Ayabu 19:4

If it is true that I have erred, My error remains with myself.

Kwamba mtajitukuza juu yangu, Na kunena juu yangu shutumu langu; Ayabu 19:5

If indeed you will magnify yourselves against me, And plead against me my reproach;

Jueni basi kuwa Mungu amenipotosha, Na kunizingira kwa wavu wake. Ayabu 19:6

Know now that God has subverted me, And has surrounded me with his net.

Tazama, nalia, Udhalimu, lakini sisikiwi; Naulilia msaada, wala hapana hukumu. Ayabu 19:7

"Behold, I cry out of wrong, but I am not heard: I cry for help, but there is no justice.

Yeye ameiziba njia yangu nisipate kupita, Na kutia giza katika mapito yangu. Ayabu 19:8

He has walled up my way so that I can't pass, And has set darkness in my paths.

Amenivua utukufu wangu, Na kuiondoa taji kichwani mwangu. Ayabu 19:9

He has stripped me of my glory, And taken the crown from my head.

Amenibomoa pande zote, nami nimetoweka; Na tumaini langu ameling'oa kama mti. Ayabu 19:10

He has broken me down on every side, and I am gone. My hope he has plucked up like a tree.

Tena ameziwasha ghadhabu zake juu yangu, Akanihesabia kuwa mmoja katika watesi wake. Ayabu 19:11

He has also kindled his wrath against me. He counts me among his adversaries.

Majeshi yake husongea pamoja, na kunipandishia njia yao, Na kupiga marago kuizunguka hema yangu. Ayabu 19:12

His troops come on together, Build a siege ramp against me, And encamp around my tent.

Amewaweka ndugu zangu mbali nami, Na wanijuao wametengwa nami kabisa. Ayabu 19:13

"He has put my brothers far from me. My acquaintances are wholly estranged from me.

Watu wa mbari yangu wamekoma, Na rafiki zangu niwapendao wamenisahau. Ayabu 19:14

My relatives have gone away. My familiar friends have forgotten me.

Wakaao nyumbani mwangu, na vijakazi vyangu, wanihesabu kuwa mgeni; Mimi ni mgeni machoni pao. Ayabu 19:15

Those who dwell in my house, and my maids, count me for a stranger. I am an alien in their sight.

Namwita mtumishi wangu, wala haniitikii, Ingawa namsihi kwa kinywa changu. Ayabu 19:16

I call to my servant, and he gives me no answer; I beg him with my mouth.

Pumzi zangu ni kama za mgeni kwa mke wangu, Nami ni machukizo kwa ndugu zangu. Ayabu 19:17

My breath is offensive to my wife. I am loathsome to the children of my own mother.

Hata watoto wadogo hunidharau; Nikiondoka, huninena. Ayabu 19:18

Even young children despise me. If I arise, they speak against me.

Wasiri wangu wote wanichukia; Na hao niliowapenda wamenigeukia. Ayabu 19:19

All my familiar friends abhor me. They whom I loved have turned against me.

Mfupa wangu unagandamana na ngozi yangu na nyama yangu, Nami nimeokoka na ngozi ya meno yangu tu. Ayabu 19:20

My bones stick to my skin and to my flesh. I have escaped by the skin of my teeth.

Nihurumieni, nihurumieni, enyi rafiki zangu, Kwa maana mkono wa Mungu umenigusa. Ayabu 19:21

"Have pity on me, have pity on me, you my friends; For the hand of God has touched me.

Mbona ninyi mnaniudhi kama Mungu, Wala hamkutosheka na nyama yangu? Ayabu 19:22

Why do you persecute me as God, And are not satisfied with my flesh?

Laiti maneno yangu yangeandikwa sasa! Laiti yangeandikwa kitabuni! Ayabu 19:23

"Oh that my words were now written! Oh that they were inscribed in a book!

Yakachorwa katika mwamba milele, Kwa kalamu ya chuma na risasi. Ayabu 19:24

That with an iron pen and lead They were engraved in the rock forever!

Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi. Ayabu 19:25

But as for me, I know that my Redeemer lives. In the end, he will stand upon the earth.

Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi, Lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu; Ayabu 19:26

After my skin is destroyed, Then in my flesh shall I see God,

Nami nitamwona mimi nafsi yangu, Na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine. Mtima wangu unazimia ndani yangu. Ayabu 19:27

Whom I, even I, shall see on my side. My eyes shall see, and not as a stranger. "My heart is consumed within me.

Kama mkisema, Jinsi tutakavyomwudhi! Kwa kuwa shina la jambo hili limeonekana kwake; Ayabu 19:28

If you say, 'How we will persecute him!' Because the root of the matter is found in me,

Uogopeni upanga; Kwa maana adhabu za upanga zina ghadhabu, Mpate kujua ya kwamba hukumu iko. Ayabu 19:29

Be afraid of the sword, For wrath brings the punishments of the sword, That you may know there is a judgment."