2 Samweli 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Samweli 2 (Swahili) 2nd Samuel 2 (English)

Ikawa baada ya hayo, Daudi akauliza kwa Bwana, akasema, Je! Niupandie mji wo wote wa Yuda? Bwana akamwambia, Haya! Panda. Daudi akasema, Niupandie mji upi? Akasema, Hebroni. 2 Samweli 2:1

It happened after this, that David inquired of Yahweh, saying, Shall I go up into any of the cities of Judah? Yahweh said to him, Go up. David said, Where shall I go up? He said, To Hebron.

Basi Daudi akapanda aende huko, pamoja na wakeze wawili, Ahinoamu wa Yezreeli, na Abigaili, mkewe Nabali, wa Karmeli. 2 Samweli 2:2

So David went up there, and his two wives also, Ahinoam the Jezreelitess, and Abigail the wife of Nabal the Carmelite.

Daudi naye akawapandisha watu wake waliokuwa pamoja naye, kila mtu na watu wa nyumbani mwake; wakakaa katika miji ya Hebroni. 2 Samweli 2:3

His men who were with him did David bring up, every man with his household: and they lived in the cities of Hebron.

Basi watu wa Yuda wakaenda, wakamtia Daudi mafuta huko, awe mfalme juu ya nyumba ya Yuda. Wakamwambia Daudi wakasema, Watu wa Yabesh-gileadi ndio waliomzika Sauli. 2 Samweli 2:4

The men of Judah came, and there they anointed David king over the house of Judah. They told David, saying, The men of Jabesh Gilead were those who buried Saul.

Basi Daudi akatuma wajumbe kwa watu wa Yabesh-gileadi, na kuwaambia, Na mbarikiwe ninyi na Bwana, kwa kuwa mmemtendea bwana wenu fadhili hii, yaani Sauli, mkamzika. 2 Samweli 2:5

David sent messengers to the men of Jabesh Gilead, and said to them, Blessed be you of Yahweh, that you have shown this kindness to your lord, even to Saul, and have buried him.

Bwana naye sasa awatendee ninyi fadhili na kweli; mimi nami nitawalipeni fadhili hiyo, kwa sababu mmetenda jambo hilo. 2 Samweli 2:6

Now Yahweh show loving kindness and truth to you: and I also will requite you this kindness, because you have done this thing.

Basi sasa, mikono yenu na itiwe nguvu, nanyi iweni mashujaa; maana Sauli, bwana wenu, amekufa, tena nyumba ya Yuda wamenitia mimi mafuta niwe mfalme juu yao. 2 Samweli 2:7

Now therefore let your hands be strong, and be you valiant; for Saul your lord is dead, and also the house of Judah have anointed me king over them.

Basi Abneri, mwana wa Neri, amiri wa jeshi la Sauli, alikuwa amemtwaa Ishboshethi, mwana wa Sauli, na kumvusha na kumpeleka Mahanaimu; 2 Samweli 2:8

Now Abner the son of Ner, captain of Saul's host, had taken Ish-bosheth the son of Saul, and brought him over to Mahanaim;

akamweka awe mfalme juu ya Gileadi, na Waasheri, na Yezreeli, na Efraimu, na Benyamini, na juu ya Israeli wote. 2 Samweli 2:9

and he made him king over Gilead, and over the Ashurites, and over Jezreel, and over Ephraim, and over Benjamin, and over all Israel.

(Huyo Ishboshethi, mwana wa Sauli, umri wake alikuwa amepata miaka arobaini alipoanza kutawala juu ya Israeli, akatawala miaka miwili.) Lakini nyumba ya Yuda waliandamana na Daudi. 2 Samweli 2:10

Ish-bosheth, Saul's son, was forty years old when he began to reign over Israel, and he reigned two years. But the house of Judah followed David.

Na wakati Daudi alipotawala Hebroni juu ya nyumba ya Yuda ulikuwa miaka saba na miezi sita. 2 Samweli 2:11

The time that David was king in Hebron over the house of Judah was seven years and six months.

Basi Abneri, mwana wa Neri, na watumishi wa Ishboshethi, mwana wa Sauli, wakatoka Mahanaimu kwenda Gibeoni. 2 Samweli 2:12

Abner the son of Ner, and the servants of Ish-bosheth the son of Saul, went out from Mahanaim to Gibeon.

Huyo Yoabu naye, mwana wa Seruya, na watumishi wa Daudi, wakatoka, wakakutana nao karibu na ziwa la Gibeoni; wakaketi, hawa upande huu wa ziwa, na hawa upande huu wa ziwa. 2 Samweli 2:13

Joab the son of Zeruiah, and the servants of David, went out, and met them by the pool of Gibeon; and they sat down, the one on the one side of the pool, and the other on the other side of the pool.

Abneri akamwambia Yoabu, Tafadhali vijana hawa na waondoke na kucheza mbele yetu. Yoabu akasema, Haya! Na waondoke. 2 Samweli 2:14

Abner said to Joab, Please let the young men arise and play before us. Joab said, Let them arise.

Basi wakaondoka, wakaenda upande wa pili kwa hesabu yao watu kumi na wawili wa Benyamini, na wa Ishboshethi, mwana wa Sauli na watu kumi na wawili wa watumishi wa Daudi. 2 Samweli 2:15

Then they arose and went over by number: twelve for Benjamin, and for Ish-bosheth the son of Saul, and twelve of the servants of David.

Wakakamatana, kila mtu akimshika mwenziwe kichwa chake, na kutia upanga wake katika ubavu wa mwenzake; wakaanguka pamoja; hata mahali pale pakaitwa Helkath-hasurimu, napo ni katika Gibeoni. 2 Samweli 2:16

They caught everyone his fellow by the head, and [thrust] his sword in his fellow's side; so they fell down together: therefore that place was called Helkath Hazzurim, which is in Gibeon.

Vita vile vilikuwa vikali sana siku ile; naye Abneri akashindwa, na watu wa Israeli, mbele ya watumishi wa Daudi. 2 Samweli 2:17

The battle was very severe that day: and Abner was beaten, and the men of Israel, before the servants of David.

Na wana watatu wa Seruya walikuwako huko, Yoabu, na Abishai, na Asaheli; na Asaheli alikuwa mwepesi wa miguu kama kulungu. 2 Samweli 2:18

The three sons of Zeruiah were there, Joab, and Abishai, and Asahel: and Asahel was as light of foot as a wild gazelle.

Naye Asaheli akamfuatia Abneri; na katika kwenda kwake hakugeuka kwenda mkono wa kuume wala mkono wa kushoto katika kumfuatia Abneri. 2 Samweli 2:19

Asahel pursued after Abner; and in going he didn't turn to the right hand nor to the left from following Abner.

Basi Abneri akatazama nyuma yake, akasema, Ni wewe, Asaheli? Akajibu, Ni mimi. 2 Samweli 2:20

Then Abner looked behind him, and said, Is it you, Asahel? He answered, It is I.

Basi Abneri akamwambia, Geuka mkono wa kuume au mkono wa kushoto, ukamshike mmoja wa vijana, ukazitwae silaha zake. Lakini Asaheli hakukubali kugeuka na kuacha kumfuata. 2 Samweli 2:21

Abner said to him, Turn you aside to your right hand or to your left, and lay you hold on one of the young men, and take you his armor. But Asahel would not turn aside from following him.

Abneri akamwambia Asaheli mara ya pili, Geuka, acha kunifuatia mimi; kwa nini nikupige hata chini? Hapo ningewezaje kuinua uso wangu mbele ya Yoabu, ndugu yako? 2 Samweli 2:22

Abner said again to Asahel, Turn you aside from following me: why should I strike you to the ground? how then should I hold up my face to Joab your brother?

Lakini akakataa kugeuka; kwa hiyo Abneri akampiga tumboni kwa ncha ya nyuma ya mkuki wake, ule mkuki ukamtoka kwa nyuma; naye akaanguka hapo, akafa papo hapo; ikawa, watu wote waliofika hapo, alipoanguka Asaheli na kufa, wakasimama. 2 Samweli 2:23

However he refused to turn aside: therefore Abner with the hinder end of the spear struck him in the body, so that the spear came out behind him; and he fell down there, and died in the same place: and it happened, that as many as came to the place where Asahel fell down and died stood still.

Ila Yoabu na Abishai wakamfuatia Abneri; na jua likachwa hapo walipoufikilia mlima wa Ama, uelekeao Gia, katika njia ya nyika ya Gibeoni. 2 Samweli 2:24

But Joab and Abishai pursued after Abner: and the sun went down when they were come to the hill of Ammah, that lies before Giah by the way of the wilderness of Gibeon.

Nao wana wa Benyamini wakakusanyika pamoja nyuma ya Abneri, wakawa kikosi kimoja, wakasimama juu ya mlima. 2 Samweli 2:25

The children of Benjamin gathered themselves together after Abner, and became one band, and stood on the top of a hill.

Ndipo huyo Abneri akamwita Yoabu, akasema, Je! Upanga uwale watu sikuzote? Je! Hujui ya kwamba utakuwa uchungu mwisho wake? Basi itakuwa hata lini usijewaamuru watu warudi na kuacha kuwafuatia ndugu zao? 2 Samweli 2:26

Then Abner called to Joab, and said, "Shall the sword devour forever? Don't you know that it will be bitterness in the latter end? How long shall it be then, before you bid the people return from following their brothers?"

Naye Yoabu akasema, Aishivyo Mungu, usingalinena, basi asubuhi wangalikwenda zao, wasiwafuatie kila mtu ndugu yake. 2 Samweli 2:27

Joab said, As God lives, if you had not spoken, surely then in the morning the people had gone away, nor followed everyone his brother.

Basi Yoabu akapiga tarumbeta, na watu wote wakasimama, wasiwafuatie Israeli tena, wala hawakupigana tena. 2 Samweli 2:28

So Joab blew the trumpet; and all the people stood still, and pursued after Israel no more, neither fought they any more.

Wakaenda Abneri na watu wake usiku ule wote kati ya ile Araba; wakavuka Yordani, wakapita kati ya Bithroni yote, wakaja Mahanaimu. 2 Samweli 2:29

Abner and his men went all that night through the Arabah; and they passed over the Jordan, and went through all Bithron, and came to Mahanaim.

Akarudi Yoabu naye kutoka kumfuatia Abneri; na alipokwisha kuwakusanya watu wote pamoja, wa hao watumishi wa Daudi walipungukiwa na watu kumi na kenda pamoja na Asaheli. 2 Samweli 2:30

Joab returned from following Abner: and when he had gathered all the people together, there lacked of David's servants nineteen men and Asahel.

Ila watumishi wa Daudi walikuwa wamewapiga watu wa Benyamini, na watu wa Abneri, hata wakafa watu mia tatu na sitini. 2 Samweli 2:31

But the servants of David had struck of Benjamin, and of Abner's men, [so that] three hundred sixty men died.

Nao wakamwinua Asaheli, wakamzika katika kaburi la baba yake, lililokuwako Bethlehemu. Yoabu na watu wake wakaenda usiku kucha, wakapambazukiwa huko Hebroni. 2 Samweli 2:32

They took up Asahel, and buried him in the tomb of his father, which was in Bethlehem. Joab and his men went all night, and the day broke on them at Hebron.