2 Samweli 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Samweli 3 (Swahili) 2nd Samuel 3 (English)

Basi kulikuwa na vita siku nyingi kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi; Daudi akaendelea akasitawi, lakini nyumba ya Sauli ikaendelea kudhoofika. 2 Samweli 3:1

Now there was long war between the house of Saul and the house of David: and David grew stronger and stronger, but the house of Saul grew weaker and weaker.

Naye Daudi akazaliwa wana huko Hebroni; mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Amnoni, wa Ahinoamu wa Yezreeli; 2 Samweli 3:2

To David were sons born in Hebron: and his firstborn was Amnon, of Ahinoam the Jezreelitess;

na wa pili wake Danieli, wa Abigaili mkewe Nabali wa Karmeli; na wa tatu Absalomu, mwana wa Maaka binti Talmai, mfalme wa Geshuri, 2 Samweli 3:3

and his second, Chileab, of Abigail the wife of Nabal the Carmelite; and the third, Absalom the son of Maacah the daughter of Talmai king of Geshur;

na wa nne Adoniya, mwana wa Hagithi; na wa tano Shefatia, mwana wa Abitali; 2 Samweli 3:4

and the fourth, Adonijah the son of Haggith; and the fifth, Shephatiah the son of Abital;

na wa sita Ithreamu, wa Egla, mkewe Daudi. Hawa walizaliwa kwa Daudi huko Hebroni. 2 Samweli 3:5

and the sixth, Ithream, of Eglah, David's wife. These were born to David in Hebron.

Ikawa, wakati vilipokuwapo vita kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi, Abneri akajipatia nguvu nyumbani kwa Sauli. 2 Samweli 3:6

It happened, while there was war between the house of Saul and the house of David, that Abner made himself strong in the house of Saul.

Basi Sauli alikuwa na suria, jina lake akiitwa Rispa, binti Aya; Ishboshethi akamwuliza Abneri, Kwa nini umeingia kwa suria ya babangu? 2 Samweli 3:7

Now Saul had a concubine, whose name was Rizpah, the daughter of Aiah: and [Ish-bosheth] said to Abner, Why have you gone in to my father's concubine?

Basi Abneri akakasirika kwa maneno ya Ishboshethi, akasema, Je! Mimi ni kichwa cha mbwa, aliye wa Yuda? Hata leo hivi nawafanyia fadhili nyumba ya Sauli babako, na ndugu zake, na rafiki zake, nisikutie wewe mkononi mwa Daudi; nawe hata hivyo wanitia hatiani leo kwa mwanamke huyu. 2 Samweli 3:8

Then was Abner very angry for the words of Ish-bosheth, and said, Am I a dog's head that belongs to Judah? This day do I show kindness to the house of Saul your father, to his brothers, and to his friends, and have not delivered you into the hand of David; and yet you charge me this day with a fault concerning this woman.

Mungu amfanyie Abneri vivyo, na kuzidi, nisipomtendea Daudi kama vile Bwana alivyomwapia; 2 Samweli 3:9

God do so to Abner, and more also, if, as Yahweh has sworn to David, I don't do even so to him;

kuupitisha ufalme toka nyumba ya Sauli, na kukisimamisha kiti cha Daudi juu ya Israeli, na juu ya Yuda, toka Dani mpaka Beer-sheba. 2 Samweli 3:10

to transfer the kingdom from the house of Saul, and to set up the throne of David over Israel and over Judah, from Dan even to Beersheba.

Wala hakuweza kumjibu Abneri tena, kwa sababu alimwogopa. 2 Samweli 3:11

He could not answer Abner another word, because he feared him.

Basi Abneri akatuma wajumbe kwa Daudi mahali alipokuwapo, akisema, Nchi hii ni ya nani? Fanya agano nami, na tazama, mkono wangu utakuwa pamoja nawe, ili kuwaleta Israeli wote kwako. 2 Samweli 3:12

Abner sent messengers to David on his behalf, saying, Whose is the land? saying [also], Make your league with me, and, behold, my hand shall be with you, to bring about all Israel to you.

Daudi akasema, Vema, nitafanya agano nawe, lakini nina sharti moja nitakalo kwako, nalo ni hili; Hutaniona uso wangu, isipokuwa uniletee Mikali, binti Sauli, hapo ujapo kuniona uso wangu. 2 Samweli 3:13

He said, Well; I will make a league with you; but one thing I require of you: that is, you shall not see my face, except you first bring Michal, Saul's daughter, when you come to see my face.

Basi Daudi akatuma wajumbe kwa Ishboshethi, mwana wa Sauli, kusema, Nipe mke wangu Mikali, niliyemposa kwa govi mia za Wafilisti. 2 Samweli 3:14

David sent messengers to Ish-bosheth, Saul's son, saying, Deliver me my wife Michal, whom I pledged to be married to me for one hundred foreskins of the Philistines.

Basi Ishboshethi akatuma watu, akamnyang'anya Paltieli, mwana wa Laishi, mumewe, mwanamke huyo. 2 Samweli 3:15

Ish-bosheth sent, and took her from her husband, even from Paltiel the son of Laish.

Huyo mumewe akafuatana naye, akiendelea na kulia, akamfuata mpaka Bahurimu. Ndipo Abneri akamwambia, Haya, rudi. Naye akarudi. 2 Samweli 3:16

Her husband went with her, weeping as he went, and followed her to Bahurim. Then said Abner to him, Go, return: and he returned.

Basi Abneri akafanya mashauri na wazee wa Israeli, akasema, Zamani mlitaka Daudi awamiliki; 2 Samweli 3:17

Abner had communication with the elders of Israel, saying, In times past you sought for David to be king over you:

basi, sasa, fanyeni hayo; kwa maana Bwana amemtaja Daudi, akisema, kwa mkono wa mtumishi wangu, Daudi, nitawaokoa watu wangu Israeli katika mikono ya Wafilisti, na katika mikono ya adui zao wote. 2 Samweli 3:18

now then do it; for Yahweh has spoken of David, saying, By the hand of my servant David I will save my people Israel out of the hand of the Philistines, and out of the hand of all their enemies.

Tena Abneri alinena masikioni mwa Benyamini; kisha Abneri akaenda ili kunena masikioni mwa Daudi huko Hebroni maneno yote yaliyoonekana kuwa mema machoni pa Israeli, na machoni pa nyumba yote ya Benyamini. 2 Samweli 3:19

Abner also spoke in the ears of Benjamin: and Abner went also to speak in the ears of David in Hebron all that seemed good to Israel, and to the whole house of Benjamin.

Basi Abneri akamwendea Daudi huko Hebroni, na watu ishirini pamoja naye. Daudi akamfanyia karamu Abneri, na watu wote waliokuwa pamoja naye. 2 Samweli 3:20

So Abner came to David to Hebron, and twenty men with him. David made Abner and the men who were with him a feast.

Kisha Abneri akamwambia Daudi, Nitaondoka, niende zangu; nami nitamkusanyia bwana wangu mfalme Israeli wote, ili wafanye agano nawe, ukamiliki juu ya wote inaowatamani roho yako. Basi Daudi akamruhusu Abneri; naye akaenda zake kwa amani. 2 Samweli 3:21

Abner said to David, I will arise and go, and will gather all Israel to my lord the king, that they may make a covenant with you, and that you may reign over all that your soul desires. David sent Abner away; and he went in peace.

Na tazama, watumishi wa Daudi pamoja na Yoabu walitoka jeshini, wakaleta mateka mengi pamoja nao; lakini Abneri hakuwako Hebroni kwa Daudi; maana alikuwa amemruhusu, naye amekwisha kwenda zake kwa amani. 2 Samweli 3:22

Behold, the servants of David and Joab came from a foray, and brought in a great spoil with them: but Abner was not with David in Hebron; for he had sent him away, and he was gone in peace.

Hata Yoabu, na jeshi lote waliokuwa pamoja naye, walipofika, watu wakamwambia Yoabu, wakisema, Abneri, mwana wa Neri, alikuja kwa mfalme, naye amemruhusu, naye amekwenda zake kwa amani. 2 Samweli 3:23

When Joab and all the host who was with him had come, they told Joab, saying, Abner the son of Ner came to the king, and he has sent him away, and he is gone in peace.

Basi Yoabu akamwendea mfalme, akasema, Umefanyaje? Tazama, Abneri amekuja kwako; mbona umemruhusu, naye amekwisha kwenda zake? 2 Samweli 3:24

Then Joab came to the king, and said, What have you done? behold, Abner came to you; why is it that you have sent him away, and he is quite gone?

Wewe wamjua Abneri, mwana wa Neri, ya kuwa alikuja ili kukudanganya, apate kujua kutoka kwako, na kuingia kwako, akajue yote uyatendayo. 2 Samweli 3:25

You know Abner the son of Ner, that he came to deceive you, and to know your going out and your coming in, and to know all that you do.

Naye Yoabu alipotoka kwa Daudi, akapeleka wajumbe kumfuata Abneri, wakamrudisha kutoka kisima cha Sira; lakini Daudi alikuwa hana habari. 2 Samweli 3:26

When Joab was come out from David, he sent messengers after Abner, and they brought him back from the well of Sirah: but David didn't know it.

Basi Abneri alipokuwa amerudi Hebroni, Yoabu akamchukua kando hata katikati ya lango, ili aseme naye kwa faragha; akampiga mkuki wa tumbo huko, hata akafa; kwa ajili ya damu ya Asaheli, ndugu yake. 2 Samweli 3:27

When Abner was returned to Hebron, Joab took him aside into the midst of the gate to speak with him quietly, and struck him there in the body, so that he died, for the blood of Asahel his brother.

Hata baadaye Daudi aliposikia, akasema, Mimi na ufalme wangu hatuna hatia milele mbele za Bwana, kwa sababu ya damu ya Abneri, mwana wa Neri; 2 Samweli 3:28

Afterward, when David heard it, he said, I and my kingdom are guiltless before Yahweh forever of the blood of Abner the son of Ner:

na imwangukie Yoabu kichwani pake, na nyumba yote ya babaye, tena hiyo nyumba ya Yoabu isikose kuwa na mtu mwenye kutoka damu, au aliye na ukoma, au mwenye kutegemea fimbo, au mwenye kuanguka kwa upanga au mwenye kuhitaji chakula. 2 Samweli 3:29

let it fall on the head of Joab, and on all his father's house; and let there not fail from the house of Joab one who has an issue, or who is a leper, or who leans on a staff, or who falls by the sword, or who lacks bread.

Basi Yoabu, na Abishai nduguye, walimwua Abneri, kwa sababu yeye alimwua ndugu yao Asaheli katika vita huko Gibeoni. 2 Samweli 3:30

So Joab and Abishai his brother killed Abner, because he had killed their brother Asahel at Gibeon in the battle.

Kisha Daudi alimwambia Yoabu, na watu wote waliokuwa pamoja naye, Rarueni nguo zenu, mkajivike nguo za magunia, mkamlilie Abneri. Naye mfalme Daudi akaifuata jeneza. 2 Samweli 3:31

David said to Joab, and to all the people who were with him, Tear your clothes, and gird you with sackcloth, and mourn before Abner. King David followed the bier.

Wakamzika Abneri katika Hebroni; naye mfalme akapaza sauti yake, akalia kaburini kwa Abneri, nao watu wote wakalia. 2 Samweli 3:32

They buried Abner in Hebron: and the king lifted up his voice, and wept at the grave of Abner; and all the people wept.

Ndipo mfalme akamwomboleza Abneri, akasema, Ilimpasaje Abneri kufa afavyo mpumbavu? 2 Samweli 3:33

The king lamented for Abner, and said, Should Abner die as a fool dies?

Mikono yako haikufungwa, Wala miguu yako haikutiwa pingu; Aangukavyo mtu mbele ya wana wa uovu, ndivyo ulivyoanguka. Na watu wote wakaongeza kumlilia. 2 Samweli 3:34

Your hands were not bound, nor your feet put into fetters: As a man falls before the children of iniquity, so did you fall. All the people wept again over him.

Wakaja na watu wote wamshurutishe Daudi kula chakula, ukalipo bado mchana; lakini Daudi akaapa, akasema Mungu anitendee vivyo, na kuzidi, nikionja mkate, au kingine cho chote kabla lichwapo jua. 2 Samweli 3:35

All the people came to cause David to eat bread while it was yet day; but David swore, saying, God do so to me, and more also, if I taste bread, or anything else, until the sun be down.

Wakaangalia watu wote, yakawa mema machoni pao; kama yalivyokuwa mema machoni pao yote aliyoyatenda mfalme. 2 Samweli 3:36

All the people took notice of it, and it pleased them; as whatever the king did pleased all the people.

Wakajua watu wote, na Israeli wote, siku ile, ya kuwa si nia ya mfalme kwamba auawe Abneri, mwana wa Neri. 2 Samweli 3:37

So all the people and all Israel understood that day that it was not of the king to kill Abner the son of Ner.

Kisha mfalme akawaambia watumishi wake, Hamjui ya kuwa mkuu mmoja, naye ni mtu mkubwa ameanguka leo katika Israeli? 2 Samweli 3:38

The king said to his servants, "Don't you know that there a prince and a great man has fallen this day in Israel?

Nami leo nimedhoofika, hata nijapotiwa mafuta niwe mfalme; na watu hao, wana wa Seruya, ni wagumu kwangu mimi; Bwana amlipie mwovu sawasawa na uovu wake. 2 Samweli 3:39

I am this day weak, though anointed king; and these men the sons of Zeruiah are too hard for me. May Yahweh reward the evil-doer according to his wickedness."