2 Samweli 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Samweli 5 (Swahili) 2nd Samuel 5 (English)

Ndipo kabila zote za Israeli wakamwendea Daudi huko Hebroni, wakasema naye, wakinena, Tazama, sisi tu mfupa wako na nyama yako. 2 Samweli 5:1

Then came all the tribes of Israel to David to Hebron, and spoke, saying, Behold, we are your bone and your flesh.

Zamani za kale, hapo Sauli alipokuwa mfalme juu yetu, wewe ndiwe uliyewaongoza Israeli watoke nje, na kuingia ndani. Naye Bwana akakuambia, Wewe utawalisha watu wangu Israeli, nawe utakuwa mkuu juu ya Israeli. 2 Samweli 5:2

In times past, when Saul was king over us, it was you who led out and brought in Israel: and Yahweh said to you, You shall be shepherd of my people Israel, and you shall be prince over Israel.

Basi wazee wote wa Israeli wakamwendea mfalme huko Hebroni, naye mfalme Daudi akapatana nao huko Hebroni mbele za Bwana; wakamtia Daudi mafuta awe mfalme juu ya Israeli. 2 Samweli 5:3

So all the elders of Israel came to the king to Hebron; and king David made a covenant with them in Hebron before Yahweh: and they anointed David king over Israel.

Daudi alikuwa amepata miaka thelathini alipoanza kutawala, akatawala miaka arobaini. 2 Samweli 5:4

David was thirty years old when he began to reign, and he reigned forty years.

Huko Hebroni alitawala miaka saba na miezi sita; na katika Yerusalemu alitawala miaka thelathini na tatu juu ya Israeli wote na Yuda. 2 Samweli 5:5

In Hebron he reigned over Judah seven years and six months; and in Jerusalem he reigned thirty-three years over all Israel and Judah.

Kisha mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu ili kupigana na Wayebusi, wenyeji wa nchi ile; hao ndio waliomwambia Daudi, wakisema, Usipowaondoa vipofu, na viwete, hutaingia humu kamwe; huku wakidhania ya kuwa Daudi hawezi kuingia humo. 2 Samweli 5:6

The king and his men went to Jerusalem against the Jebusites, the inhabitants of the land, who spoke to David, saying, Except you take away the blind and the lame, you shall not come in here; thinking, David can't come in here.

Lakini Daudi aliipiga ngome ya Sayuni; huu ndio mji wa Daudi. 2 Samweli 5:7

Nevertheless David took the stronghold of Zion; the same is the city of David.

Naye Daudi alisema siku hiyo, Yeye atakayewapiga Wayebusi, na apande kwenye mfereji wa maji, na kuwapiga viwete, na hao vipofu, ambao roho yake Daudi inawachukia. Kwa sababu hii watu husema, Wako vipofu na viwete hawawezi kuingia nyumbani. 2 Samweli 5:8

David said on that day, Whoever strikes the Jebusites, let him get up to the watercourse, and [strike] the lame and the blind, who are hated of David's soul. Therefore they say, There are the blind and the lame; he can't come into the house.

Basi Daudi akakaa ndani ya ngome hiyo, akaiita mji wa Daudi. Kisha Daudi akajenga toka Milo na pande za ndani. 2 Samweli 5:9

David lived in the stronghold, and called it the city of David. David built round about from Millo and inward.

Naye Daudi akazidi kuwa mkuu; kwa maana Bwana, Mungu wa majeshi, alikuwa pamoja naye. 2 Samweli 5:10

David grew greater and greater; for Yahweh, the God of hosts, was with him.

Kisha Hiramu, mfalme wa Tiro, akatuma wajumbe kwa Daudi, akampelekea na mierezi, na maseremala, na waashi; nao wakamjengea Daudi nyumba. 2 Samweli 5:11

Hiram king of Tyre sent messengers to David, and cedar trees, and carpenters, and masons; and they built David a house.

Akajua Daudi ya kwamba Bwana amemweka imara awe mfalme juu ya Israeli, na ufalme wake ameutukuza kwa ajili ya watu wake, Israeli. 2 Samweli 5:12

David perceived that Yahweh had established him king over Israel, and that he had exalted his kingdom for his people Israel's sake.

Naye Daudi akazidi kujitwalia masuria na wake huko Yerusalemu baada ya kutoka Hebroni; wakazaliwa zaidi kwa Daudi wana na binti. 2 Samweli 5:13

David took him more concubines and wives out of Jerusalem, after he was come from Hebron; and there were yet sons and daughters born to David.

Na haya ndiyo majina ya hao waliozaliwa kwake huko Yerusalemu; Shamua, na Shobabu, na Nathani, na Sulemani, 2 Samweli 5:14

These are the names of those who were born to him in Jerusalem: Shammua, and Shobab, and Nathan, and Solomon,

na Ibhari, na Elishua; na Nefegi, na Yafia; 2 Samweli 5:15

and Ibhar, and Elishua, and Nepheg, and Japhia,

na Elishama, na Eliada, na Elifeleti. 2 Samweli 5:16

and Elishama, and Eliada, and Eliphelet.

Na hao Wafilisti waliposikia kwamba wamemtia Daudi mafuta ili awe mfalme juu ya Israeli, Wafilisti wote wakapanda kumtafuta Daudi; naye Daudi akapata habari, akashuka akaenda ngomeni. 2 Samweli 5:17

When the Philistines heard that they had anointed David king over Israel, all the Philistines went up to seek David; and David heard of it, and went down to the stronghold.

Basi Wafilisti walikuwa wamekuja na kujitawanya bondeni mwa Warefai. 2 Samweli 5:18

Now the Philistines had come and spread themselves in the valley of Rephaim.

Basi Daudi akauliza kwa Bwana, akisema, Je! Nipande juu ya Wafilisti? Utawatia mkononi mwangu? Naye Bwana akamwambia Daudi, Panda; kwa kuwa hakika nitawatia Wafilisti mikononi mwako. 2 Samweli 5:19

David inquired of Yahweh, saying, Shall I go up against the Philistines? will you deliver them into my hand? Yahweh said to David, Go up; for I will certainly deliver the Philistines into your hand.

Basi Daudi akaja Baal-perasimu, naye Daudi akawapiga huko; akasema, Bwana amewafurikia adui zangu mbele yangu, kama mafuriko ya maji. Basi akapaita mahali pale Baal-perasimu. 2 Samweli 5:20

David came to Baal Perazim, and David struck them there; and he said, Yahweh has broken my enemies before me, like the breach of waters. Therefore he called the name of that place Baal Perazim.

Nao wakaziacha sanamu zao huko, na Daudi na watu wake wakaziondolea mbali. 2 Samweli 5:21

They left their images there; and David and his men took them away.

Lakini wakapanda hao Wafilisti tena mara ya pili, wakajitawanya bondeni mwa Warefai. 2 Samweli 5:22

The Philistines came up yet again, and spread themselves in the valley of Rephaim.

Naye Daudi alipouliza kwa Bwana, alisema, Usipande; zunguka nyuma yao, ukawajie huko mbele ya miforsadi. 2 Samweli 5:23

When David inquired of Yahweh, he said, You shall not go up: make a circuit behind them, and come on them over against the mulberry trees.

Kisha itakuwa, hapo utakapoisikia sauti ya kwenda katika vilele vya miforsadi, ndipo nawe ujitahidi; kwa maana ndipo Bwana ametoka mbele yako awapige jeshi la Wafilisti. 2 Samweli 5:24

It shall be, when you hear the sound of marching in the tops of the mulberry trees, that then you shall bestir yourself; for then is Yahweh gone out before you to strike the host of the Philistines.

Ndivyo alivyotenda Daudi, vile vile kama Bwana alivyomwagiza; naye akawapiga Wafilisti toka Geba hata ujapo Gezeri.

2 Samweli 5:25

David did so, as Yahweh commanded him, and struck the Philistines from Geba until you come to Gezer.