2 Samweli 11 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Samweli 11 (Swahili) 2nd Samuel 11 (English)

Hata ikawa, mwanzo wa mwaka mpya, wakati watokapo wafalme kwenda vitani, Daudi akampeleka Yoabu, na watumishi wake pamoja naye, na Israeli wote; wakawaangamiza wana wa Amoni, wakauhusuru Raba. Lakini Daudi mwenyewe akakaa Yerusalemu. 2 Samweli 11:1

It happened, at the return of the year, at the time when kings go out [to battle], that David sent Joab, and his servants with him, and all Israel; and they destroyed the children of Ammon, and besieged Rabbah. But David stayed at Jerusalem.

Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho. 2 Samweli 11:2

It happened at evening, that David arose from off his bed, and walked on the roof of the king's house: and from the roof he saw a woman bathing; and the woman was very beautiful to look on.

Naye Daudi akapeleka, akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bath-sheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti? 2 Samweli 11:3

David send and inquired after the woman. One said, Is not this Bathsheba, the daughter of Eliam, the wife of Uriah the Hittite?

Basi Daudi akapeleka wajumbe, akamtwaa; naye akaingia kwake; naye akalala naye; (maana yule mwanamke amekwisha kutakasika unajisi wake); kisha akarudi nyumbani kwake. 2 Samweli 11:4

David sent messengers, and took her; and she came in to him, and he lay with her (for she was purified from her uncleanness); and she returned to her house.

Yule mwanamke akachukua mimba; basi akapeleka na kumwambia Daudi, akasema, Ni mja-mzito. 2 Samweli 11:5

The woman conceived; and she sent and told David, and said, I am with child.

Ndipo Daudi akapeleka kwa Yoabu, akisema, Unipelekee Uria, Mhiti. Naye Yoabu akampeleka Uria kwa Daudi. 2 Samweli 11:6

David sent to Joab, [saying], Send me Uriah the Hittite. Joab sent Uriah to David.

Uria alipomwendea Daudi, Daudi alimwuliza habari za Yoabu, na habari za watu, na habari za vita. 2 Samweli 11:7

When Uriah was come to him, David asked of him how Joab did, and how the people fared, and how the war prospered.

Daudi akamwambia Uria, Haya, shuka nyumbani kwako, ukanawe miguu yako. Basi Uria akatoka katika nyumba ya mfalme, na tunu ya vyakula ikamfuata, iliyotoka kwa mfalme. 2 Samweli 11:8

David said to Uriah, Go down to your house, and wash your feet. Uriah departed out of the king's house, and there followed him a mess [of food] from the king.

Lakini Uria akalala mlangoni pa nyumba ya mfalme, pamoja na watumishi wote wa bwana wake, wala hakushuka nyumbani kwake. 2 Samweli 11:9

But Uriah slept at the door of the king's house with all the servants of his lord, and didn't go down to his house.

Watu walipomwambia Daudi ya kwamba, Uria hakushuka nyumbani kwake, Daudi akamwambia Uria, Je! Hukutoka safarini? Mbona hukushuka nyumbani kwako? 2 Samweli 11:10

When they had told David, saying, Uriah didn't go down to his house, David said to Uriah, Haven't you come from a journey? why did you not go down to your house?

Naye Uria akamwambia Daudi, Sanduku, na Israeli, na Yuda, wanakaa vibandani; na bwana wangu Yoabu, na watumishi wa bwana wangu, wamepiga kambi waziwazi uwandani; nami niende nyumbani kwangu, kula na kunywa, na kulala na mke wangu? Uishivyo, na kama roho yako iishivyo, mimi sitafanya jambo hili. 2 Samweli 11:11

Uriah said to David, The ark, and Israel, and Judah, abide in booths; and my lord Joab, and the servants of my lord, are encamped in the open field; shall I then go into my house, to eat and to drink, and to lie with my wife? as you live, and as your soul lives, I will not do this thing.

Basi Daudi akamwambia Uria, Ngoja hapa leo tena, na kesho nitakuacha kwenda zako. Basi Uria akakaa Yerusalemu siku ile, na siku ya pili yake. 2 Samweli 11:12

David said to Uriah, Stay here today also, and tomorrow I will let you depart. So Uriah abode in Jerusalem that day, and the next day.

Naye Daudi akamwalika, akala, akanywa mbele yake; naye akamlevya; hata wakati wa jioni akatoka kwenda kulala kitandani mwake pamoja na watumishi wa bwana wake, lakini hakushuka nyumbani kwake. 2 Samweli 11:13

When David had called him, he ate and drink before him; and he made him drunk: and at even he went out to lie on his bed with the servants of his lord, but didn't go down to his house.

Hata ikawa asubuhi, Daudi akamwandikia Yoabu waraka, akaupeleka kwa mkono wa Uria. 2 Samweli 11:14

It happened in the morning, that David wrote a letter to Joab, and sent it by the hand of Uriah.

Akaandika katika waraka huo, kusema, Mwekeni Uria mbele ya watu penye vita vikali, kisha ondokeni, mmwache, ili apigwe akafe. 2 Samweli 11:15

He wrote in the letter, saying, Set Uriah in the forefront of the hottest battle, and retire you from him, that he may be struck, and die.

Ikawa, Yoabu alipokuwa akiuhusuru mji, akamweka Uria mahali alipojua ya kuwa pana mashujaa. 2 Samweli 11:16

It happened, when Joab kept watch on the city, that he assigned Uriah to the place where he knew that valiant men were.

Watu wa mji wakatoka, wakapigana na Yoabu; na baadhi ya watu, watumishi wa Daudi, wakaanguka; Uria Mhiti naye akafa. 2 Samweli 11:17

The men of the city went out, and fought with Joab: and there fell some of the people, even of the servants of David; and Uriah the Hittite died also.

Ndipo Yoabu akapeleka na kumwarifu Daudi habari zote za vita; 2 Samweli 11:18

Then Joab sent and told David all the things concerning the war;

akamwagiza yule mjumbe, akisema, Ukiisha kumpa mfalme habari zote za vita, 2 Samweli 11:19

and he charged the messenger, saying, "When you have made an end of telling all the things concerning the war to the king,

itakuwa, hasira ya mfalme ikiwaka, akakuambia, Kwani mliukaribia mji namna ile ili kuupiga? Je! Hamkujua ya kuwa watapiga mishale toka ukutani? 2 Samweli 11:20

it shall be that, if the king's wrath arise, and he tells you, 'Why did you go so near to the city to fight? Didn't you know that they would shoot from the wall?

Ni nani aliyempiga Ahimeleki, mwana wa Yeru-beshethi? Je! Si mwanamke aliyemtupia jiwe la kusagia la juu kutoka ukutani? Hata akafa huko Thebesi? Kwani kuukaribia ukuta namna ile? Ndipo utakaposema, Mtumishi wako Uria, Mhiti, amekufa naye. 2 Samweli 11:21

who struck Abimelech the son of Jerubbesheth? Didn't a woman cast an upper millstone on him from the wall, so that he died at Thebez? Why did you go so near the wall?' then shall you say, 'Your servant Uriah the Hittite is dead also.'"

Basi yule mjumbe akaenda, akafika na kumwonyesha Daudi yote aliyomtuma Yoabu. 2 Samweli 11:22

So the messenger went, and came and shown David all that Joab had sent him for.

Yule mjumbe akamwambia Daudi, Watu hao walitushinda, wakatutokea nje hata uwandani, tukashindana nao hata mahali pa kuingilia langoni. 2 Samweli 11:23

The messenger said to David, The men prevailed against us, and came out to us into the field, and we were on them even to the entrance of the gate.

Wapiga mishale wakatupiga sisi, watumishi wako, toka juu ya ukuta; na baadhi ya watumishi wa mfalme wamekufa, na Uria, Mhiti, mtumishi wako, amekufa naye. 2 Samweli 11:24

The shooters shot at your servants from off the wall; and some of the king's servants are dead, and your servant Uriah the Hittite is dead also.

Basi Daudi akamwambia yule mjumbe, Basi, mwambie Yoabu maneno haya, Jambo hili lisiwe baya machoni pako, maana upanga hula huyu kama unavyomla huyu; zidi kutia nguvu vita vyako juu ya mji ukauangushe; nawe mtie moyo. 2 Samweli 11:25

Then David said to the messenger, Thus shall you tell Joab, Don't let this thing displease you, for the sword devours one as well as another; make your battle more strong against the city, and overthrow it: and encourage you him.

Na yule mke wa Uria alipopata habari ya kuwa Uria mumewe amekufa, akamwombolezea mumewe. 2 Samweli 11:26

When the wife of Uriah heard that Uriah her husband was dead, she made lamentation for her husband.

Hata maombolezo hayo yalipokwisha, Daudi akatuma mtu, akamtwaa, akamtia nyumbani mwake; naye akawa mkewe, akamzalia mwana. Lakini jambo lile alilolitenda Daudi likamchukiza Bwana.

2 Samweli 11:27

When the mourning was past, David sent and took her home to his house, and she became his wife, and bore him a son. But the thing that David had done displeased Yahweh.