2 Samweli 17 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Samweli 17 (Swahili) 2nd Samuel 17 (English)

Zaidi ya hayo Ahithofeli akamwambia Absalomu, Niache nichague watu kumi na mbili elfu, nami nitaondoka na kumfuatia Daudi usiku huu; 2 Samweli 17:1

Moreover Ahithophel said to Absalom, Let me now choose out twelve thousand men, and I will arise and pursue after David this night:

nami nitamshambulia wakati atakaokuwa amechoka, na mikono yake imekuwa dhaifu, nami nitamtia hofu; na watu wote walio pamoja naye watakimbia; nami nitampiga mfalme peke yake; 2 Samweli 17:2

and I will come on him while he is weary and weak-handed, and will make him afraid; and all the people who are with him shall flee; and I will strike the king only;

na hao watu wote nitawarejeza kwako; mtu yule umtafutaye ni kana kwamba wamerudi wote; na hivyo watu wote watakuwa katika amani. 2 Samweli 17:3

and I will bring back all the people to you: the man whom you seek is as if all returned: [so] all the people shall be in peace.

Shauri hili likawa jema machoni pa Absalomu, na machoni pa wazee wote wa Israeli. 2 Samweli 17:4

The saying pleased Absalom well, and all the elders of Israel.

Ndipo Absalomu akasema, Basi, mwiteni Hushai, Mwarki, naye, tukasikie atakayosema yeye pia. 2 Samweli 17:5

Then said Absalom, Call now Hushai the Archite also, and let us hear likewise what he says.

Basi Hushai alipofika kwa Absalomu, Absalomu akamwambia, akasema, Ahithofeli amesema hivi; je! Tufanye kama alivyosema? Kama sivyo, sema maneno yako. 2 Samweli 17:6

When Hushai was come to Absalom, Absalom spoke to him, saying, Ahithophel has spoken after this manner: shall we do [after] his saying? if not, speak up.

Hushai akamwambia Absalomu, Shauri hili alilolitoa Ahithofeli si jema wakati huu. 2 Samweli 17:7

Hushai said to Absalom, The counsel that Ahithophel has given this time is not good.

Hushai akafuliza kusema, Wamjua baba yako na watu wake, ya kuwa ni watu mashujaa hawa, nao wana uchungu katika mioyo yao, kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake nyikani; tena baba yako ni mtu wa vita, hatalala pamoja na watu wake. 2 Samweli 17:8

Hushai said moreover, You know your father and his men, that they are mighty men, and they are fierce in their minds, as a bear robbed of her cubs in the field; and your father is a man of war, and will not lodge with the people.

Angalia, amefichwa sasa katika shimo, au penginepo; kisha itakuwa, watakapoanguka baadhi yao mwanzo, kila mtu atakayesikia, atasema, Kuna machinjo katika watu wanaofuatana na Absalomu. 2 Samweli 17:9

Behold, he is hid now in some pit, or in some [other] place: and it will happen, when some of them are fallen at the first, that whoever hears it will say, There is a slaughter among the people who follow Absalom.

Basi hata yeye aliye shujaa, mwenye moyo kama moyo wa simba, atayeyuka kabisa; maana Israeli wote wanajua ya kuwa baba yako ni shujaa, na ya kuwa watu wale walio pamoja naye ni mashujaa. 2 Samweli 17:10

Even he who is valiant, whose heart is as the heart of a lion, will utterly melt; for all Israel knows that your father is a mighty man, and those who are with him are valiant men.

Kwa hiyo shauri langu ni hili, Waisraeli wote toka Dani mpaka Beer-sheba wakusanyike kwako, kama mchanga wa bahari kwa wingi; na wewe uende vitani mwenyewe. 2 Samweli 17:11

But I counsel that all Israel be gathered together to you, from Dan even to Beersheba, as the sand that is by the sea for multitude; and that you go to battle in your own person.

Hivyo tutamfikia mahali po pote atakapoonekana, na kumwangukia kama vile umande uangukavyo juu ya nchi; wala hatutaacha hata mmoja wao, yeye na watu wote walio pamoja naye. 2 Samweli 17:12

So shall we come on him in some place where he shall be found, and we will light on him as the dew falls on the ground; and of him and of all the men who are with him we will not leave so much as one.

Tena, ikiwa amejitia katika mji uwao wote, basi Israeli wote wataleta kamba, na kuuendea mji ule, nasi tutaukokota mpaka mtoni, wala halitaonekana huko hata jiwe dogo moja la mawe yake. 2 Samweli 17:13

Moreover, if he be gotten into a city, then shall all Israel bring ropes to that city, and we will draw it into the river, until there not be one small stone found there.

Naye Absalomu na watu wote wa Israeli wakasema, Shauri la Hushai, Mwarki, ni jema kuliko shauri la Ahithofeli. Kwa maana Bwana alikuwa amekusudia kulivunja shauri jema la Ahithofeli, ili Bwana alete mabaya juu ya Absalomu. 2 Samweli 17:14

Absalom and all the men of Israel said, The counsel of Hushai the Archite is better than the counsel of Ahithophel. For Yahweh had ordained to defeat the good counsel of Ahithophel, to the intent that Yahweh might bring evil on Absalom.

Ndipo Hushai akawaambia Sadoki na Abiathari, makuhani, Ahithofeli amempa Absalomu na wazee wa Israeli mashauri kadha wa kadha; na mimi nimetoa mashauri kadha wa kadha. 2 Samweli 17:15

Then said Hushai to Zadok and to Abiathar the priests, Thus and thus did Ahithophel counsel Absalom and the elders of Israel; and thus and thus have I counseled.

Basi sasa pelekeni habari upesi kamwambieni Daudi ya kwamba, Usilale usiku huu karibu na vivuko vya jangwani; bali usikose kuvuka; asije akamezwa mfalme, na watu wote walio pamoja naye. 2 Samweli 17:16

Now therefore send quickly, and tell David, saying, Don't lodge this night at the fords of the wilderness, but by all means pass over; lest the king be swallowed up, and all the people who are with him.

Basi Yonathani na Ahimaasi walikuwa wakikaa karibu na Enrogeli; na mjakazi mmoja alikuwa akienda na kuwapa habari; nao huenda kumwambia mfalme Daudi; maana ilikuwa lazima wasionekane wakiingia mjini. 2 Samweli 17:17

Now Jonathan and Ahimaaz were staying by En Rogel; and a maid-servant used to go and tell them; and they went and told king David: for they might not be seen to come into the city.

Lakini kijana mmoja aliwaona, akamwambia Absalomu; basi wakaenda wote wawili kwa haraka, wakafika Bahurimu, nyumbani kwa mtu aliyekuwa na kisima uani mwake; wakashuka ndani yake. 2 Samweli 17:18

But a boy saw them, and told Absalom: and they went both of them away quickly, and came to the house of a man in Bahurim, who had a well in his court; and they went down there.

Na mwanamke akatwaa kifuniko akakiweka juu ya mdomo wa kile kisima, akaanika ngano iliyotwangwa juu yake; wala halikujulikana neno lo lote. 2 Samweli 17:19

The woman took and spread the covering over the well's mouth, and strewed bruised grain thereon; and nothing was known.

Nao watumishi wa Absalomu wakamwendea yule mwanamke mle nyumbani; wakasema, Wako wapi Yonathani na Ahimaasi? Yule mwanamke akawaambia, Wamevuka kijito cha maji. Basi walipokwisha kuwatafuta wasiwaone, wakarudi Yerusalemu. 2 Samweli 17:20

Absalom's servants came to the woman to the house; and they said, Where are Ahimaaz and Jonathan? The woman said to them, They have gone over the brook of water. When they had sought and could not find them, they returned to Jerusalem.

Kisha ikawa, baada ya kuondoka kwao, wale wakatoka kisimani, wakaenda wakamwarifu mfalme Daudi; wakamwambia Daudi, Ondokeni, mkavuke maji haya upesi; maana ndivyo alivyotoa shauri Ahithofeli juu yenu. 2 Samweli 17:21

It happened, after they had departed, that they came up out of the well, and went and told king David; and they said to David, Arise you, and pass quickly over the water; for thus has Ahithophel counseled against you.

Ndipo Daudi, na watu wote waliokuwa pamoja naye, wakaondoka, wakavuka Yordani; na kulipopambazuka hakubaki mmojawapo wao asiyevuka Yordani. 2 Samweli 17:22

Then David arose, and all the people who were with him, and they passed over the Jordan: by the morning light there lacked not one of them who had not gone over the Jordan.

Naye Ahithofeli alipoona ya kuwa shauri lake halikufuatwa, akatandika punda wake, akaondoka, akaenda nyumbani kwake, mjini mwake, akaitengeneza nyumba yake, akajisonga; akafa, akazikwa kaburini mwa babaye. 2 Samweli 17:23

When Ahithophel saw that his counsel was not followed, he saddled his donkey, and arose, and got him home, to his city, and set his house in order, and hanged himself; and he died, and was buried in the tomb of his father.

Basi Daudi akaja Mahanaimu. Naye Absalomu akauvuka Yordani yeye na watu wote wa Israeli pamoja naye. 2 Samweli 17:24

Then David came to Mahanaim. Absalom passed over the Jordan, he and all the men of Israel with him.

Naye Absalomu akamweka Amasa awe juu ya jeshi mahali pa Yoabu. Basi huyo Amasa alikuwa mwana wa mtu, jina lake Yetheri, Mwishmaeli, aliyeingia kwa Abigali, binti Nahashi, nduguye Seruya, mamaye Yoabu. 2 Samweli 17:25

Absalom set Amasa over the host instead of Joab. Now Amasa was the son of a man, whose name was Ithra the Israelite, who went in to Abigail the daughter of Nahash, sister to Zeruiah, Joab's mother.

Israeli na Absalomu wakapiga kambi katika nchi ya Gileadi. 2 Samweli 17:26

Israel and Absalom encamped in the land of Gilead.

Ikawa, Daudi alipofika Mahanaimu, Shobi, mwana wa Nahashi wa Raba, wa wana wa Amoni, na Makiri, mwana wa Amieli wa Lo-debari, na Barzilai, Mgileadi wa Rogelimu, 2 Samweli 17:27

It happened, when David was come to Mahanaim, that Shobi the son of Nahash of Rabbah of the children of Ammon, and Machir the son of Ammiel of Lodebar, and Barzillai the Gileadite of Rogelim,

wakaleta magodoro, na mabakuli, na vyungu, na ngano, na shayiri, na unga, na bisi, na kunde, na dengu, 2 Samweli 17:28

brought beds, and basins, and earthen vessels, and wheat, and barley, and meal, and parched [grain], and beans, and lentils, and parched [pulse],

na asali, na siagi, na kondoo, na samli ya ng'ombe, wapate kula Daudi na watu waliokuwa pamoja naye; kwani walisema, Watu hao waona njaa, tena wamechoka, nao wana kiu huku nyikani.

2 Samweli 17:29

and honey, and butter, and sheep, and cheese of the herd, for David, and for the people who were with him, to eat: for they said, The people are hungry, and weary, and thirsty, in the wilderness.