2 Samweli 24 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Samweli 24 (Swahili) 2nd Samuel 24 (English)

Tena hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, akamtia Daudi nia juu yao, akisema, Nenda, ukawahesabu Israeli na Yuda. 2 Samweli 24:1

Again the anger of Yahweh was kindled against Israel, and he moved David against them, saying, Go, number Israel and Judah.

Basi mfalme akamwambia Yoabu, jemadari wa jeshi la askari, waliokuwa pamoja naye, Zunguka sasa katikati ya kabila zote za Israeli, tangu Dani mpaka Beer-sheba, mkawahesabu watu, nipate kujua jumla ya hao watu. 2 Samweli 24:2

The king said to Joab the captain of the host, who was with him, Go now back and forth through all the tribes of Israel, from Dan even to Beersheba, and number you the people, that I may know the sum of the people.

Naye Yoabu akamwambia mfalme, Bwana, Mungu wako, na awaongeze watu, hesabu yao ikiwa yo yote, mara mia, tena macho ya bwana wangu mfalme na yawaone; ila kwa nini neno hili limempendeza bwana wangu mfalme? 2 Samweli 24:3

Joab said to the king, Now Yahweh your God add to the people, however many they may be, one hundred times; and may the eyes of my lord the king see it: but why does my lord the king delight in this thing?

Lakini neno la mfalme likawa na nguvu juu ya Yoabu, na juu ya majemadari wa jeshi. Basi Yoabu akatoka na majemadari wa jeshi machoni pa mfalme, kwenda kuwahesabu watu wa Israeli. 2 Samweli 24:4

Notwithstanding, the king's word prevailed against Joab, and against the captains of the host. Joab and the captains of the host went out from the presence of the king, to number the people of Israel.

Wakavuka Yordani, wakapiga kambi huko Aroeri, upande wa kuume wa mji ulioko kati ya bonde la Gadi, na mpaka Yazeri; 2 Samweli 24:5

They passed over the Jordan, and encamped in Aroer, on the right side of the city that is in the middle of the valley of Gad, and to Jazer:

kisha wakaja Gileadi, na nchi ya Wahiti huko Kadeshi; kisha wakaja Dani, na kutoka Dani wakazunguka mpaka Sidoni, 2 Samweli 24:6

then they came to Gilead, and to the land of Tahtim Hodshi; and they came to Dan Jaan, and round about to Sidon,

wakaja ngomeni kwa Tiro, na kwa miji yote ya Wahivi, na ya Wakanaani; tena wakatoka kusini kwa Yuda huko Beer-sheba. 2 Samweli 24:7

and came to the stronghold of Tyre, and to all the cities of the Hivites, and of the Canaanites; and they went out to the south of Judah, at Beersheba.

Nao walipokwisha kuzunguka nchi yote, wakaja Yerusalemu mwisho wa miezi kenda na siku ishirini. 2 Samweli 24:8

So when they had gone back and forth through all the land, they came to Jerusalem at the end of nine months and twenty days.

Naye Yoabu akamtolea mfalme jumla ya hesabu ya watu; nao walikuwa wa Israeli mashujaa wenye kufuta panga mia nane elfu; nao wa Yuda walikuwa watu mia tano elfu. 2 Samweli 24:9

Joab gave up the sum of the numbering of the people to the king: and there were in Israel eight hundred thousand valiant men who drew the sword; and the men of Judah were five hundred thousand men.

Ndipo moyo wake Daudi ukamchoma baada ya kuwahesabu hao watu. Naye Daudi akamwambia Bwana, Nimekosa sana kwa haya niliyoyafanya; lakini sasa, Ee Bwana, nakusihi uuondolee mbali uovu wa mtumishi wako; kwani nimefanya upumbavu kabisa. 2 Samweli 24:10

David's heart struck him after that he had numbered the people. David said to Yahweh, I have sinned greatly in that which I have done: but now, Yahweh, put away, I beg you, the iniquity of your servant; for I have done very foolishly.

Na Daudi alipoondoka asubuhi, neno la Bwana likamjia nabii Gadi, mwonaji wake Daudi, kusema, 2 Samweli 24:11

When David rose up in the morning, the word of Yahweh came to the prophet Gad, David's seer, saying,

Nenda, ukanene na Daudi, Bwana asema hivi, Nakuwekea mambo matatu; katika haya uchague moja, nikutendee hilo. 2 Samweli 24:12

Go and speak to David, Thus says Yahweh, I offer you three things: choose you one of them, that I may do it to you.

Basi Gadi akamwendea Daudi, akamweleza, akamwambia, Basi, miaka saba ya njaa ikujie katika nchi yako? Au miezi mitatu ukimbie mbele ya adui zako, huku wakikufuatia? Au siku tatu iwe tauni katika nchi yako? Fanya shauri sasa, ufikiri, ni jawabu gani nimrudishie yeye aliyenituma. 2 Samweli 24:13

So Gad came to David, and told him, and said to him, Shall seven years of famine come to you in your land? or will you flee three months before your foes while they pursue you? or shall there be three days' pestilence in your land? now advise you, and consider what answer I shall return to him who sent me.

Naye Daudi akamwambia Gadi, Nimeingia katika mashaka sana; basi sasa na tuanguke katika mkono wa Bwana; kwa kuwa rehema zake ni nyingi; wala nisianguke katika mkono wa wanadamu. 2 Samweli 24:14

David said to Gad, I am in a great strait: let us fall now into the hand of Yahweh; for his mercies are great; and let me not fall into the hand of man.

Basi Bwana akawaletea Israeli tauni tangu asubuhi hata wakati ulioamriwa; nao wakafa watu toka Dani mpaka Beer-sheba sabini elfu. 2 Samweli 24:15

So Yahweh sent a pestilence on Israel from the morning even to the time appointed; and there died of the people from Dan even to Beersheba seventy thousand men.

Lakini huyo malaika aliponyosha mkono wake kuelekea Yerusalemu ili auharibu, Bwana akaghairi katika mabaya, akamwambia huyo malaika mwenye kuwaharibu watu, Yatosha, sasa ulegeze mkono wako. Naye yule malaika wa Bwana alikuwako karibu na kiwanja cha kupuria cha Arauna, Myebusi. 2 Samweli 24:16

When the angel stretched out his hand toward Jerusalem to destroy it, Yahweh repented him of the evil, and said to the angel who destroyed the people, It is enough; now stay your hand. The angel of Yahweh was by the threshing floor of Araunah the Jebusite.

Daudi, alipomwoma malaika aliyewapiga watu, akanena na Bwana, akasema, Tazama, ni mimi niliyekosa, ni mimi niliyepotoka; lakini kondoo hawa, wamefanya nini? Mkono wako na uwe juu yangu, na juu ya nyumba ya baba yangu. 2 Samweli 24:17

David spoke to Yahweh when he saw the angel who struck the people, and said, Behold, I have sinned, and I have done perversely; but these sheep, what have they done? Please let your hand be against me, and against my father's house.

Siku hiyo Gadi akamwendea Daudi, akamwambia, Haya! Kwea wewe, ukamwinulie Bwana madhabahu penye kiwanja cha Arauna, Myebusi. 2 Samweli 24:18

Gad came that day to David, and said to him, Go up, rear an altar to Yahweh in the threshing floor of Araunah the Jebusite.

Basi Daudi akakwea sawasawa na neno la Gadi, kama Bwana alivyoamuru. 2 Samweli 24:19

David went up according to the saying of Gad, as Yahweh commanded.

Huyo Arauna akatazama, akamwona mfalme na watumishi wake wakimjia; Arauna akatoka, akasujudu mbele ya mfalme kifulifuli hata nchi. 2 Samweli 24:20

Araunah looked forth, and saw the king and his servants coming on toward him: and Araunah went out, and bowed himself before the king with his face to the ground.

Arauna akasema, Bwana wangu mfalme amemjia mtumwa wake kwa kusudi gani? Naye Daudi akasema, Makusudi ninunue kwako kiwanja hiki, ili nimjengee Bwana madhabahu, ili kwamba tauni ipate kuzuiliwa katika watu. 2 Samweli 24:21

Araunah said, Why is my lord the king come to his servant? David said, To buy the threshing floor of you, to build an altar to Yahweh, that the plague may be stayed from the people.

Arauna akamwambia Daudi, Bwana wangu mfalme na akitwae, akatolee yaliyo mema machoni pake; tazama, ng'ombe hawa kwa sadaka ya kuteketezwa, tena vyombo vya kupuria, na vyombo vya ng'ombe, viko kwa kuni, 2 Samweli 24:22

Araunah said to David, Let my lord the king take and offer up what seems good to him: behold, the oxen for the burnt offering, and the threshing instruments and the yokes of the oxen for the wood:

vitu hivi vyote, Ee mfalme, mimi Arauna nakupa wewe mfalme. Kisha Arauna akamwambia mfalme, Bwana, Mungu wako, na akukubali. 2 Samweli 24:23

all this, king, does Araunah give to the king. Araunah said to the king, Yahweh your God accept you.

Lakini mfalme akamwambia Arauna, La, sivyo; lakini kweli nitavinunua kwako kwa thamani yake; wala sitamtolea Bwana, Mungu wangu, sadaka za kuteketezwa nisizozigharimia. Hivyo Daudi akakinunua hicho kiwanja cha kupuria na wale ng'ombe kwa shekeli hamsini za fedha. 2 Samweli 24:24

The king said to Araunah, No; but I will most assuredly buy it of you at a price. Neither will I offer burnt-offerings to Yahweh my God which cost me nothing. So David bought the threshing floor and the oxen for fifty shekels of silver.

Naye Daudi akamjengea Bwana madhabahu huko, akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Basi Bwana aliiridhia nchi, na tauni ikazuiliwa katika Israeli. 2 Samweli 24:25

David built there an altar to Yahweh, and offered burnt offerings and peace-offerings. So Yahweh was entreated for the land, and the plague was stayed from Israel.