Mwanzo 14 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 14 (Swahili) Genesis 14 (English)

Ikawa siku za Amrafeli mfalme wa Shinari, na Arioko mfalme wa Elasari, na Kedorlaoma mfalme wa Elamu na Tidali mfalme wa Goimu, Mwanzo 14:1

It happened in the days of Amraphel, king of Shinar, Arioch, king of Ellasar, Chedorlaomer, king of Elam, and Tidal, king of Goiim,

walifanya vita na Bera mfalme wa Sodoma na Birsha mfalme wa Gomora, na Shinabu mfalme wa Adma, na Shemeberi mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela, ndio Soari. Mwanzo 14:2

that they made war with Bera, king of Sodom, and with Birsha, king of Gomorrah, Shinab, king of Admah, and Shemeber, king of Zeboiim, and the king of Bela (the same is Zoar).

Hawa wote wakakutana panapo bonde la Sidimu, kwenye Bahari ya Chumvi. Mwanzo 14:3

All these joined together in the valley of Siddim (the same is the Salt Sea).

Miaka kumi na miwili walimtumikia Kedorlaoma, hata mwaka wa kumi na tatu wakaasi. Mwanzo 14:4

Twelve years they served Chedorlaomer, and in the thirteenth year, they rebelled.

Na mwaka wa kumi na nne akaja Kedorlaoma na wafalme waliokuwa pamoja naye, wakawapiga Warefai katika Ashteroth-karnaimu, na Wazuzi katika Hamu, na Waemi katika Shawe-kiryathaimu, Mwanzo 14:5

In the fourteenth year Chedorlaomer came, and the kings who were with him, and struck the Rephaim in Ashteroth Karnaim, and the Zuzim in Ham, and the Emim in Shaveh-kiriathaim,

na Wahori katika mlima wao Seiri, mpaka Elparani iliyo karibu na jangwa. Mwanzo 14:6

and the Horites in their Mount Seir, to Elparan, which is by the wilderness.

Kisha wakarudi wakaja mpaka Enmisfati, ndio Kadeshi, wakapiga nchi yote ya Waamaleki, na Waamori waliokaa Hasason-tamari. Mwanzo 14:7

They returned, and came to En-mishpat (the same is Kadesh), and struck all the country of the Amalekites, and also the Amorites, that lived in Hazazon Tamar.

Mfalme wa Sodoma, na mfalme wa Gomora, na mfalme wa Adma, na mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela, ndio Soari, wakatoka wakapanga vita panapo bonde la Sidimu; Mwanzo 14:8

There went out the king of Sodom, and the king of Gomorrah, and the king of Admah, and the king of Zeboiim, and the king of Bela (the same is Zoar); and they set the battle in array against them in the valley of Siddim;

wapigane na Kedorlaoma mfalme wa Elamu, na Tidali mfalme wa Goimu, na Amrafeli mfalme wa Shinari, na Arioko mfalme wa Elasari, wafalme wanne juu ya wale watano. Mwanzo 14:9

against Chedorlaomer king of Elam, and Tidal king of Goiim, and Amraphel king of Shinar, and Arioch king of Ellasar; four kings against the five.

Na bonde la Sidimu lilikuwa limejaa mashimo ya lami. Nao wafalme wa Sodoma na Gomora wakakimbia, wakaanguka huko, nao waliosalia wakakimbia milimani. Mwanzo 14:10

Now the valley of Siddim was full of tar pits; and the kings of Sodom and Gomorrah fled, and they fell there, and those who remained fled to the mountain.

Wakachukua mali zote za Sodoma na Gomora na vyakula vyao vyote, wakaenda zao. Mwanzo 14:11

They took all the goods of Sodom and Gomorrah, and all their food, and went their way.

Wakamtwaa Lutu, mwana wa nduguye Abramu, aliyekaa huko Sodoma, na mali yake, wakaenda zao. Mwanzo 14:12

They took Lot, Abram's brother's son, who lived in Sodom, and his goods, and departed.

Mtu mmoja aliyeponyoka akaenda, akampasha habari Abramu Mwebrania; naye amekaa panapo mialoni ya Mamre, yule Mwamori, ndugu ya Eshkoli, na ndugu ya Aneri, na hao walikuwa wamepatana na Abramu. Mwanzo 14:13

One who had escaped came and told Abram, the Hebrew. Now he lived by the oaks of Mamre, the Amorite, brother of Eshcol, and brother of Aner; and these were allies of Abram.

Abramu aliposikia ya kwamba nduguye ametekwa mateka, akawapa silaha vijana wake, waliozaliwa katika nyumba yake, watu mia tatu na kumi na wanane, akawafuata mpaka Dani. Mwanzo 14:14

When Abram heard that his relative was taken captive, he led forth his trained men, born in his house, three hundred and eighteen, and pursued as far as Dan.

Akajipanga apigane nao usiku, yeye na watumwa wake, akawapiga, akawafukuza mpaka Hoba, ulioko upande wa kushoto wa Dameski. Mwanzo 14:15

He divided himself against them by night, he and his servants, and struck them, and pursued them to Hobah, which is on the left hand of Damascus.

Naye akarudisha mali zote, akamrudisha na Lutu nduguye na mali zake, na wanawake pia, na watu. Mwanzo 14:16

He brought back all the goods, and also brought back his relative, Lot, and his goods, and the women also, and the people.

Abramu aliporudi kutoka kumpiga Kedorlaoma na wale wafalme waliokuwa pamoja naye, mfalme wa Sodoma akatoka amlaki katika bonde la Shawe, nalo ni Bonde la Mfalme. Mwanzo 14:17

The king of Sodom went out to meet him, after his return from the slaughter of Chedorlaomer and the kings who were with him, at the valley of Shaveh (the same is the King's Valley).

Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana. Mwanzo 14:18

Melchizedek king of Salem brought forth bread and wine: and he was priest of God Most High.

Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi. Mwanzo 14:19

He blessed him, and said, "Blessed be Abram of God Most High, possessor of heaven and earth:

Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote. Mwanzo 14:20

and blessed be God Most High, who has delivered your enemies into your hand." Abram gave him a tenth of all.

Mfalme wa Sodoma akamwambia Abramu, Nipe mimi hao watu, na hizo mali uchukue wewe. Mwanzo 14:21

The king of Sodom said to Abram, "Give me the people, and take the goods to yourself."

Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, Nimeinua mkono wangu kwa Bwana, Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi, Mwanzo 14:22

Abram said to the king of Sodom, "I have lifted up my hand to Yahweh, God Most High, possessor of heaven and earth,

ya kuwa sitatwaa uzi wala gidamu ya kiatu wala cho chote kilicho chako, usije ukasema, Nimemtajirisha Abramu; Mwanzo 14:23

that I will not take a thread nor a shoe-latchet nor anything that is yours, lest you should say, 'I have made Abram rich.'

isipokuwa hivyo walivyokula vijana, na sehemu za watu waliokwenda nami, yaani, Aneri, na Eshkoli, na Mamre; na watwae wao sehemu zao. Mwanzo 14:24

Except only that which the young men have eaten, and the portion of the men who went with me, Aner, Eshcol, and Mamre: let them take their portion."