Mwanzo 18 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 18 (Swahili) Genesis 18 (English)

Bwana akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari. Mwanzo 18:1

Yahweh appeared to him by the oaks of Mamre, as he sat in the tent door in the heat of the day.

Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi, Mwanzo 18:2

He lifted up his eyes and looked, and saw that three men stood opposite him. When he saw them, he ran to meet them from the tent door, and bowed himself to the earth,

akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako. Mwanzo 18:3

and said, "My lord, if now I have found favor in your sight, please don't go away from your servant.

Na yaletwe basi maji kidogo mkanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu. Mwanzo 18:4

Now let a little water be fetched, wash your feet, and rest yourselves under the tree.

Nami nitaleta chakula kidogo, mkaburudishe moyo, baadaye mwendelee, iwapo mmemjia mtumwa wenu. Wakasema, Haya, fanya kama ulivyosema. Mwanzo 18:5

I will get a morsel of bread so you can refresh your heart. After that you may go your way, now that you have come to your servant." They said, "Very well, do as you have said."

Basi Ibrahimu akaenda hima hemani kwa Sara, akasema, Himiza vipimo vitatu vya unga safi, uukande, ufanye mikate. Mwanzo 18:6

Abraham hurried into the tent to Sarah, and said, "Quickly make ready three measures of fine meal, knead it, and make cakes."

Ibrahimu akapiga mbio kwenda kundini, akaleta ndama wa ng'ombe aliye laini, mzuri, akampa mtumishi, naye akahimiza kuiandaa. Mwanzo 18:7

Abraham ran to the herd, and fetched a tender and good calf, and gave it to the servant. He hurried to dress it.

Akatwaa siagi na maziwa, na ndama aliyoiandaa, akawaandikia mbele yao, akasimama karibu nao chini ya mti, nao wakala. Mwanzo 18:8

He took butter, milk, and the calf which he had dressed, and set it before them. He stood by them under the tree, and they ate.

Wakamwambia, Yu wapi Sara mkeo? Akasema, Yumo hemani. Mwanzo 18:9

They said to him, "Where is Sarah, your wife? He said, "See, in the tent."

Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake. Mwanzo 18:10

He said, "I will certainly return to you when the season comes round. Behold, Sarah your wife will have a son." Sarah heard in the tent door, which was behind him.

Basi Ibrahimu na Sara walikuwa wazee, na umri wao mkubwa, na Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake. Mwanzo 18:11

Now Abraham and Sarah were old, well advanced in age. It had ceased to be with Sarah after the manner of women.

Kwa hiyo Sara akacheka moyoni mwake, akisema, Niwapo mkongwe, nitapata furaha, na bwana wangu mzee? Mwanzo 18:12

Sarah laughed within herself, saying, "After I have grown old will I have pleasure, my lord being old also?"

Bwana akamwambia Ibrahimu, Mbona Sara amecheka akisema, Mimi kweli nitazaa mwana, nami ni mzee? Mwanzo 18:13

Yahweh said to Abraham, "Why did Sarah laugh, saying, 'Will I really bear a child, yet I am old?'

Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda Bwana? Kwa muhula wake nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume. Mwanzo 18:14

Is anything too hard for Yahweh? At the set time I will return to you, when the season comes round, and Sarah will have a son."

Akakana Sara, akisema, Sikucheka, maana aliogopa. Naye akasema, Sivyo, umecheka. Mwanzo 18:15

Then Sarah denied, saying, "I didn't laugh," for she was afraid." He said, "No, but you did laugh."

Kisha watu hao wakaondoka huko wakaelekeza nyuso zao Sodoma. Ibrahimu akaenda pamoja nao awasindikize. Mwanzo 18:16

The men rose up from there, and looked toward Sodom. Abraham went with them to see them on their way.

Bwana akanena, Je! Nimfiche Ibrahimu jambo nilifanyalo, Mwanzo 18:17

Yahweh said, "Will I hide from Abraham what I do,

akiwa Ibrahimu atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa? Mwanzo 18:18

seeing that Abraham has surely become a great and mighty nation, and all the nations of the earth will be blessed in him?

Kwa maana nimemjua ya kwamba atawaamuru wanawe, na nyumba yake baada yake waishike njia ya Bwana, wafanye haki na hukumu, ili kwamba Bwana naye akamtimizie Ibrahimu ahadi zake. Mwanzo 18:19

For I have known him, to the end that he may command his children and his household after him, that they may keep the way of Yahweh, to do righteousness and justice; to the end that Yahweh may bring on Abraham that which he has spoken of him."

Bwana akasema, Kwa kuwa kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi, na dhambi zao zimeongezeka sana, Mwanzo 18:20

Yahweh said, "Because the cry of Sodom and Gomorrah is great, and because their sin is very grievous,

basi, nitashuka sasa nione kama wanayotenda ni kiasi cha kilio kilichonijia; na kama sivyo, nitajua. Mwanzo 18:21

I will go down now, and see whether they have done altogether according to the cry of it, which is come to me. If not, I will know."

Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Ibrahimu alikuwa akali akisimama mbele za Bwana. Mwanzo 18:22

The men turned from there, and went toward Sodom, but Abraham stood yet before Yahweh.

Ibrahimu akakaribia, akasema, Je! Utaharibu mwenye haki pamoja na mwovu? Mwanzo 18:23

Abraham drew near, and said, "Will you consume the righteous with the wicked?

Huenda wakawapo wenye haki hamsini katika mji, utaharibu, wala hutauacha mji kwa ajili ya hao hamsini wenye haki waliomo? Mwanzo 18:24

What if there are fifty righteous within the city? Will you consume and not spare the place for the fifty righteous who are therein?

Hasha usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha; Mhukumu ulimwengu wote asitende haki? Mwanzo 18:25

Be it far from you to do things like that, to kill the righteous with the wicked, that so the righteous should be as the wicked. May that be far from you. Shouldn't the Judge of all the earth do right?"

Bwana akasema, Nikiona katika Sodoma wenye haki hamsini mjini, nitapaacha mahali pote kwa ajili yao. Mwanzo 18:26

Yahweh said, "If I find in Sodom fifty righteous within the city, then I will spare all the place for their sake."

Ibrahimu akajibu, akasema, Basi, nimeshika kusema na Bwana, nami ni mavumbi na majivu tu. Mwanzo 18:27

Abraham answered, "See now, I have taken it on myself to speak to the Lord, who am but dust and ashes.

Huenda wakapunguka watano katika wale hamsini wenye haki, je! Utaharibu mji wote kwa kupungua watano? Akasema, Sitauharibu, nikiona humo arobaini na watano. Mwanzo 18:28

What if there will lack five of the fifty righteous? Will you destroy all the city for lack of five?" He said, "I will not destroy it, if I find forty-five there."

Akazidi tena kusema naye, akinena, Huenda wakaonekana humo arobaini? Akasema, Sitafanya kwa ajili ya hao arobaini. Mwanzo 18:29

He spoke to him yet again, and said, "What if there are forty found there?" He said, "I will not do it for the forty's sake."

Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema, Huenda wakaonekana huko thelathini? Akasema, Sitafanya, nikiona humo thelathini. Mwanzo 18:30

He said, "Oh don't let the Lord be angry, and I will speak. What if there are thirty found there?" He said, "I will not do it, if I find thirty there."

Akasema, Tazama, nimeshika kusema na Bwana, huenda wakaonekana huko ishirini? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao ishirini. Mwanzo 18:31

He said, "See now, I have taken it on myself to speak to the Lord. What if there are twenty found there?" He said, "I will not destroy it for the twenty's sake."

Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema mara hii tu, Huenda wakaonekana huko kumi? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao kumi. Mwanzo 18:32

He said, "Oh don't let the Lord be angry, and I will speak yet but this once. What if ten are found there?" He said, "I will not destroy it for the ten's sake."

Basi Bwana alipokwisha kuzungumza na Ibrahimu, akaenda zake; Ibrahimu naye akarudi mahali pake.

Mwanzo 18:33

Yahweh went his way, as soon as he had finished communing with Abraham, and Abraham returned to his place.