Mwanzo 6 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 6 (Swahili) Genesis 6 (English)

Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, Mwanzo 6:1

It happened, when men began to multiply on the surface of the ground, and daughters were born to them,

wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua. Mwanzo 6:2

that God's sons saw that men's daughters were beautiful, and they took for themselves wives of all that they chose.

Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini. Mwanzo 6:3

Yahweh said, "My Spirit will not strive with man forever, because he also is flesh; yet will his days be one hundred twenty years."

Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile;tena ,baada ya hayo ,wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana;hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani ,watu wenye sifa. Mwanzo 6:4

The Nephilim were in the earth in those days, and also after that, when God's sons came to men's daughters. They bore children to them: the same were the mighty men who were of old, men of renown.

Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote. Mwanzo 6:5

Yahweh saw that the wickedness of man was great in the earth, and that every imagination of the thoughts of his heart was only evil continually.

Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. Mwanzo 6:6

Yahweh was sorry that he had made man on the earth, and it grieved him in his heart.

Bwana akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya. Mwanzo 6:7

Yahweh said, "I will destroy man whom I have created from the surface of the ground; man, along with animals, creeping things, and birds of the sky; for I am sorry that I have made them."

Lakini Nuhu akapata neema machoni pa Bwana. Mwanzo 6:8

But Noah found favor in Yahweh's eyes.

Hivi ndivyo vizazi vya Nuhu. Nuhu alikuwa mtu wa haki, mkamilifu katika vizazi vyake; Nuhu alikwenda pamoja na Mungu. Mwanzo 6:9

This is the history of the generations of Noah. Noah was a righteous man, blameless among the people of his time. Noah walked with God.

Nuhu akazaa wana watatu wa kiume, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Mwanzo 6:10

Noah became the father of three sons: Shem, Ham, and Japheth.

Dunia ikaharibika mbele za Mungu, dunia ikajaa dhuluma. Mwanzo 6:11

The earth was corrupt before God, and the earth was filled with violence.

Mungu akaiona dunia, na tazama, imeharibika; maana kila mwenye mwili amejiharibia njia yake duniani. Mwanzo 6:12

God saw the earth, and saw that it was corrupt, for all flesh had corrupted their way on the earth.

Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia. Mwanzo 6:13

God said to Noah, "The end of all flesh has come before me, for the earth is filled with violence through them. Behold, I will destroy them with the earth.

Ujifanyie safina ya mti wa mvinje; fanya na vyumba ndani ya safina, ukaifunike ndani na nje kwa lami. Mwanzo 6:14

Make an ark of gopher wood. You shall make rooms in the ark, and shall seal it inside and outside with pitch.

Hivi ndivyo utakavyoifanya; mikono mia tatu urefu wa safina, mikono hamsini upana wake, na mikono thelathini kwenda juu kwake. Mwanzo 6:15

This is how you shall make it. The length of the ark will be three hundred cubits, the breadth of it fifty cubits, and the height of it thirty cubits.

Uifanyie safina mwangaza, ukaumalize juu kiasi cha mkono mmoja; ukautie mlango wa safina katika ubavu wake; ukaifanyie dari tatu, ya chini, ya pili, na ya tatu. Mwanzo 6:16

You shall make a roof in the ark, and to a cubit shall you finish it upward. You shall set the door of the ark in the side of it. You shall make it with lower, second, and third levels.

Na tazama, nitaleta gharika ya maji juu ya nchi, niharibu kila kitu chenye mwili na pumzi ya uhai, kisiwepo chini ya mbingu; kila kilichoko duniani kitakufa. Mwanzo 6:17

I, even, I do bring the flood of waters on this earth, to destroy all flesh having the breath of life from under the sky. Everything that is in the earth will die.

Lakini nitafanya agano langu nawe kuwa thabiti; nawe utaingia katika safina, wewe, na wanao, na mkeo, na wake za wanao, pamoja nawe. Mwanzo 6:18

But I will establish my covenant with you. You shall come into the ark, you, your sons, your wife, and your sons' wives with you.

Na katika kila kilicho hai chenye mwili, wawili wa kila namna utawaleta ndani ya safina, kuwahifadhi pamoja nawe; wawe mume na mke. Mwanzo 6:19

Of every living thing of all flesh, you shall bring two of every sort into the ark, to keep them alive with you. They shall be male and female.

Katika vyote virukavyo kwa jinsi yake, na kila namna ya mnyama kwa jinsi yake, kila kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake, wawili wa kila namna watakuja kwako ili uwahifadhi. Mwanzo 6:20

Of the birds after their kind, of the cattle after their kind, of every creeping thing of the ground after its kind, two of every sort shall come to you, to keep them alive.

Ukajitwalie chakula cha kila namna kinacholika, ukakusanye, nacho kitakuwa ni chakula chenu na chao. Mwanzo 6:21

Take with you of all food that is eaten, and gather it to you; and it will be for food for you, and for them."

Ndivyo alivyofanya Nuhu, sawasawa na vyote alivyomwamuru Mungu, hivyo ndivyo alivyofanya.

Mwanzo 6:22

Thus Noah did. According to all that God commanded him, so he did.