Mwanzo 20 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 20 (Swahili) Genesis 20 (English)

Ibrahimu akaondoka huko kwenda nchi ya kusini, akakaa kati ya Kadeshi na Shuri, naye akatembea katika Gerari. Mwanzo 20:1

Abraham traveled from there toward the land of the South, and lived between Kadesh and Shur. He lived as a foriegner in Gerar.

Ibrahimu akamnena Sara mkewe, Huyu ni ndugu yangu. Basi Abimeleki mfalme wa Gerari akapeleka watu akamtwaa Sara. Mwanzo 20:2

Abraham said about Sarah his wife, "She is my sister." Abimelech king of Gerar sent, and took Sarah.

Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mkewe mtu. Mwanzo 20:3

But God came to Abimelech in a dream of the night, and said to him, "Behold, you are a dead man, because of the woman whom you have taken. For she is a man's wife."

Basi Abimeleki alikuwa hakumkaribia, akasema, Ee Bwana, Je! Utaua hata taifa lenye haki? Mwanzo 20:4

Now Abimelech had not come near her. He said, "Lord, will you kill even a righteous nation?

Je! Hakuniambia mwenyewe, Huyu ni ndugu yangu? Na mwanamke mwenyewe naye alisema, Huyu ni ndugu yangu. Kwa ukamilifu wa moyo wangu, na kwa kuwa safi mikono yangu, nimefanya hivi. Mwanzo 20:5

Didn't he tell me, 'She is my sister?' She, even she herself said, 'He is my brother.' In the integrity of my heart and the innocence of my hands have I done this."

Mungu akamwambia katika ndoto, Nami nimejua ya kwamba kwa ukamilifu wa moyo wako umefanya hivi, ndipo nami nikakuzuia usinitendee dhambi, kwa hiyo sikukuacha umguse. Mwanzo 20:6

God said to him in the dream, "Yes, I know that in the integrity of your heart you have done this, and I also withheld you from sinning against me. Therefore I didn't allow you to touch her.

Basi sasa umrudishe mwanamke kwa mtu huyo, maana yeye ni nabii, naye atakuombea, upate kuishi. Bali usipomrudisha, fahamu ya kwamba kwa hakika utakufa wewe na watu wote ulio nao. Mwanzo 20:7

Now therefore, restore the man's wife. For he is a prophet, and he will pray for you, and you will live. If you don't restore her, know for sure that you will die, you, and all who are yours."

Abimeleki akaamka asubuhi na mapema, akawaita watumwa wake wote, akawaambia maneno hayo yote masikioni mwao, nao watu hao wakaogopa sana. Mwanzo 20:8

Abimelech rose early in the morning, and called all his servants, and told all these things in their ear. The men were very scared.

Kisha Abimeleki akamwita Ibrahimu, akamwambia, Umetutenda nini? Nimekukosa nini, hata ukaleta juu yangu na juu ya ufalme wangu dhambi kuu? Umenitenda matendo yasiyotendeka. Mwanzo 20:9

Then Abimelech called Abraham, and said to him, "What have you done to us? How have I sinned against you, that you have brought on me and on my kingdom a great sin? You have done deeds to me that ought not to be done!"

Abimeleki akamwambia Ibrahimu, Umeona nini hata ukatenda jambo hili? Mwanzo 20:10

Abimelech said to Abraham, "What did you see, that you have done this thing?"

Ibrahimu akasema, Kwa sababu naliona, Yakini hapana hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa ajili ya mke wangu. Mwanzo 20:11

Abraham said, "Because I thought, 'Surely the fear of God is not in this place. They will kill me for my wife's sake.'

Naye kweli ni ndugu yangu, binti wa baba yangu ila siye mwana wa mama yangu, ndipo akawa mke wangu. Mwanzo 20:12

Moreover she is indeed my sister, the daughter of my father, but not the daughter of my mother; and she became my wife.

Ikawa hapo Mungu aliponisafirisha kutoka nyumba ya baba yangu, nikamwambia, Hii ndiyo fadhili yako, utakayonifanyia. Kila mahali tuingiapo, useme, Huyu ni ndugu yangu. Mwanzo 20:13

It happened, when God caused me to wander from my father's house, that I said to her, 'This is your kindness which you shall show to me. Everywhere that we go, say of me, "He is my brother."'"

Basi Abimeleki akatwaa kondoo, na ng'ombe, na watumwa, na wajakazi, akampa Ibrahimu, akamrudishia Sara mkewe. Mwanzo 20:14

Abimelech took sheep and oxen, men-servants and women-servants, and gave them to Abraham, and restored Sarah, his wife to him.

Abimeleki akasema, Nchi yangu iko mbele yako, kaa upendapo. Mwanzo 20:15

Abimelech said, "Behold, my land is before you. Dwell where it pleases you."

Naye akamwambia Sara, Tazama! Nimempa ndugu yako fedha elfu, itakuwa kifunika macho kwako mbele ya wote walio pamoja nawe, nawe utakuwa na haki mbele ya watu wote. Mwanzo 20:16

To Sarah he said, "Behold, I have given your brother a thousand pieces of silver. Behold, it is for you a covering of the eyes to all that are with you. In front of all you are vindicated."

Ibrahimu akamwomba Mungu, Mungu akamponya Abimeleki, na mkewe, na wajakazi wake, nao wakazaa wana. Mwanzo 20:17

Abraham prayed to God. God healed Abimelech, and his wife, and his maid-servants, and they bore children.

Maana Bwana alikuwa ameyafunga matumbo ya watu wa nyumbani mwa Abimeleki, wasizae, kwa ajili ya Sara mkewe Ibrahimu.

Mwanzo 20:18

For Yahweh had closed up tight all the wombs of the house of Abimelech, because of Sarah, Abraham's wife.